Johnson Matembo Mtanzania Mzalendo

Johnson Matembo Mtanzania Mzalendo TUONGELEE VYA KWETU......

02/11/2023
07/07/2022

...UKIONA UNASIKIA BARIDI UJUE WAZI HUNA NGUVU ZA K**E WALA ZA KIUME...🙁🙁😀😀

07/06/2021
19/07/2017
_______________ wahenga ______________
15/07/2017

_______________ wahenga ______________

G9t
14/07/2017

G9t

___________The  C. E. O him self__________
22/05/2017

___________The C. E. O him self__________

_________Wanawake banaaaa_________Tusaidie BaabaJamaa kaamka asubuhi kavaa track suit akamuasha mkeweMUME:Amka twende jo...
19/05/2017

_________Wanawake banaaaa_________

Tusaidie Baaba

Jamaa kaamka asubuhi kavaa track suit akamuasha mkewe
MUME:Amka twende jogging mke wangu? 😊

MKE: Alaaa kwa hiyo una maana mi tipwatipwa?😒

MUME: Hapana si hivyo jogging ni nzuri kwa afya. 😯

MKE: Kwa hiyo una maana mi mgonjwa? 😕

MUME: Basi yaishe endelea kulala🤗

MKE: Kwa hiyo unaniona mi mvivu sana sio?

MUME:Hujanielewa mpenzi wangu sikuwa na maana hiyo baby 😧

MKE:Kwa hiyo mie mjinga mpaka nashindwa kukuelewa?😷

MUME:Jamani mi sijasema hilo😞

MKE:Kwa hiyo mie muongo?

MUME:Chonde tusiendeleze haya asubuhi namna hii😣

MKE:Kwa hiyo mie ndio naendeleza ugomvi?😤

MUME:Sikia we lala mie naenda jogging.😵

MKE:Ndio zako hizo mambo yote unafanya peke yako hunishirikishi"🤐

MUME:Unajua nimeanza kusikia kizunguzungu

MKE: Unaona nikiongea kidogo unakimbilia kuumwa, mbinafsi sana wewe......

Jamaa nimemuacha kibarazani kwake amewasha kipisi cha bangi anapiga paf anatafakari la kufanya💭💭💭

Na !!!

________________Taarifa tu_______________....Soon ntàomba kazi hii aiseee.... Na  !!
16/05/2017

________________Taarifa tu_______________
....Soon ntàomba kazi hii aiseee....

Na !!

______________Neno la Usiku_____________....MAMA mmoja alienda kukaa nyumbani kwa mwanae kwa miezi miwili, ilikuwa ni ma...
15/05/2017

______________Neno la Usiku_____________
....MAMA mmoja alienda kukaa nyumbani kwa mwanae kwa miezi miwili, ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo kwani mara nyingi alipoambiwa alikataa k**a unavyojua wazee wengi hupenda kukaa vijijini.

Alikuwa anaumwa hivyo alilazimika kuja mjini kwaajili matibabu. Baada ya kupata nafuu alijiandaa kurudi kijijini, asubuhi kabla ya kuondoka alimuita mtoto wake na kumuambia.

"....Mwanangu una mke mzuri sana, anakupenda na anatabia nzuri, lakini huna furaha..." Mwanaea alishangaa kwani katika kipindi hicho cha miezi miwili alijaribu sana kuigiza ili Mama yake aone kuwa wanafuraha lakini wapi Mama aligundua kitu.

Alijitetea lakini Mama yake alimuambia ".....mwanangu, acha kumwaga kinyesi kwenye kitanda unacholala na mkeo, acha kumwagia mkeo kinyesi. Baba yako alifanya hivyo na alikufa kwa msongo wa mawazo, hakua na furaha katika ndoa yetu........"

Yule kijana alistuka zaidi kwani hakuwahi kumwaga kinyesi katika chumba chao achilia mbali kitandani. "... Huyu Mama ni mchawi nini mbona ananiambia maneno k**a haya?......". Aliwaza hivyo huku akimuangalia Mama yake kwa wasiwasi, kisha Mama yake akamuambia.

".......Baba yako alikuwa akininyanyasa sana, kila siku alikuwa akinisimanga na kunitukana, alikuwa akinipiiga sana......."

Mtoto alishangaa kwani katika maisha yake yote aliwaona wazazi wake wanafuraha.

"......Najua unashangaa lakini sisi wanawake ni wavumilivu, mama yake aliendelea kuongea, tunajua kuigiza, ndoa yetu haikuwa ya furaha, nilitamani kuondoka lakini kuna kitu kimoja kilinizuia, wewe na wadogo zako, nilijua k**a nikiondoka basi mateso aliyokuwa akinipa mimi atayageuzia kwenu. Ingawa haukuwa uamuzi sahihi lakini nilizoea ile hali.....

Baba yenu alidhani ananikomoa lakini haikuwa kweli, alikua anaumia kuliko mimi. Alipokuwa akinipiga mimi nilipata maumivu ya mwili lakini yaye alipata maumivu ya roho, alikuwa mpweke kwani ndoa haikuwa na furaha, mpaka siku anakufa Baba yako hakua na furaha.

Nimekaa kwako miezi miwili, mkeo anafuraha kwakua ana watoto, anacheka nao na kufurahi. wewe ukiingia ndani hata watoto wanakuogopa, unajifanya mbabe hivyo hakuna anayekusemesha, unakua mpweke na nakuona unaumia...

Alitulia kidogo kisha akaendelea. "Mwanangu kumnyanyasa mkeo nisawa na kummwagia kinyesi au kumwaga kinyesi kitandani, unaweza kukimwaga upande wake lakini jua harufu ya kinyesi haichagui pua, itaingia kwenye pua yake na itaingia kwako pia......

Mkeo anapokosa raha hakosi raha peke yake na wewe unakosa kwani hutakuwa na mtu wa kuongea naye, mtu wa kutaniana naye na mbaya zaidi nikuwa anapokufanyia kitu kizuri utahisi nikwakua anakuogopa si kwakuwa anakupenda.

Kila wakati unakuwa ni mtu wa mawazo tu, haikufanyi mwanaume zaidi kumnyanyasa mkeo bali inakufanya mwanaume mkatili. Nakuonea huruma mwanangu, badilika usije kufa k**a Baba yako mpweke. Baba yako alikua akinimwagia kinyesi kila siku ila wote hatukulala kwa amani kwani harufu ya kinyesi ilituathiri wote. Mama alimaliza kuongea akaaga.....

Kutwa nzima yule kijana aliwaza na kugundua kweli alikua hana amani, hakua akipata faida yoyote kumnyanyasa mkewe, uanaume wake haukuongezeka, sana sana alijihisi pungufu kwani hata kumridhisha mkewe alikua hamridhishi tena.

Siku iliyofuata alimfuata mkewe na kumuomba msamaha. Alimuomba waanze ukurasa mpya na mpaka sasa wanaishi kwa amani, wakikorofishana wanaongea na kiumaliza tofauti zako k**a watu wazima.

Hata wewe unaweza kuwa na furaha pia k**a utaamua kuchagua njia ya amani kusuluhisha tofauti zako na mwenza wako. Kummwagia kinyesi (kumpiga) hakutasaidia kwani mnalala kitanda kimoja........

Na !!!

14/05/2017

Under 17
Full time:

Gabon 1 - 5 Guinea (1st match)
Ghana 4 - 0 cameroon (2nd match)

Kesho serengeti boys muda saa 11 jioni tujitokeze kwenda kuiangalia huko Gaboni mpk kombe la dunia, mie nishafika Gaboni hapa!!!!

!!!

Address

P. O. BOX 50, , KILELENI SECONDARY, , HANDENI/TANGA
Handeni

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Johnson Matembo Mtanzania Mzalendo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Johnson Matembo Mtanzania Mzalendo:

Shortcuts

Share

Category