Tuzungumze_Kuhusu_Wewe

Tuzungumze_Kuhusu_Wewe hili ni jukwaa maalumu la kutoa elimu kuhusu maisha na ukuaji pamoja na masuala ya afya na mwonekano!

Forever Aloe Vera Gel – Chaguo Bora kwa Afya na Ustawi wa MwiliForever Aloe Vera Gel ni kinywaji cha asili chenye virutu...
21/02/2025

Forever Aloe Vera Gel – Chaguo Bora kwa Afya na Ustawi wa Mwili

Forever Aloe Vera Gel ni kinywaji cha asili chenye virutubisho vingi vinavyosaidia kuboresha afya yako kwa ujumla. Imetengenezwa kutoka kwa gel halisi ya aloe vera, mmea unaofahamika kwa faida zake nyingi za kiafya.

Kwa Nini Uhitaji Forever Aloe Vera Gel?

Husaidia Mfumo wa Hupumuaji na Usagaji Chakula

Inasaidia kusafisha na kulainisha utumbo, kupunguza matatizo k**a gesi tumboni, kiungulia, na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula.

Inasaidia kuweka uwiano mzuri wa bakteria wenye manufaa tumboni, hivyo kuimarisha afya ya mfumo wa usagaji chakula.

Hutengeneza Kinga ya Mwili

Aloe vera ina vitamini k**a C, E, na beta-carotene, ambazo zinasaidia mwili kupambana na magonjwa na kuimarisha kinga.

Pia ina amino acids na enzymes zinazosaidia mwili kujijenga na kujikinga dhidi ya maambukizi.

Husaidia Ngozi na Nywele

Huimarisha ngozi kwa kupunguza vipele, chunusi, na ukavu wa ngozi kwa sababu ina sifa za kuzuia uvimbe na kuongeza unyevunyevu wa ngozi.

Inasaidia nywele kuwa na afya, kuzuia kukatika na kudumisha unyevu wa ngozi ya kichwa.

Husafisha Mwili (Detoxification)

Inasaidia kutoa sumu mwilini, kuboresha mzunguko wa damu, na kuongeza nishati mwilini.

Husaidia ini na figo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi katika kuondoa taka mwilini.

Husaidia Kudhibiti Uzito

Inasaidia katika kupunguza uzito kwa kuongeza kasi ya mmeng’enyo wa chakula na kutoa sumu mwilini.

Husaidia kudhibiti hamu ya kula na kuongeza nishati mwilini.

Hutunza Mifupa na Viungo

Inasaidia kupunguza maumivu ya viungo na magonjwa k**a arthritis kwa sababu ya sifa zake za kupunguza uvimbe.

Jinsi ya Kutumia

Unashauriwa kunywa 30-120ml kila siku, peke yake au kuchanganya na juisi nyingine upendayo. Matumizi ya mara kwa mara huleta matokeo bora zaidi.

Kwa Nini Uchague Forever Aloe Vera Gel?

Imetengenezwa kwa Aloe Vera Halisi – Haina kemikali hatari, haina ladha bandia wala viambato vyenye madhara.

Imeidhinishwa Kimataifa – Ina vyeti vya ubora kutoka mashirika makubwa ya afya duniani k**a International Aloe Science Council (IASC)

Jinsi Ya Kupata Matokeo Unayoyataka...Mbinu ya 2&3_________________2. Tafuta Njia Zitakazokufanikisha Upate Kile Unachok...
08/06/2023

Jinsi Ya Kupata Matokeo Unayoyataka...
Mbinu ya 2&3
_________________

2. Tafuta Njia Zitakazokufanikisha Upate Kile Unachokitaka

Kujua unachokitaka siyo kigezo cha kupata matokeo unayoyataka.
Hivyo basi ili kupata matokeo unayoyataka unatakiwa uweke wazi njia zitakazopelekea upate matokeo hayo!

Kumbuka hakuna matokeo ambayo hujitengeneza yenyewe pasipo kichocheo kitakachopelekea matokeo hayo…

Na, ndiyo maana hata katika hesabu huwezi kupata jibu pasipo kutumia njia, jaribu tu kuwaza na kuwazua, sasa jibu litakujaje ilihali hakuna njia uliyoitumia ili uweze kulipata?

Kwa mfano katika hoja ya kwanza nilisema kwamba ninachokitaka ni “kuongeza pato langu la mwezi lifikie 300,000/=” kwa mantiki hiyo itabidi niweze kuja na njia ambazo zitanisaidia ili niweze kuyapata matokeo hayo ninayoyataka.

Kwa mfano ninaweza kuja na njia zifuatazo: kutafuta kazi nyingine, kuongeza mifereji ya kipato changu kwa kuwekeza pesa yangu katika maeneo mbalimbali, kutafuta elimu ya fedha na uwezekaji, kuweka akiba yangu binafsi pamoja na kujifunza kuhusu bajeti.

Unatakiwa kujua kwamba kujua njia itakayokusaidia ili upate kile unachokipata ni jambo la msingi, kwani njia ni muhimu zaidi kuliko hata kile unachokitaka…

Kwamba kupitia kutumia njia kadhaa utapata matokeo ya kile unachokitaka, na endapo hautaazimia njia kadhaa hakuna chochote kile utakachokipata.

Jambo moja unalopaswa kuepuka hapa, ni kutaka kutumia kila njia, unatakiwa kujua kwamba siyo kila njia itakuongoza na kukupeleka kule unakotaka ufike.

Unatakiwa uchague njia sahihi zitakazokusaidia uweze kupata matokeo unayoyataka.

Hata hivyo kabla hujaichagua jaribu kujiuliza je hii njia itanisaidia kweli kupata yale matokeo ninayoyataka?

Kumbuka siyo kila njia itakusaidia upate matokeo unayoyataka, hivyo basi ili upate matokeo unayoyataka huna budi kuja na njia sahihi zitakazopelekea matokeo hayo!

3. Badilisha Mfumo Wako Wa Kuamini
Ukishaweka wazi kile unachokitaka ni lazima uamini kwamba utakipata.
Na, ndiyo maana kanuni ya kuamini inasema kwamba, “chochote kile utakachokiamini kuhusu wewe na dunia yako kitafanyika kwako pamoja na dunia yako k**a uaminivyo”
Hii inamaanisha kwamba, ukiamini kwamba haya matokeo nitayapata utayapata kweli kwa sababu umeamini kwamba utayapata.
Kumbuka “nawe utapokea kwa kadri ya uaminivyo”

Hata hivyo ukija katika maandiko matakatifu mwinjili marko 11:24 anasema kwamba “kwa sababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”

Unatakiwa kujua kwamba sala ni jambo lolote lile unalolitamani uweze kulipata, hii inamaanisha kwamba hata yale matokeo unayoyataka ni k**a sala kwa sababu ni jambo unalotaka ulipate…

Kwa mantiki hiyo ukiweza kubadilisha mfumo wako kuamini na kuona kwamba utalipata nawe utalipata kwani kwa muda mrefu ulikuwa ukilitamani ulipate…

Mbali na hilo ukisoma waebrania 11:1 neno la BWANA linasema kwamba “basi Imani ni kuwa na hakika yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”.

Chukua hili, “kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo”, kwamba unatakiwa uwe na hakika juu ya kile unachokitaka ambapo mwisho wa siku utakipata hali ambayo itakusaidia uweze kupata yale matokeo unayoyataka!

My friend unatakiwa uamini katika kuamini! Kwani nawe utapokea kwa kadri ya uaminivyo!
Badili mfumo wako wa kuamini, baada ya hapo amini kwamba kile unachokitaka utakipata, na endapo utaamiini hivyo nawe utakipokea.
Na, unatakiwa kudumu katika Imani hiyo muda wote!

Ahsante Sana Kwa Kuwa Mwanafamilia Wa Masomo Haya!
Somo Lihusulo Jinsi Ya Kupata Matokeo Unayoyataka Litaendelea kesho!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e, Mwl, Mwandishi Muelimishaji Katika Eneo La Maendeleo Binafsi, Life Coach And Consultant!

Unaweza ukawasiliana na Mimi kupitia Whatsapp no +255744284329 au tembelea blog yangu kwa kuandika ekingunge.blogspot.com

Fahumu Kuhusu Dondoo Zitakazokusaidia Utengeneze Fikra Za Uwezekezaji ...Jambo la kwanza unalopaswa kujua ni kwamba haku...
05/04/2023

Fahumu Kuhusu Dondoo Zitakazokusaidia Utengeneze Fikra Za Uwezekezaji ...

Jambo la kwanza unalopaswa kujua ni kwamba hakuna binadamu ambaye huzaliwa akiwa na Fikra fulani, bali kila mtu amekuwa na mtizamo wa kuona mambo kwa namna fulani kwa sababu kuna fikra zilizomtengeneza aone mambo hayo kwa namna hiyo...

Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba hivyo ulivyo pamoja na hali uliyonayo kiuchumi ni kutokana na wewe mwenyewe!

Hivyo basi kabla sijaenda mbali zaidi somo la leo ngoja tufafanue vipengele vifuatavyo, ni matumaini yangu kwamba vitapanua uelewa wako...

Fikra: ni ile namna ya kufikiri, hali ya kutizama mambo kwa namna fulani pamoja na kuyapa tafsiri fulani...

Uwekezaji: ni mfumo utakaokusaidia uweze kuzalisha pesa zako na kuzifanya ziwe nyingi zaidi!

Aseti: ni kile kitu ambacho thamani yake inazidi kuongezeka kadri muda unavyozidi kusonga mbele...
Au
Aseti: ni kitu ambacho kinaingiza pesa mfukoni mwako! Hii inamaanisha aseti inafanya pesa iendelee kuongezeka mfukoni mwako!

Liability: ni kile kitu ambacho thamani yake inazidi kushuka kadri miaka inavyozidi kuongezeka!
Au
Liability: ni kile kitu ambacho kinatoa fedha mfukoni mwako kila iitwapo leo!

Hii inamaanisha endapo utakuwa ni muumini wa kununua liability utakuwa unaufukuza utajiri na kuukaribisha umaskini maishani mwako!

Je mpaka hapa wewe ni mfuasi wa kununua aseti au liability!

Tuendelee na somo kwa kuangalia mambo matatu ambayo watu hufanya wakipata fedha!

Tumia mambo haya kujipima k**a una fikra za uwezekezaji au una fikra ufujaji...

1. Ufujaji pesa!

Ni jambo ambalo hufanywa na watu wengi wasio na busara!
Hapa mtu anakuwa hana mpangilio wa manunuzi bali ananunua kila anachokiona...
Hawa ndiyo wale watu ambao wakishika pesa huwa zinakuwa ni k**a zinawawasha!

Yaani wanakuwa wanaendeshwa na pesa mwisho wa siku wanajikuta hawafanyi kitu cha maana kwenye pato walilotengeneza..

Je wewe ni mfujaji? Je ukipata fedha kitu cha kwanza huwa unawaza ufanyie nini?
Ndugu Unapaswa kujua kwamba kuna kesho inakuja ambayo huijui!

Kuna kesho inakuja ambayo hata uwezo wa kufanya kazi hutakuwa nao!

Kuna kesho inakuja ambayo uwezekano wa kutengeneza fedha k**a leo hautakuwa nao!

Je unajipangaje kwa ajili ya kesho yako?

Tambua kwamba fedha unayoingiza leo ndiyo mbegu yako ya kesho!
Ndiyo maana wahenga walisema akipandacho mtu ndicho akivunacho!

Je unapanda nini kwa ajili ya kesho yako?

2. Kutumia pesa!

Hapa ni pale mtu anapotumia fedha zake zote kwenye masuala ambayo huonekana ni ya msingi kwa upande wake huku akiathiri kesho yake!

Watu wanaondondokea kwenye kufanya tabia hii ni wafanyakazi! Yaani anatumia pato lake lote kulipa Kodi, kulipa ada, bili pamoja na matumizi mengine!

Hata hivyo mbali na kuwa hufanya matumizi sahihi lakini kosa lao ni moja tu wanatumia fedha zote pasipo kuwekeza hata shilingi mia!

Ndugu mtu mwenye busara anajua kwamba kuna kesho inakuja!

Je wewe nawe upo kwenye kundi la kutumia tu pasipo kuwekeza?

Huna budi kujiandaa na kujipanga kwa ajili ya kesho yako!

Unatakiwa utokomeze kufanya kabisa tabia ya kuwa mtumiaji tu na kuwa muwekezaji!

3. Uwekezaji wa pesa:

Hii ni tabia ambayo hufanywa na watu wachache sana!

Hapa mtu anakuwa ametambua kwamba kuna kesho inakuja!
Unatakiwa kujua kwamba hakuna atakayekupangia kesho yako pasipo uhusika wako mwenyewe!

Ndugu unatakiwa kujua kwamba kitengo cha uchumi katika maisha yako kinakutegemea wewe!

Hivyo ukishindwa kuwekeza utakifanya kitengo hiki adimu kife!

Wekeza pesa zako!

Hautakiwi kuishia tu kuwa mfujaji au mtumiaji bali kuwa mwekezaji!

Mtu mwenye busara huwekeza PESA zake kwa sababu anatambua kwamba kuna Kesho inakuja!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e: mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!

Kwa msaada zaidi wasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329

05/04/2023

Fahamu Kuhusu Sababu Ambazo Huathiri Fikra Za Binadamu...

Jambo la kwanza unalopaswa kujua ni kwamba hivyo ulivyo ni matokeo ya Fikra zako mwenyewe. Pia, unatakiwa kujua kwamba maisha ya kila binadamu ni matokeo ya fikra zake mwenyewe...

Ukiachilia mbali hilo unatakiwa kujua kwamba unaona dunia na vitu vilivyomo kutokana na wewe ulivyo, na siyo jinsi dunia na vitu vyote vilivyomo vilivyo!

Kadhalika, unaipa dunia na vitu vyote vilivyomo tafsiri fulani siyo kwamba vinastahili kupewa tafsiri hiyo, ila ni kutokana na wewe ulivyojipa tafsiri...

Hii inamaanisha kwamba unatizama vitu kwa angle ya Fikra zako na siyo kwa angle ya vitu hivyo k**a vilivyo!

Unachotakiwa kuchukua hapa ni kwamba, fikra zimewaweka watu wengi kwenye ukomo, uhaba na mateso pamoja na kuwafanya watu hao wawe wazito katika kuchukua maamuzi hali ambayo inawafanya wapige hatua ndogo kimaisha...

Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba huwezi ukaenda Mbali ya zaidi ya pale ulipoishia kujiona!

Mbali na hilo unatakiwa kujua kwamba duniani hakuna vikwazo halisi zaidi ya vikwazo unavyojiwekea mwenyewe kupitia mtindo wako wa kufikiri!

Hivyo basi ukitaka kubadili maisha yako anza kubadili fikra zako kwanza! Yaani change your thinking change your life!

Katika makala hii fupi utajifunza sababu ambazo Huathiri Fikra Za Binadamu...
Hauhitaji kufanya mengi chukua kiti Kaa then relax, k**a una soda na popcorn zichukue then anza kula na kunywa huku ukishushia na content makini sana kuwahi kuandikwa....

Hata hivyo zifuatazo ni sababu hizo:

1. Historia ya Malezi...
Kuna watu wameathirika kifikra kutokana na athari za malezi...
Na hii ni kutokana na manyanyaso, kukemewa, kudharauliwa, kukosolewa sana, kauli za kukatishwa tamaa, kuitwa majina ya hovyo, kufananishwa na viumbe vya ajabu pamoja vipigo vya hapa na pale, watu wengi wamejikuta wakitengeneza fikra za kuona hawastahili na hawawezi kufika popote pale!

Unatakiwa kujua kwamba historia yako imebeba mengi sana kuhusu maisha yako na ndiyo imekufanya uwe hivyo ulivyo!

Mbali na hilo kuna watu wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa eti kwa vile kwenye ukoo wanaotokea hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa...

Pia kuna watu wengine utawakuta wakisema siwezi kufanikiwa kwa sababu niliambiwa mimi ni mjinga, nimezaliwa kwenye familia maskini, mimi ni mweusi, Mimi ni mfupi, familia yetu ina laana na mikosi n.k

Ndugu wakati uliokubalika ndiyo Sasa, unachopaswa kufanya ni kufuta fikra zote hizo hasi, ili kubadili kabisa historia ya maisha yako!

Unatakiwa kujua kwamba wewe unaweza na ulizaliwa ili uje uwe mtu mkuu, unayestahili uishi maisha yenye furaha, amani na mafanikio!

2. Mazingira.
Ni nguvu isiyoonekana ambayo humtawala binadamu kifikra, kimawazo, kitabia, kimienendo pamoja na kimtizamo!

Unatakiwa kujua kwamba unaweza ukawa na mawazo makubwa lakini k**a mazingira uliyopo siyo supportive hakuna cha maana utakachofanya.

Pia kuna baadhi ya watu wamekufa kifikra kwa sababu ya kuzungukwa na mazingira yaliyojaa uhaba na ukomo...

Mbali na hilo kuna watu wanajiona hawawezi, hawastahili, hawatafika popote pale na hawatabadili chochote kile kwa sababu mazingira waliyopo yamewafanya wawe hivyo!

Unatakiwa kujua kwamba mazingira yana Nguvu sana katika kupima kila kinachotokea maishani mwako!

Ukitaka kujua Nguvu ya mazingira fanya hili, mchukue papa Halafu muweke kwenye chumba kidogo, katika kukua kwake papa huyo hatakua mkubwa kuzidi chumba alichomo, ila mchukue papa huyohuyo halafu muweke kwenye bahari kubwa atakua mkubwa mpaka uatashangazwa...
Hii inamaanisha kwamba mazingira ya bahari hayajampa papa Ukomo wa kukua ukilinganisha na mazingira ya chumbani alimowekwa mara ya kwanza...

Ni wakati wa kuhama na kwenda kwenye mazingira mengine, k**a mazingira uliyopo siyo rafiki Kwako!

3. Watu wako wa karibu!
Kwa mujibu wa tafiti za kisaikolojia kuwahi kufanyika zimeonesha kwamba hivyo ulivyo ni wastani wa watu sita unaoshinda nao kila siku!

Hii inamaanisha kwamba k**a watu wako unaoshinda nao watakuwa ni waoga, hawajiamini, ni watu hasi, basi na wewe utakuwa k**a wao...

Hivyo unachopaswa kufanya ni kuepuka mazima kushinda na watu hasi kwani na wewe mwisho wa siku na wewe utajikuta unakuwa k**a wao!

Ndugu epuka kushinda saa zima na mtu wa kushinda naye dakika moja..
Epuka kushinda siku saba na mtu wa kushinda naye masaa saba..
Epuka kushinda 30 na mtu wa kushinda naye siku tatu...
Epuka kushinda siku 365 na mtu wa kushinda naye siku 30..

Epuka! Epuka! Epuka! Kwa usalama wa maisha yako!
Kumbuka watu wako wa karibu ni k**a ngazi! Kwamba wanaweza kukupandisha au kukushusha !
Daima chagua watu hawa kwa Makini ili uwe na fikra chanya..

4. Maono Yako..
Kuna watu wameathirika kifikra kutokana na kuwa maono hafifu. Maono ni nini labda? .... ndiyo upo sahihi maono ni picha kamili ya maisha yajayo ya mtu fulani.
Hii inamaanisha kwamba k**a hauna maono bado hujaanza kuishi... Na utaanza kuishi siku ukipata maono kuhusu maisha yako!

Watu wengi wanaishi lakini hawana picha kamili juu ya kile wanachotaka wakikamilishe maishani mwao...
Kutokana na hilo hujikuta wanaishi ili mradi tu wanaishi ila hakuna kitu cha maana wanachoyafanyia maisha yao.

Sasa k**a una maono hafifu utatoa wapi fikra nzuri?
Na utatengeneza fikra nzuri ili upate nini?
Ndugu ni huu ni wakati wa kutengeneza maono na kuanza kuyapigania!

5. Exposure!
Kuna watu wameathirika kifikra kwa Sababu exposure yao ni ndogo sana kwa watu!

Najua hujanielewa namaanisha hivi kuna watu wana uwezo wa kufanya mambo makubwa ila hawaoneshi watu wengine kile ambacho wanaweza kukifanya, kutokana na hilo wanaishia kujiona ni watu wa kawaida tu...

Huenda kuna mtu yupo anaangalia jumbe zangu hizi na anajua sana kuandika lakini haandiki, mtu huyo manake ana uwezo lakini hajiexpozi kwa watu...

Pia usiwe reluctant wa mazingira ongeza exposure yako kwa watu kwa kujaribu kufanya mambo mbalimbali katika mazingira tofauti tofauti!

Na huu ndiyo mwisho wa somo la leo!

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e: mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!
Unaweza kuwasaliana nami kupitia Whatsapp no+255744284329

*Kile Unachokijua Ndicho Kitapima Umbali Utakaoenda Kimaisha...* Hivi unafahamu kwamba moja ya adui tishio sana wa binad...
05/04/2023

*Kile Unachokijua Ndicho Kitapima Umbali Utakaoenda Kimaisha...*

Hivi unafahamu kwamba moja ya adui tishio sana wa binadamu katika kizazi hiki tulichonacho leo ni ujinga?

K**a ulikuwa hujui basi leo ukweli unaenda kufahamika...

Unatakiwa kujua kwamba hata baba wa taifa hayati Mwl J. K. Nyerere aliutaja ujinga k**a miongoni mwa wale maadui watatu wakubwa wa taifa letu pendwa la Tanzania...

Hii inamaanisha ujinga lilikuwa janga la taifa toka enzi hizo...
Lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ndivyo tatizo hili linavyozidi kukua na kwenda hatua mbaya zaidi...

mategemeo yangu makubwa yalikuwa ni kuisha kwa tatizo hilo cha kushangaza zaidi ni kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda hali imekuwa kinyume chake...
The situation is getting worse as long as the days moves on...

Moja ya kitu ambacho natamani hata leo kingeondoka kwenye jamii yangu ni ujinga..

Natamani ujinga ungeondolewa kwa nguvu zote kutokana na giza linalosababishwa na ujinga hasa kwenye Fahamu za watu wengi...

Unatakiwa kujua kwamba ujinga ni giza nene lililotanda Totoro kwenye Fahamu za Watu wengi.
Hata hivyo ni ukweli usio na kipingamizi kwamba, popote pale palipofunikwa na giza hakuna chochote kile cha maana kitakachotokea...

Na hii kwa sababu giza huashiria kuwa hakuna Nuru, na k**a hakuna nuru manake hakuna matumaini.
Hata hivyo k**a hakuna matumaini manake hakuna maisha, na k**a hakuna maisha manake hakuna maendeleo...

Huenda ukawa unajiuliza huyu kijana mdogo anamaanisha nini?
Okay mimi k**a kijana mdogo namaanisha kile kinachomaanishwa...😃

Anyway tuache masihara maana yangu ni kwamba kuna baadhi ya shida, matatizo, changamoto pamoja na hali ambazo wengi wetu tunapitia zinasababishwa na ujinga wa kutokujua.

Hii inamaanisha kwamba ukosefu wa maarifa ndiyo kimekuwa chanzo cha matatizo hayo yote...

Kuna baadhi ya mambo hayatakaa yabadilike katika maisha yetu na jamii yetu k**a tutaendelea kubaki na kiwango kilekile cha ufahamu...

Hii inamaanisha kwamba tutaendelea kupitia matatizo yaleyale kizazi hadi kizazi k**a hatutatokomeza ujinga katika jamii yetu...

Huenda nikawa nazungumza jambo ambalo ni geni kwako (yaani hujui maana ya ujinga)... Hata hivyo sipo hapa kuibua na kufanya mjadala uwe mkubwa, Bali nipo hapa kuweka sawa uelewa wako kuhusu neno ujinga...

Kwa mujibu wa Brian Tracy katika kitabu chake kiitwacho "change your thinking change your life", yeye anafafanua ujinga k**a ile hali ya kutokujua na kutokujua K**a hujui! Tumeelewana?

Mbali na hilo siyo mbaya endapo tukafafanua maana ya neno mjinga...

Kwa tafsiri nyepesi mjinga ni yule mtu ambaye hajui na hajui k**a hajui...

Imagine haujui kuhusu jambo fulani au tatizo fulani au changamoto fulani, au hali fulani unayopitia na ubaya zaidi ni kwamba haujui k**a hujui😀😀

Tukirudi katika uumbaji tutaona kwamba Mwenyezi Mungu alimpa kila mtu akili na utashi!

Hivyo basi sitakosea endapo nitasema Mungu hakuumba ujinga, ila ujinga ni matokeo ya juhudi za kutokujifunza zinazofanywa na binadamu mwenyewe..

Na ndiyo maana ukisoma biblia takatifu utakutana na andiko linaosema *"watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"*

Hii inamaanisha kwamba maarifa ulishapewa ila kutokana na ujinga umejikuta ukikosa kabisa maarifa ya kukusaidia ili uishi kweli ya maish Yako, ndiyo maana kila upande unakutana na vipingamizi na vikwazo k**a vyote!

Mpenzi msomaji nakala hii fupi na ikawe k**a alamu ya kuamsha fahamu zako nawe uanze kupiga vita ujinga...

Unatakiwa kujua kwamba kile Unachokijua ndicho kitapima umbali utakaoenda kimaisha!

Hii inamaanisha kwamba ukijua vingi utaweza kufika mbali kimaisha!
Ilihali ukijua vitu vichache hutafika mbali kimaisha...

Hata hivyo Unatakiwa kujua kwamba mbinu kubwa ya kupambana na ujinga ni kupitia kujifunza!

Na ndiyo maana sisi wanafalsafa tunaamini kwamba siku utakayoacha kujifunza ndiyo siku ya kifo chako, Kwani utajizika kwa kujichimbia kaburi lako mwenyewe...

Na hii ni kwa sababu ubongo wako utaanza kuzalisha mawazo yaliyokufa au yaliyopitwa na wakati!

Kutokana na ukweli huo hapa ndipo huwa tunapata aina mbili za watu!

Aina ya kwanza ya watu ni wale watu ambao wanaishi lakini wamekufa.
Na aina ya pili ya watu ni hujumuisha watu ambao wamekufa lakini bado wanaishi!

Ukitaka uishi ukiwa hai huna budi kujifunza...

Yes boss jifunze kujifunza!
Unatakiwa kujua kwamba unaweza kujifunza kupitia social medias (Facebook, Whatsapp, Instagram, Twitter n.k), kusoma vitabu, kuhudhiria semina mbalimbali, kusikiliza audio books, kujifunza kupitia podcast, CD, audios mbalimbali n.k.

Ndugu unatakiwa ufahamu kwamba kila eneo la maisha yako linahitaji uwe na maarifa fulani ili uweze kulikabili ipasavyo...

Kumbuka kadri unavyojua kuhusu jambo fulani ndivyo na hofu ya kufanya jambo hilo inavyopungua, ikiwa kadri usivyokuwa na uelewa wa jambo hilo ndivyo na hofu ya kufanya jambo hilo inavyoongezeka!

Wakati mwingine mimi na wewe hapo hatuna budi kufahamu kwamba, hatuna: umaskini, hali ngumu, maradhi, changamoto, dhiki pamoja na matatizo mengine mengi, bali tuna ujinga mwingi vichwani mwetu kuhusu mambo hayo!

Kwamba hatuna uelewa wa kutosha juu ya mambo hayo..

Ndugu huenda ukawa umeona pengine labda una mikosi, nuksi, laana, .nk.
Na huenda ukawa umehama mpaka mtaa, kijiji, wilaya mkoa, mpaka nchi unayoishi na umeona hakuna kitu kinachobalika mbali na kuwa umehama...
Hata hivyo huenda ukawa umebadili mpaka kazi na biashara na haujaona mabadiliko yoyote yale usijue shida nini!
Kumbe tatizo halisi lipo kichwani mwako!

Unahitaji uamuzi mmoja tu... Ambao ni huu hapaa...

ANZA KUJIFUNZA!
YAANI JIFUNZE KUJIFUNZA!

Kesho nitakuletea aina tano za ujinga zilizopo miongoni mwetu...

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e; mwalimu, mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant!

Unaweza kuwasiliana nami kupitia Whatsapp no +255744284329

21/02/2023

*Jinsi kanuni ya visaco ilivyobadili maisha yangu...*

Hivi unafahamu kwamba katika maisha ni ngumu sana kufanikiwa pasipo kutumia kanuni?

Unatakiwa kujua kwamba maisha yetu yanaongozwa na kanuni ndiyo maana hata kwenye hesabu kuna kanuni ya jibu sahihi ila hakuna kanuni ya kosa!

Wengi wetu huwa tunashindwa kufanikiwa katika mambo yetu kutokana na kushindwa kutumia kanuni hii!
Unatakiwa kujua kwamba kuna uwezekano wa kufanikiwa katika jambo lolote lile Kwa asilimia 100% endapo utatumia kanuni hii!

*Ufafanuzi wake.*
Kanuni ya visaco ni ufupisho wa maneno matatu k**a ifuatavyo:
👇👇👇👇👇
VI= VISION
SA= SACRIFICE
CO= CONSISTENCE.

Yafuatayo ni mambo ya msingi yanayopatikana kwenye kanuni hii!

1. Vision (maono)
Maono ni picha kamili ya maisha ya mtu yajayo! Unatakiwa kujua kwamba mtu ambaye hana maono hajaanza bado kuishi ila ataanza kuishi pindi akipata maono.

Mbali na hilo huwa tunapanga malengo fulani kulingana na maono tuliyonayo!
Je unaona nini kuhusu kesho ya maisha yako?
Je unaona nini kuhusu kipato chako cha fedha siku zako zijazo?

Unaalikwa utengeneze malengo makubwa kwani ndiyo yatachochea hamasa na nguvu za kupambana zaidi!

2. Kuwa tayari kulipa gharama (sacrifice)
Kwa chochote kile kizuri utakachokuwa unakitaka katika maisha yako tambua kuna gharama utapaswa kulipa!

Unatakiwa kujua kwamba kuna gharama za aina mbalimbali, k**a vile: gharama ya muda, nguvu, pesa, maarifa, hisia n.k.

Jambo moja unalopaswa kujua ni kwamba ukiona kuna matokeo mazuri juu ya jambo fulani jua kuna mtu alikubali kuingia gharama ili kupata matokeo hayo!

Pia, usiogope maumivu unayoyapata bali ogopa kukwepa maumivu yaliyobeba mafanikio yako!

Kumbuka ni kheri kuumia leo ili ufurahie kesho kuliko kufurahia leo na kuja kuumia kesho.
Hebu jisacrifice kulipa gharama my mentees!

3. Fanya kwa mwendelezo (consistence)

Hapa unapaswa kujenga nidhamu ya hali ya juu ili ufanye masuala yote unayopaswa kuyafanya kwa mwendelezo.
Kuna watu ambao huanza kufanya jambo fulani kwa moyo wao wote lakini hujikuta wakiishia njia!
Watu hawa hukosa sanaa ya mwendelezo katika mambo yao ambapo mwisho wa siku hujikuta wakiishia njiani.

Unatakiwa kujua kwamba dakika moja ya uzembe wa kutokufanya jambo fulani inaweza kuharibu kabisa matokeo makubwa ambayo umeyahangaikia kwa muda mrefu!

Linda sana kila ulichonacho, huku ukifanya juhudi zaidi kutafuta kile usichonacho!

Hivyo ndiyo unavyoaswa utumie Kanuni ya visaco kubadili maisha yako!

Yaani pata maono makubwa
Halafu jitoe sadaka kukamilisha maono hayo,
Mwishowe kuwa tayari kufanya kila siku ili upate matokeo unayoyataka (yaani fanya jambo fulani kila siku)

Ndimi Emmanuel Samuel King'ung'e mwandishi, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi, life coach and consultant..
+255744284329

UKWELI KUHUSU WEWE NA UWEZO ULIOZALIWA NAO..👇👇👇👇👇👇Hakuna mwanadamu anayezaliwa akiwa empty ndani yake...Kila mtu huzaliw...
19/02/2023

UKWELI KUHUSU WEWE NA UWEZO ULIOZALIWA NAO..
👇👇👇👇👇👇
Hakuna mwanadamu anayezaliwa akiwa empty ndani yake...
Kila mtu huzaliwa na uwezo asilia ambao Mungu alimuumbia ili umsaidie katika kuishi kwake hapa duniani..

Kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba huwa hatugundui hili kwa vile kuna mifumo imetuficha juu ya uhalisia wa jambo hilo.

Mbali na hilo utakuta mtu unaona k**a watu ambao wamefanikiwa kuiishi uwezo wao ni watu wenye bahati kumbe hapana bali walitangulia kupata taarifa sahihi kuhusu uwezo wao wakatumia taarifa hizo vizuri kubadili maisha yao.

Habari njema ni kwamba hata wewe utaenda kugundua uwezo uliolala ndani yako pasipo kutumikaa hali itakayobadilisha kabisa historia ya maisha yako.

Unachopaswa kufahamu ni kwamba ndani yako unamiliki uwezo mkubwa sana ambao endapo utaamua kuutumia utavuta mafanikio maishani mwako na utapata kila unachohitaji..

N B
Hakuna ambaye hazaliwi akiwa hana uwezo fulani ndani yake. Sote tunazaliwa nao lakini mifumo tunayokutana nayo inakuwa siyo rafiki hali inayopekelea uwezo wetu uweze kufa.

Katika sehemu hii utajifunza kuhusu uwezo mkubwa sana unaoumiliki lakini umebaki umelala tu ndani bila kutumika..

Nimekuombea kwa Mungu ili tukimaliza kipengele hiki ugundue uwezo wako, hata hivyo sitapendeza kuona unaishia tu kugundua uwezo wako lakini nitapendezwa zaidi endapo utatumia uwezo huo unaoumiliki.

KILA MTU NI GENIUS...

Kila mtu ni jenius katika eneo fulani...
Mungu alipokuumba alikuumbia uwezo fulani ambao unapaswa uutumie ili uweze kuishi maisha yaliyo na furaha, amani na mafanikio..

Kitu unachopaswa kujua ni kwamba unamiliki uwezo mkubwa sana ndani yako ambao uliumbwa ili ukusaidie katika kuliishi kusudi la kuumbwa kwako pamoja na kutekeleza masuala mbalimbali yahusuyo maisha yako..

Kwanini unajiona huwezi?... ndiyo uko sahihi ni kwa sababu mifumo imeshindwa kugundua uwezo wako..
Yaani umepimwa kwenye eneo ambalo ugenius wako haupo huko..

Kwa mfano badala ya samaki kupimwa uwezo wa kuogelea, yeye anapimwa uwezo wa kukwea miti..

Kwa mfano shuleni unapimwa uwezo wa kuzungumza na kuhesabu tu ili hali uwezo wako wewe upo kwenye uimbaji..

Vipii K**a uwezo wako ungetambulika mapemaa.

Katika sehemu hii utajifunza ugenius/uwezo ulionao pamoja na kazi ambazo unafaa kufanya kutokana na uwezo unaoumiliki..

FAHAMU UTAFITI WA HOWARD GARDENER KUHUSU UWEZO BINADAMU HUZALIWA NAO..

Kutokana na utafiti uliofanywa na Charles handy pamoja na Howard Gardner mwaka 2012 uliolenga kuchunguza uwezo ambao kila mwanadamu huzaliwa nao...
Kwa mujibu wa utafiti huo yalipatikana maeneo kumi ya uwezo ambayo kila binadamu huzaliwa nao...

Nitakuwa natuma uwezo wa eneo moja pamoja na kazi unazoweza kufanya kutokana na uwezo huo..

Lakini kabla sijafunga sehemu hii ya UTANGULIZI jiulize haya:
Je unaufahamu uwezo ulionao?
Je wewe ni bora katika eneo gani?
Ni kitu gani ambacho unapenda sana kukifanya?
Ni jambo gani unalopenda sana kulifanya?
Ni kipi ambacho huwa unahisi ni rahisi sana kwako kukifanya?

Tukutane siku nyingine.
Naitwa Emmanuel Samuel King'ung'e
Ni mwalimu, mwandishi, copywriter's, Mentor, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi & life consultant..

For anything wasiliana nami kupitia Whatsapp no 0744284329

Hata Mimi Ilinishangaza....______________Hivi unafahamu kwamba huu ulimwengu tunaoishi umegawanyika katika sehemu mbili ...
12/02/2023

Hata Mimi Ilinishangaza....
______________
Hivi unafahamu kwamba huu ulimwengu tunaoishi umegawanyika katika sehemu mbili zinazokamilishana katika utendaji kazi?
Huenda ukawa unaishi kwenye dunia ambayo huijui vizuri ndiyo maana mambo kwako yamekuwa yanakuendea kombo...
Unatakiwa kujua kwamba dunia yako imegawanyika katika sehemu mbili yaani Ulimwengu wa Kiroho na Ulimwengu wa Kawaida...

UFAFANUZI WAKE...

ULIMWENGU WA KIROHO
👇👇👇👇👇👇👇👇
Huu ni ulimwengu unaohusu vitu visiovyoonekana..
Hata hivyo huu ndiyo ulimwengu ambao vitu huanzia kutokea. Hivyo basi unatakiwa kujua kwamba ulimwengu huu wa kawaida (wa vitu vinavyoonekana) unatawaliwa na Ulimwengu wa Kiroho).
Kwa mantiki hiyo chochote kinachotokea katika ulimwengu wa kawaida ni lazima kianze kutokea ulimwengu wa kiroho kwanza!

👇👇👇👇👇👇👇👇
Kutokana na hilo ili ufanikiwe katika jambo lolote lile ni lazima uweze kuumiliki ulimwengu wa kiroho vizuri, ili hilo jambo litokee katika ulimwengu wa kawaida...
Kitu kimoja unachopaswa kujua ni kwamba mambo yote hutendekea kwenye ulimwengu wa kiroho kwanza ndiposa huthibitika katika ulimwengu wa kawaida..
Mbali na hilo watu wengi wamekuwa wakipuuza ulimwengu wa kiroho wasijue kwamba kufanya hivyo ni kosa kubwa sana..
Kumbuka kwamba endapo utafanya jambo ambalo halijaachiliwa kwenye ulimwengu wa kiroho halitafanikiwa!

👇👇👇👇👇👇👇👇
Mpendwa suala la kiroho siyo la kupuuzia kabisa!
Unatakiwa kujua kwamba Unaweza ukapuuza suala hili kadri uwezavyo lakini viumbe vya rohoni visikupuuze kabisa!
Kuna watu wanaanzisha biashara zinakufa, kuna watu kila wakianzisha mahusiano yanaishia kuvunjika, kuna watu huwa hawadumu kazini, kwa ufupi niseme kila wanachajaribu kufanya kinakuja na matokeo kinyume chake..
Leo nakusihi kwamba uanze kuutawala ulimwengu wa kiroho kwanza.. yaani anza kuomba kibali rohoni kwanza ndiposa utaweza kuutawala ulimwengu wa kawaida..

👇👇👇👇👇👇👇
Unatakiwa kujua kwamba vita ya roho ipiganwe kiroho..
Siyo inatokea vita ya kiroho halafu wewe unapigania katika ulimwengu wa kawaida..
Hutokuwa tofauti na mtu anayezima moto kwa kutumia petroli..
Mpendwa jitahidi kuumiliki ulimwengu wa kiroho vizuri..
Patana na Mungu wako kwa kuomba kibali mbele kwake.
Kumbuka jambo lililopata kibali kwenye ulimwengu wa roho hakuna kitacholizuia kwenye ulimwengu wa kawaida..

ULIMWENGU WA KAWAIDA..
Huu unahusu vitu vinavyoonekana..
Huu ndiyo ulimwengu tunaoishi na kufanya shughuli mbalimbali..
Sasa basi ili kufanikiwa katika ulimwengu huu ni lazima uweze kuutawala ulimwengu wa kiroho..
Ndiyo maana awali nilisema kwamba huna budi kuutawala ulimwengu wa kiroho vizuri ili kila utakalolifanya lipate kibali na liweze kufanikiwa..
Kumbuka mamlaka utakayokuwa nayo kwenye ulimwengu huu yatategemea kibali kutoka ulimwengu wa kiroho.
Pia, ni muhimu kufahamu kwamba hakuna chochote kitakachotokea katika ulimwengu huu k**a hakitapata kibali kwenye ulimwengu wa kiroho...

Naitwa Emmanuel Samuel King'ung'e...
Mimi ni mwalimu, mwandishi, copywriter's, Mentor, mshauri, muelimishaji katika eneo la maendeleo Binafsi & life consultant...
Nimemaliza zangu kutoa Somo!
Unaweza ukawasiliana nami kupitia Whatsapp no+255744284329.

Address

Dodoma

Telephone

+255744284329

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tuzungumze_Kuhusu_Wewe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Tuzungumze_Kuhusu_Wewe:

Shortcuts

Share