Livestock Training Agency-LITA

Livestock Training Agency-LITA Mifugo ni Mali

Udahili #2026.2027
30/05/2026

Udahili #2026.2027

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, akihutubia Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, katika M...
08/05/2026

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, akihutubia Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, katika Mkutano wa Kumi na Tatu (13) wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), uliyofanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar, Mei 8, 2026 Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) ambaye ni Mte...
08/05/2026

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) ambaye ni Mtendaji Mkuu LITA, Dkt. Pius Lazaro Mwambene, akitoa neno la Utangulizi katika katika Mkutano wa Kumi na Tatu (13) wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo, uliyofanyika katika Ukumbi wa St. Gaspar, Mei 8, 2026 Dodoma.

Salamu   Mosi 2026
01/05/2026

Salamu Mosi 2026

Pasaka Njema 2026
05/04/2026

Pasaka Njema 2026

Eid Mubarak 2026
21/03/2026

Eid Mubarak 2026

Timu ya wataalam wa uandaaji mitaala kutoka LITA ikiendelea na kazi ya kuandaa mtaala tarajiwa wa Teknolojia  Uzalishaji...
11/02/2026

Timu ya wataalam wa uandaaji mitaala kutoka LITA ikiendelea na kazi ya kuandaa mtaala tarajiwa wa Teknolojia Uzalishaji wa Kuku, kwa kushirikiana na AERES PC kutoka Uholanzi, DRTE, na NACTVET kwa kuzingatia maudhui yaliyobainishwa na wadau mbalimbali kutoka sekta ya Mifugo hususani sekta ndogo ya Kuku.

Salamu za Pongezi
11/02/2026

Salamu za Pongezi

Heri ya Siku ya Kuzaliwa #2026
27/01/2026

Heri ya Siku ya Kuzaliwa #2026

WARSHA YA KUANDAA MTAALA WA TEKNOLOJIA ZA UZALISHAJI WA KUKU YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAMWakala wa Vyuo vya Mafunzo ya...
22/01/2026

WARSHA YA KUANDAA MTAALA WA TEKNOLOJIA ZA UZALISHAJI WA KUKU YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) imeandaa na kuendesha warsha ya kuanza mchakato wa uandaaji wa Mtaala wa Teknolojia za Uzalishaji Kuku kwa kufanya Upembuzi wa mahitaji ya stadi zinazohitajika kufundishwa kwa Wataalam katika mnyororo wa thamani wa kuku. Lengo la Warsha hii ni kuchambua na kupata maoni ya wadau kuhusu stadi na ujuzi (situational analysis) katika tasnia ya kuku.

Warsha hiyo imefanyika Januari 20, 2026 katika Ukumbi wa Wakala ya Maabara ya Vetenari Tanzania (TVLA), na imewakutanisha Wadau muhimu wakiwemo Wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi; Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Uholanzi; Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Wawakilishi kutoka Vyama vya Wafugaji Kuku nchini; Makampuni yaliyopo katika mnyororo wa thamani wa kuku (Silverland, Alvine, Interchick, Falcon); Wataalam kutoka MSM; Wafugaji; Wakufunzi kutoka LITA na Vyuo Binafsi.

Akizungumza katika warsha hiyo, Naibu Mkuu wa Chuo LITA, Bw. Balija Luyombya amewasilisha malengo na matarajio ya Warsha kuwa ni kupata maoni na kupitisha stadi zinazohitajika na wadau zitakazojumuishwa katika Mtaala. Naye Dkt. Edward Mneda wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), aliwasilisha mwaongozo na hatua za kuzingatia katika uandaaji wa mitaala.

Aidha, katika maelezo ya awali Bw. Sebastian Shilangalila Mwakilishi kutoka Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani alieleza kuwa warsha hii ni hatua muhimu kwa wadau kutoa maoni kwa kuzingatia mahitaji halisi ya sekta ya mifugo, hususan katika kuandaa wataalam wenye stadi, ujuzi na weledi wa kushauri, kujiajiri, kuajiri katika mnyororo wa thamani wa kuku. Hivyo, aliwaasa wadau kushiriki kikamilifu na kutoa maoni yatakayotumika katika kuandaa mtaala.

Address

Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Livestock Training Agency-LITA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Livestock Training Agency-LITA:

Shortcuts

Share