Lusako Empire

Lusako Empire karibuni katika ukurasa huu. Nitawahabarisha taarifa mbali mbali kuhusu masuala ya Utu, Haki za Binadamu, Siasa, Pamoja na Umajumui wa Africa 🌍

Alphonce Lusako .M. alias Emekha ikhe, ni Mwanafunzi niliyefukuzwa chuo kikuu cha Taifa “UDSM” Mnamo tarehe 14.11.2011 Nikiwa natetea haki za wanafunzi wenzangu nchini, mzee wangu anaitwa Alphonce Mwamwile, mama yangu anaitwa Joyce Mwamwile, pia nina wadogo zangu watano ambao kwa majina ni Grace, Gelitha, Meshaki, Majaliwa, na Glory bila kumsahau kaka yangu mpendwa Fredrick. Mimi binafsi nimezaliw

a mkoani Mbeya, Tukuyu kijiji cha Ipagika mnamo tarehe 5-11-1988, nimesoma shule ya msingi Mapambano mkoani Mbeya, shule ya sekondari Samora Machel, iliyopo mkoani Mbeya na hatimaye kidato cha tano na sita katika shule ya Sangu High school. Mwenyezi mungu hakunitupa na umaskini wangu akanifanikisha kuja chuo kikuu cha Taifa “Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam” nikafukuzwa chuo mnamo tarehe 14/11/2011, nikiwa mwaka wa tatu kwa kuongoza maandamano tarehe 11/11/2011, ya kuwatetea wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao hawakudhaminiwa mikopo nchini.Mnamo mwaka 2013 oktoba nikajiunga na chuo kikuu huria nikichukua shahada ya sheria “LLB” wakati kesi ya madai zidi ya utawal a wa chuo kikuu cha Dar es salaam, bado inaendelea mahak**a kuu.

02/01/2026
01/01/2026
01/01/2026

Nimesoma HUKUMU ya Kesi ya THADEY KWEKA ambayo imetolewa jana kinyemela hata bila yeye mwenyewe kujitetea au kutetewa na Mawakili wake tangu kuk**atwa kwake, Ninasikitika Kuona kwamba hata Mahak**a kupitia Hakimu imejielekeza Vibaya Kutoa HUKUMU husika Raia Wanategemea Mahak**a itende Haki na...

UTAWALA WA SHERIA, HAURUHUSU VYOMBO VYA UCHUNGUZI NA MAHAKAMA, KUVUNJA HAKI ZA KIKATIBA NA SHERIA, KATIKA UTOAJI HUKUMU ...
31/12/2025

UTAWALA WA SHERIA, HAURUHUSU VYOMBO VYA UCHUNGUZI NA MAHAKAMA, KUVUNJA HAKI ZA KIKATIBA NA SHERIA, KATIKA UTOAJI HUKUMU ZAKE (Kesi ya THADEY KWEKA)

Nimesoma HUKUMU ya Kesi ya THADEY KWEKA ambayo imetolewa jana kinyemela hata bila yeye mwenyewe kujitetea au kutetewa na Mawakili wake tangu kuk**atwa kwake, Ninasikitika Kuona kwamba hata Mahak**a kupitia Hakimu imejielekeza Vibaya Kutoa HUKUMU husika

Raia Wanategemea Mahak**a itende Haki na sio kushirikiana na Vyombo Vya Uk**ataji na Uchunguzi kuminya Haki za KIKATIBA za Mtuhumiwa k**a ambavyo nitaeleza Juu ya Sakata la THADEY KWEKA k**a nyaraka zinavyojifafanua, binafsi nitaandika kwa ufupi na straight to the point

Kitendo cha Ofisi ya DPP kufungua kesi dhidi ya Mtuhumiwa (Thadey Kweka) ya kuitaka Mahak**a kutoa Amri dhidi ya KWEKA ili atoe Nywila(Password) yake ili Polisi na Ofisi ya DPP kufanya Uchunguzi, na kesi Kusikilizwa na Mahak**a hata bila Mtuhumiwa kupewa wito ili kuwepo kwa utetezi au kutetewa na Wakili wake, Kunaibua maswali Mengi ya kisheria dhidi ya Vyombo Vya Uchunguzi pamoja na Mahak**a yenyewe

Mosi, Kesi umesikilizwa Upande mmoja kwa hati ya dharura bila mtuhumiwa wala Wakili wake kujulishwa kwa wito wa Mahak**a huku kesi iliyofunguliwa ikiwa Inter-Parte Application (Kwamba Mtuhumiwa alipaswa kupewa wito kwa utetezi) na sio Exparte Application (Kwamba kesi isikilizwe Upande mmoja kulingana na nyaraka zilizofailiwa

Ukisoma Wito wa Mahak**a( Chamber summons) hauonyeshi kwamba kesi hii ilikuwa ya Kusikilizwa Upande mmoja (Exparte Application) hivyo, Thadei alipaswa kuwakilishwa na Wakili au kujiwakilisha katika utetezi wake ili Kutekeleza Haki ya Asili ya Kusikilizwa inayolindwa na Katiba ya Nchi kabla ya Mahak**a Kuja na Uamuzi uliotolewa

Bahati Mbaya sana Hakimu aliyetoa Uamuzi anakili kwamba kesi hii ilikuwa kwa hati ya dharura ili isikilizwe Upande mmoja kinyume na nyaraka zilizowasilishwa Mahak**ani na Hakimu anaamua kesi husika bila kutii Katiba ya Nchi na Sheria zake k**a nitavyofafanua hapa;

Mahak**a hazina Mamlaka ya ku-dis regard Haki za Msingi za Kikatiba mathalani haki ya Faragha (Right to privacy) bila Kutoa Haki ya Kusikilizwa kwa Mtuhumiwa (Principle of Natural Justice) k**a ambavyo Hakimu alivyojielekeza vibaya katika Uamuzi wake unaopswa kukatiwa Rufaa haraka iwezekanavyo

Pia Kifungu cha 32 cha Sheria, Cyber Crime Act, licha ya kwamba Kifungu hiki kimeipa Mamlaka Mahak**a Kutoa Amri husika, Sheria husika haijaipa Mamlaka Kufanya Maamuzi kwa KUVUNJA Sheria na Katiba ya Nchi, hususani kukinzana na matakwa ya Katiba juu ya Haki ya Kusikilizwa (Fair hearing) kabla ya uamuzi

Ifahamike kuwa, Polisi na DPP hawezi Kumk**ata Mtuhumiwa kwa tuhuma hewa za jinai ( kupublish Taarifa za UONGO (False nformation) bila kuzitaja in specific k**a Kifungu cha 32 cha Sheria ya Cyber crime Act kinavyotaka

Ni Bahati mbaya sana Hakimu huyu wa Mahak**a(RMC) ametoa HUKUMU ya Amri ya Mtuhumiwa Kutoa nywila zake bila kujua ziitwazo Taarifa za UONGO ni zipi ambazo zilipelekea Mtuhumiwa kuk**atwa k**a Sheria inavyotaka

Ni takwa la Sheria zetu kwamba,Mahak**a katika Kutoa HUKUMU au Uamuzi wake haswa katika kesi ya Jinai inapaswa kuongozwa kanuni ya kuthibitisha bila Shaka (Prove Beyond Reasonable drought), kwenye hili Mahak**a imejielekeza Vibaya hivyo Uamuzi husika unapaswa kukatiwa Rufaa haraka

Hatuwezi tukawa na Mahak**a ambazo Hakimu anaamua kesi ya Jinai bila kujua in specific( details za kosa (criminal offence), bila kumpa Haki Mtuhumiwa kujitetea au kutetewa na Wakili wake (Fair hearing) na Kutoa Maamuzi

Hii ruling inapaswa kukatiwa Rufaa haraka, Ni Muhimu Mahak**a zetu kujiongoza vyema katika Kulinda Haki za Binadamu ambazo zinalundwa na Katiba ya Nchi yetu

30/12/2025

FUNGA MWAKA NA TUNDU LISSU

WATANZANIA ni Watu Wema sana, Wanaendelea kutuma Salamu kwa Upendo. Anyway 3M now;

Wengi tulitamani kwenda gerezani Ukonga kumsalimia Mhe Tundu AM Lissu, lakini ilishindikana. Hatukuruhusiwa kuingia gerezani. Tuliishia getini, tukarudi nyumbani kinyonge.

Dola imewekwa utaratibu mgumu sana, na kuanzia Desemba 5 hadi leo, hali imekuwa mbaya zaidi.
Maisha ya upweke na mateso gerezani ni magumu sana. Na Mhe Tundu Lissu anapitia hali hii ya kutengwa dunia – haoni jua wala nuru, kwa miezi 9 sasa.

Hii imeathiri hata yeye kufikia huduma za kijamii, si tu chakula, bali pia taarifa za familia yake, Chama chake CHADEMA, na hata hali ya kisiasa nchini – ikiwemo kusoma kupitia magazetu au mazungumzo na ndugu na jamaa zake.

Ili kumuunga mkono katika giza nene alilomo, tunakualika ushiriki “MASAA 48 YA FUNGA MWAKA NA TUNDU LISSU (Baba wa Gen Z).”

Gen Z wanafunga mwaka na Mtetezi weo, na sisi Watanzania tuungane kumtumia salamu za mwisho wa mwaka, tumtie moyo ili aanze Mwaka mpya kwa ujasiri mkubwa.

K**a ambavyo Mhe Lissu amejitoa kwaajili ya Taifa letu, tunalazimika kumkimbilia katika wakati ambao anatuhitaji zaidi.

Tuioneshe dunia maana halisi ya “NGUVU YA UMMA” kwa kuchangia chochote ulicho nacho.
Mwenyezi Mungu akubariki sana.

ASANTENI SANA.

Address

Dar Es Salam
P.O.BOX3814,MBEYATOWN

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lusako Empire posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Lusako Empire:

Shortcuts

Share