11/06/2021
Neno kindergarten linatoka kwenye lugha ya kijerumani
Kinder- watoto
Garten- bustani
Kwa maana hiyo neno kindergarten kwa kiswahili maana yake ni "bustani ya watoto" hii hujumuisha misamiati k**a Chekechea, shule ya awali au vidudu na haya maneno kwa lugha ya kiingereza huweza kuwa na maana sawa na maneno k**a Pre-school, day care,pre- primary or nursery school.
Chimbuko hasa la dhana ya elimu ya awali ni ujerumani a ilianzishwa na mwanafalsafa FRIEDRICK FROEBEL kwenye miaka ya 1800 kwa kutumia mawazo ya wanafalsafa wengine k**a JEAN JACQUES ROUSSEAU na JOHANN HEINRICH PESTALOZZI
Nchini Marekani kindergarten zimeanza kwenye miaka ya 1856
Barani Afrika shule za awali zililetwa na wakoloni kwa ajili ya watoto wao lakini baada ya uhuru wa nchi za Afrika kila nchi imekuwa na mkazo na sera yake kwenye elimu ya awali nchi k**a Afrika kusini na Kenya zimekuwa nchi za Mwanza kuwekeza kwenye eneo hili. Kwetu Tanzania elimu ya awali imeanza kwenye miaka ya 1980. Mwaka 2004 serikali ilianzisha mtandao wa maendeleo ya elimu ya awali yaani the Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN) ambapo kufikia mwaka 2015 77% ya watoto nchini walikuwa na uwezo wa kupata elimu ya awali.
Pamoja na mafanikio yaliyofikiwa bado zipo changamoto hasa kwenye hii elimu ya awali na ngazi nyingine za elimu nchini ambazo tutendelea kuzijadili siku hadi siku na tutapendekeza na kushauriana namna ya kukabiliana nazo hapahapa kwenye ukurasa huu.
Email: [email protected]