Tafes Chuo Cha Mipango - IRDP Dodoma

Tafes Chuo Cha Mipango - IRDP Dodoma An Inter-denominational and Non- denominational Christian Organization ministering to students in universities and colleges in Tanzania

Tanzania Fellowship of Evangelical Students (TAFES-IRDP) began
since 2003 bearing the name Christian Union
(CU) then amended by the business meeting in
year 2005 and being called Mipango Fellowship
of Evangelical Students (MIFES). Finally on the 11th
business meeting seated on 15th June 2013 at
IRDP-main campus officially declared the
amendment of the constitution and thus
changing the name of the fellowship from MIFES
to TAFES-IRDP

Ibada ya makabidhiano ya uongozi iliyofanyika IRDP Furaha Hostel Campus
21/01/2015

Ibada ya makabidhiano ya uongozi iliyofanyika IRDP Furaha Hostel Campus

Uchaguzi wa viongozi wa TAFES IRDP 11/01/2015
21/01/2015

Uchaguzi wa viongozi wa TAFES IRDP 11/01/2015

HALLELUJAH! HII SI YA KUKOSA K**A UKO DODOMA!  Shalom! Ndugu mpendwa napenda kukukaribisha ktk nusu mkesha (HALF NIGHT) ...
30/12/2014

HALLELUJAH!
HII SI YA KUKOSA K**A UKO DODOMA!
Shalom!
Ndugu mpendwa napenda kukukaribisha ktk nusu mkesha (HALF NIGHT) wa kusifu, kuabudu na kumshukuru Mungu kwa ajili mwaka 2014. Na kuomba kwa ajili ya kuupokea mwaka mpya wa 2015
Muda: 2:00-7:30 usiku
Mahali: Chuo Cha Mipango - Mwl Nyerere Hall
Tarehe: 31 dec 2014
N:B. Usafiri wa kwenda na kurudi utakuwepo hapo chuoni kwako kuanzia saa moja(1:00) jioni.
Upatapo ujumbe huu mjulishe na mwenzako!
Imeandaliwa kwa ushirikiano wa jumuiya mbalimbali za Kikristo za wanafunzi kutoka vyuo vya Dodoma!

Saturday service done at IRDP Main Campus on 13th dec 2014Title: MAFUTA YA ROHO MATAKATIFU YANAVYOKUSAIDIA KUTUMIKA VIZU...
14/12/2014

Saturday service done at IRDP Main Campus on 13th dec 2014
Title: MAFUTA YA ROHO MATAKATIFU YANAVYOKUSAIDIA KUTUMIKA VIZURI KTK NAFASI YAKO...
Ministered by the servant of God; Mwl Awadhi Mwapololo from Dar es Salaam, Tanzania

THREE DAYS SEMINAR FROM 8-10th DEC 2014Title: Kudumu, Kukua na Kutembea katika Wokovu!Venue: CR 2
10/12/2014

THREE DAYS SEMINAR FROM 8-10th DEC 2014
Title: Kudumu, Kukua na Kutembea katika Wokovu!
Venue: CR 2

MIPANGO NIGHT OF BEGINNERS-FRESHERS on 5th dec 2014
10/12/2014

MIPANGO NIGHT OF BEGINNERS-FRESHERS on 5th dec 2014

Mipango night of beginners - Freshers on Friday! A HALF NIGHT OF PRAISE AND WORSHIP! don't plan to miss it!
04/12/2014

Mipango night of beginners - Freshers
on Friday!
A HALF NIGHT OF PRAISE AND WORSHIP!
don't plan to miss it!

ISAYA 40:31 ''bali wao wamngojeao BWANA watapata NGUVU MPYA; watapanda juu kwa mbawa k**a tai; watapiga mbio wala hawata...
15/10/2014

ISAYA 40:31 ''bali wao wamngojeao BWANA watapata NGUVU MPYA; watapanda juu kwa mbawa k**a tai; watapiga mbio wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu wala hawatazimia''

Nini kazi ya Upako Mpya(Nguvu Mpya) ambao Mungu anaachilia ndani yako!? kutokana na Isaya 40:31 ni...

1. Kukuhamisha KIWANGO kimoja hadi kingine cha kiroho(ktk kumjua Bwana), kihuduma(kiutumishi) na hata 'kiuchumi' ikiwa huo ni upako wa kiuchumi(torati 8:18) n.k
imeandikwa "...WATAPANDA juu kwa MBAWA k**a tai..."
ameufananisha UPAKO MPYA na MBAWA zinamwezesha tai kwenda juu na sote tunajua kuwa tabia moja wapo kubwa ya ndege aitwae tai ni kwenda hewani ''juu sana zaidi ya'' ndege wengine wote!
IKIWA UNAHITAJI KIWANGO KIPYA BASI WEKA MSISITIZO KWA MUNGU KUKUPA UPAKO MPYA KWA NJIA YA MAOMBI!
kwa hiyo ni sahihi kusema
"upako mpya" huleta "kiwango kipya"!

2. kukuongezea MWENDOKASI katika maisha yako ya kiroho!
Imeandikwa ''... watapiga MBIO ...''
kuna mahusiano kati ya 'mwendo kasi' wako wa kiroho na 'upako mpya' unaoachiliwa ndani yako!
huu ni upako unaokupa kupiga mbio, kwa hiyo ni sahihi kusema
"upako mpya" huleta "kasi mpya"!

3. kukusaidia KWENDA MWENDO MREFU bila kuchoka!
imeandikwa ''...watapiga mbio wala HAWATACHOKA...''
mara nyingi kuchoka ni matokeo ya kwenda mwendo mrefu kwenye maisha yako bila kukifikia kile unachoki-chuchumilia!
"upako mpya" huleta "ustahimilivu"!

4. kukusaidia ''kuthubutu kupiga'' hatua bila KUKATA TAMAA!
imeandikwa ''...watakwenda kwa miguu wala HAWATAZIMIA...''
WATAKWENDA - inawakilisha ''kuthubutu''
Kwa MIGUU - inawakilisha ''kupiga hatua''
HAWATAZIMIA - inawakilisha ''kuto-kukata tamaa''
"upako mpya" hukupa "subira"!

N.B;
BADALA YA KUJITUTUMUA KUPIGA HATUA BASI JITUTUMUE KWA NJIA YA MAOMBI KUTAFUTA UPAKO WA KUKUSAIDIA KUPIGA HATUA!
Ubarikiwe!

Shalom! kwanini utafute kuwa na vyote viwili (yaani hekima na ufunuo) na si kimoja pekee yake?Mithali 9:1 ''Hekima UMEIJ...
15/10/2014

Shalom! kwanini utafute kuwa na vyote viwili (yaani hekima na ufunuo) na si kimoja pekee yake?

Mithali 9:1 ''Hekima UMEIJENGA nyumba yake,...''

nyumba tunayoweza kuizungumza hapa sio physical house pekee!
bali kikubwa tasfiri zaidi Nyumba ni familia, Nyumba ni baba, mama, watoto na ndugu.
hekima kazi yake ni KUJENGA!

unaweza kuwa na ufunuo mzuri, ushauri mzuri na maarifa bora kabisa, lakini yasiwe msaada kwako au hata kwa watu wanaokuzunguka(nyumba yako)!
hekima huusaidia ufunuo ''kujenga'' bila hekima hata k**a ni ufunuo ni mzuri hauwezi kujenga kitu kizuri!
ndio maana zipo 'cases' zinazohusisha ufunuo kuharibu uhusiano wa watu, n.k
ushauri wako ili uwe ushauri wa kujenga unahitaji hekima!
hekima inakuchagulia kitu cha kusema ktk ulivyonavyo , mahali pa kusema pia hukuchagulia wakati wakusema!!

NI KWA JINSI GANI UNAIJENGA NYUMBA YAKO? SI KWA USHAURI PEKE YAKE BALI HEKIMA INAYOFANYA USHAURI UWE NA MAANA AU TIJA KWAO WASIKIAO!
Ubarikiwe!

Huu mstari unatupa kuona mambo yafuatayo!(i)HEKIMA inaweza ''kupungua'' k**a ndivyo basi pia inaweza kuongezeka!kwa hiyo...
14/10/2014

Huu mstari unatupa kuona mambo yafuatayo!
(i)HEKIMA inaweza ''kupungua'' k**a ndivyo basi pia inaweza kuongezeka!
kwa hiyo sio ajabu kuona hekima ikiwa tofauti na zamani ktk maisha yako, ama imepungua au imeongezeka maana yote mawili yanaweza kutokea!
(ii) HEKIMA inaweza ''kuombwa'' kwa njia ya maombi!
Maarifa ya Ki-Mungu pamoja na kwamba unaweza kuomba lakini msingi wake 'mkubwa' ni KUJIFUNZA tofauti na Hekima ya Ki-Mungu ambayo huweza kupatikana kwa njia ya MAOMBI! Mhubiri 12:9,10
(iii) MUNGU hutupatia kwa UKARIMU kile tunachomwomba!
(iv) N.k
MKARIMU ni mtu ambaye k**a anacho kile unachomwomba basi hawezi kuzuia(kukubania) kukupa IKIWA utamwomba!
Tunajua watu wengi tuna imani juu ya Mungu kuwa nacho kile tunachomwomba lakini kuna umuhimu wa KUONGEZA Imani yako kwa Kuamini kuwa Mungu si tu ANACHO lakini HUTOA kwa ukarimu kile ALICHONACHO unachomwomba!

HAITOSHI TU KUAMINI KUWA ''ANACHO'' BALI PIA KUAMINI KUWA ''HUTOA'' KILE ALICHONACHO tena kwa ukarimu!
ubarikiwe unapotafakari ujumbe huu!

Address

Classroom 2 (CR 2)
Dodoma
IRDP-MAINCAMP

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tafes Chuo Cha Mipango - IRDP Dodoma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Tafes Chuo Cha Mipango - IRDP Dodoma:

Shortcuts

Share