Institute of Rural Development Planning (IRDP)

Institute of Rural Development Planning (IRDP) Ukurasa Rasmi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP)

TANZIA
25/03/2026

TANZIA

عيد مباركEid Mubarak
21/03/2026

عيد مبارك
Eid Mubarak

Siku ya Tatu ya Mafunzo – Mradi wa HEETMafunzo ya kuwajengea uwezo timu ya Mradi ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijiji...
18/03/2026

Siku ya Tatu ya Mafunzo – Mradi wa HEET

Mafunzo ya kuwajengea uwezo timu ya Mradi ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yanaendelea kwa mafanikio, ambapo leo ni siku ya tatu.

Washiriki wanaendelea kupata ujuzi na mbinu muhimu kuhusu maandalizi ya makabidhiano ya mradi pamoja na taratibu za kufunga mradi wa HEET kwa ufanisi.

Mafunzo haya yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro, yakiwa na lengo la kuimarisha usimamizi bora wa mradi na kuhakikisha uendelevu wake.

ZANA ZA KISASA ZIKAWE CHACHU YA ONGEZEKO LA THAMANI YA ZAO LA MWANI NCHINI-Mhe. NderianangaNa; Sweetbetter Njige-TangaVi...
18/03/2026

ZANA ZA KISASA ZIKAWE CHACHU YA ONGEZEKO LA THAMANI YA ZAO LA MWANI NCHINI-Mhe. Nderiananga

Na; Sweetbetter Njige-Tanga

Vikundi vya Wakulima wa zao la Mwani Wilayani Mkinga vyahimizwa kutumia fursa ya uwepo wa zana za kisasa za kuchakata zao la mwani kuongeza thamani ya zao hilo

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Mheshimiwa Ummy H. Nderiananga (Mb) Machi 16, 2026 katika hafla ya makabidhiano ya mashine mbili zenye uwezo wa kusaga kilo 500 kwa saa na kaushio moja lenye uwezo wa kukausha tani nne kwa mara moja kwa vikundi vya wakulima katika Kijiji cha Kichaka Mimba, wilayani Mkinga mkoani Tanga.

“Lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo ili kuhakikisha uchumi wa blue una kuwa kupitia mazao ya bahari na unaimarisha mnyororo wa thamani kuanzia kwenye kuzalisha hadi kuchakata mazao haya hivyo basi, nitoe rai kwenu wakulima kuhakikisha mnatumia zana za makaushio na mashine kwa ufanisi ukubwa ilimuweze kukuza uchumi wa kaya moja moja na vikundi vya wakulima kwa ujumla” Alisema Mhe. Nderiananga (Mb)

Aidha, Mheshimiwa Nderiananga amewashukuru UNDP na Serikali ya Japani kwa kushirikiana na Serikali kutengeneza mazingira wezeshi kwa vikundi vya wakulima wa mwani.

Akitoa utangulizi wa mradi, Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa Prof. Juvenal Nkonoki amesema tathmini ilibaini changamoto za mbinu duni za kilimo, ukosefu wa miundombinu na elimu kwa vikundi, na kuanza kutatuliwa kupitia mafunzo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kwa ufadhili wa Serikali ya Japani na UNDP.

Naye mkuu wa Wilaya ya Mkinga Mhe. Gilbert Kalima amewashukuru wafadhili na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuratibu upatikanaji wa zana za kuchakata mwani zitakazoongeza thamani ya zao hilo na kuwainua kiuchumi wakulima huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano na mazingira rafiki kwa wakula na wadau ili kufikia malengo.

Mratibu wa Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kupitia Elimu ya Juu (Higher Education for Economic Transformation-HEET), Bw.  S...
17/03/2026

Mratibu wa Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kupitia Elimu ya Juu (Higher Education for Economic Transformation-HEET), Bw. Said Abdallah Panga (kulia), akifuatilia Mafunzo ya Maandalizi ya Makabidhiano na Kufunga Mradi, ambapo leo ni siku ya pili ya mafunzo hayo.

Mafunzo haya yanaendeshwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) na yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) uliopo Morogoro.

Lengo la mafunzo haya ni kuwaandaa wadau wa mradi katika hatua za mwisho za utekelezaji, ikiwemo taratibu za makabidhiano, tathmini ya mafanikio, na kufunga rasmi mradi wa HEET.

Siku ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo timu ya miradi ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini juu ya Maandalizi y...
17/03/2026

Siku ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo timu ya miradi ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini juu ya Maandalizi ya Makabidhiano ya Mradi na Kufunga Mradi wa HEET yakiendelea katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.

MRADI WA  HEET WALETA CHACHU KATIKA KUIMARISHA UTENDAJI KAZINa; Andrew Mallya - MorogoroMradi wa Higher Education for Ec...
16/03/2026

MRADI WA HEET WALETA CHACHU KATIKA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI

Na; Andrew Mallya - Morogoro

Mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET) umeendelea kuwa chachu katika kuimarisha utendaji kazi na usimamizi wa miradi katika taasisi za elimu ya juu nchini kikiwemo Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.

Hayo yameelezwa leo, Jumatatu tarehe 16 Machi 2026, na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Hozen Mayaya, wakati akifungua mafunzo ya Maandalizi ya Makabidhiano ya Mradi na Kufunga Mradi yanayofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), mkoani Morogoro.

Wakati huo huo Profesa Mayaya ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukipatia Chuo hicho fedha za maendeleo. “Ninapenda kutumia fursa hii kuishukuru sana Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; kwa kuendelea kukiimarisha Chuo chetu kwa kukipatia Fedha za maendeleo kupitia mradi wa HEET. Kupitia mradi huu tunajenga jengo la kisasa la masuala ya taaluma, na tumenunua vifaa vya kufundishia na kujifunzia”, alisema Profesa Mayaya na kuongeza “ Vile vile tumehuisha mitaala yetu ili kukidhi soko la ajira, pamoja na kuwapatia watumishiv mafunzo ya muda mrefu na mfupi”


Aidha, Profesa Mayaya amewataka washiriki kuwa makini katika kipindi chote cha mafunzo ili kupata stadi muhimu za usimamizi wa mradi hususan katika hatua za mwisho za makabidhiano na kufunga mradi ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa kwa ufanisi na matokeo yaliyotarajiwa yanadumishwa.

Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) yanafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia leo.

Washiriki wa mafunzo hayo wanatoka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini ambao ni timu ya mradi pamoja na wakandarasi na washauri elekezi wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi wa HEET.

Mratibu wa Kanda kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Faraja Msangi, ametembe...
12/03/2026

Mratibu wa Kanda kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Faraja Msangi, ametembelea Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa-Mwanza, na kupokelewa na mlezi wa wanafunzi Bw. Peter Majula.

Ziara hiyo imelenga kujadili masuala ya Dawati la Jinsia katika ufuatiliaji wa mradi wa O3+ (Our Rights, Our Lives, Our Future Plus) unaoendesha mafunzo ya elimu ya Ujinsia (CSE), kuhamasisha huduma bora za afya kwa Vijana, na kujenga mazingira salama yanayounga mkono haki na usawa Vyuoni.

Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kinaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha Vijana wanapata mazingira salama na wezeshi ili kufanikisha ndoto zao wakati wote wawapo Masomoni.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Provident Dimoso (kushoto), akiendesha kikao cha 165 cha K...
09/03/2026

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Profesa Provident Dimoso (kushoto), akiendesha kikao cha 165 cha Kamati ya Menejimenti ya Chuo leo Jumatatu, tarehe 9 Machi 2026, katika Ukumbi wa Menejimenti uliopo Jengo la Kwanza la Taaluma, Kampasi Kuu Dodoma.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa za masuala ya taaluma na utawala kwa kipindi cha mwezi Januari na Februari 2026.

Wakati huo huo, kikao hicho kimetaarifiwa kuwa katika jitihada za kukifanya chuo hicho kuwa cha kimataifa, Chuo kimesaini makubaliano ya ushirikiano na Mananga Institute of Management Development ya nchini Eswatini.

Pia, kinaendelea na mchakato wa makubaliano ya mashirikiano na Chuo Kikuu cha Kilimo cha China.

Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa Chuo hicho kimekuwa mwanachama wa Inter-University Council for East Africa (IUCEA). Kwa muktadha huo, wanataaluma wa Chuo hicho wamehimizwa kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na uanachama huo, ikiwemo ushirikiano wa kitaaluma, tafiti za pamoja, pamoja na programu za kubadilishana uzoefu na vyuo vingine ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki.

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026Wanawake wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wameungana na Wanawake wengine Duniani k...
09/03/2026

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026

Wanawake wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wameungana na Wanawake wengine Duniani kote kuadhimisha Siku ya
Wanawake Duniani Jumapili tarehe 8 Machi 2026.

Kwa Mkoa wa Dodoma maadhimisho hayo yamefanyikia Kijiji cha Mbande wilaya ya Kongwa ambapo watumishi wanawake wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kampasi Kuu - Dodoma wameshiriki.

Kwa upande wa Mkoa wa Mwanza maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Nane Nane vya Nyamhongoro ambapo watumishi wanawake wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa - Mwanza cha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini nao wameshiriki.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni; “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”.

Daima tunasema, Kupanga ni Kuchagua.

HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI. “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”   💪💪💪    ...
08/03/2026

HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

“Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”

💪💪💪

Address

Miyuji
Dodoma
138DODOMA,

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:30
Tuesday 08:00 - 15:30
Wednesday 08:00 - 15:30
Thursday 08:00 - 15:30
Friday 08:00 - 15:30

Telephone

+255262963037

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Institute of Rural Development Planning (IRDP) posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Institute of Rural Development Planning (IRDP):

Shortcuts

Share