College of Business Education - CBE

College of Business Education - CBE The origin of the College of Business Education (CBE) is closely linked to the history of the Nation itself. His Excellency, J.K.

It was soon after Independence on 9th December 1961, that the newly independent state found itself in need of trained personnel to Commercial and It was soon after Independence on 9th December 1961, that the newly independent state found itself in need of trained personnel to Commercial and Industrial activities. At that time there were very few nationals with commercial education and expertise. T

he need to train nationals for the commercial sector therefore gave birth to a business training institute in the country. In 1965 the establishing Act of the College, Act of Parliament No. 31 of 1965 was enforced. The said Act gave the College its legal status as an autonomous institution with its Governing Body. The duties of the Governing Body were to govern and administer the College activities under the Ministry responsible for Trade. Nyerere, the first President of the United Republic of Tanzania officially opened the new College in January 1965. The College was officially named the “College of Business Education” (CBE).

23/08/2026
23/08/2026

📚 WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU 2026 🎓💡

Karibu kushiriki nasi katika Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, tukibeba kaulimbiu ya kuendeleza elimu, kukuza ujuzi na kuchochea ubunifu kwa maendeleo ya Taifa. 🇹🇿

📅 15–24 Agosti, 2026
📍 Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Tanga

Tembelea banda la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kujifunza zaidi kuhusu programu zetu, ubunifu, teknolojia na fursa mbalimbali za kielimu. 🎓✨

Prof. Nombo Avutiwa na "Double Degree" CBEAtoa Rai kwa Vyuo vingine Kuiga MfanoKatibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na T...
20/08/2026

Prof. Nombo Avutiwa na "Double Degree" CBE

Atoa Rai kwa Vyuo vingine Kuiga Mfano

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekipongeza Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kuanzisha programu ya Business Administration (Double Degree) inayotolewa kwa ushirikiano kati ya CBE na Southwestern University of Finance and Economics (SWUFE) hivyo mwanafunzi atasoma kwa miaka miwili CBE - Tanzania na miaka miwili SWUFE nchini China.

Prof. Nombo ameshauri vyuo vingine nchini kujifunza kutoka CBE namna ya kuanzisha na kutekeleza programu za Double Degree, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kitaaluma katika kuongeza fursa na ubora wa elimu ya juu nchini.

Aidha, Prof. Nombo amepongeza ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa CBE na kuwasisitiza kuendelea kubuni suluhisho zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii. Amehimiza wanafunzi kuzingatia zaidi mahitaji halisi ya jamii ili bunifu zao ziwe na tija na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Alipowasili katika banda la CBE, Prof. Carolyne Nombo alipokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Udahili, Ndugu Patroba Chaulo, ambaye alimweleza huduma, programu za masomo pamoja na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Chuo na CBE.

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, yanayoendelea katika ...
20/08/2026

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Tanga

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali  Mkoani Tanga walifika kujifunza kuhusu uchoraji katika Banda la CBE, wakati wa Maadhi...
20/08/2026

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali Mkoani Tanga walifika kujifunza kuhusu uchoraji katika Banda la CBE, wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Tanga.

Viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara wakishiriki hafla ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, U...
20/08/2026

Viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara wakishiriki hafla ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu tarehe 18 Agosti 2026 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Tanga. Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda.

Mkurugenzi wa Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Godfrey Bukagile, anayemwakilisha Mkuu wa Chuo, Prof. Ed...
17/08/2026

Mkurugenzi wa Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Godfrey Bukagile, anayemwakilisha Mkuu wa Chuo, Prof. Edda Tandi Lwoga, ametembelea Banda la CBE kuona huduma mbalimbali zinazotolewa pamoja na bunifu za wanafunzi wa Chuo hicho, leo Agosti 17, 2026, katika Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu jijini Tanga.

Wananchi waliojitokeza kwenye Banda la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakisikiliza maelezo kuhusu shughuli mbalimbali ...
17/08/2026

Wananchi waliojitokeza kwenye Banda la Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakisikiliza maelezo kuhusu shughuli mbalimbali na kujionea bunifu za wanafunzi wa Chuo hicho, leo hicho Agosti 17, 2026 kwenye wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu jijini Tanga.

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salam
P.O.BOX1968

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when College of Business Education - CBE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category