17/01/2026
MAOMBI YA MFUNGO YA MWANZO WA MWAKA 2026
2 - 31 January 2026
Neno la Mwaka: Nyakati za Kuburudishwa
Matendo ya Mitume 3:19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
MAOMBI YA KANISA
SIKU YA 16
Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda;
Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Mungu haangalii udogo wa kitu, udhaifu au unyonge bali Macho ya Mungu huangalia uaminifu wake. Na kwa sababu hio uaminifu wa Mungu unaweza kutoa kitu kikubwa, cha maana na cha thamani kati ya kidogo.
_ alikuwa mdogo machoni pake mwenyewe na kwenye kabila dogo lakini Mungu alimfanya kuwa mfalme.
_ alitolewa kwenye mazizi ya kondoo
alitolewa kwenye kujificha, kupepeta ngano na kwa udogo wa kabila lake alifanywa kuwa mwokozi wa Israeli
, Yusufu, Danieli, Mitume, Bwana Yesu pia alizaliwa kwenye Hori la ng'ombe lakini mwisho ameketi katika kiti cha Enzi cha Mungu baba.
Ombi: Baba tunaomba watu wa maana waanze kuinuka, Mdogo awe mkubwa, kidogo kiwe kikubwa, kinyonge kiwe na nguvu, Washirika wenye majibu kwenye maeneo mbali mbali, mitaa, miji na kitaifa, katika makampuni na Taasisi mbali mbali. Mungu alipe kanisa nguvu na uthabiti ili kusudi lake na uaminifu wake wa kuwavusha wengi zaidi litimie pamoja na kuleta uamsho kwenye kila Eneo.
Luka 12:32
Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.
Isaya 60:22
Mdogo atakuwa elfu,
Na mnyonge atakuwa taifa hodari;
Mimi, BWANA, nitayahimiza hayo wakati wake.
Isaya 9:1
Lakini yeye aliyekuwa katika dhiki hatakosa changamko. Hapo kwanza aliiingiza nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali katika hali ya kudharauliwa, lakini zamani za mwisho ameifanya kuwa tukufu, karibu na njia ya bahari; ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya mataifa.
Yohana 1:46
Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.
Isaya 9:7
Maongeo ya enzi yake na amani
Hayatakuwa na mwisho kamwe,
Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake;
Kuuthibitisha na kuutegemeza
Kwa hukumu na kwa haki,
Tangu sasa na hata milele.
Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Isaya 9:1_7 katika kifungu hiki kuna hizi hatua unyonge, changamko, Mavuno, uzao mwingi, maongezeko na ukuu
Omba; Mungu amkuze na Kumwongeza kila mmoja wetu, kiroho, kiuchumi, kimahusiano n.k na kututhibitisha kwa kuwa na matokeo ya kudumu. Kupanda na kushuka, kurudi nyuma, kuchoka na kuacha kusiwe fungu letu bali wivu wa Bwana uyatende yote haya kwenye kanisa na kwenye maisha ya mtu mmoja mmoja.
UMEBARIKIWA
ABC GLOBAL
TU ISHARA NA AJABU