Joyland International Schools- Dar es Salaam Tanzania

Joyland International Schools- Dar es Salaam Tanzania

We offer the best education for the future of Tanzanian young generation, for their well being. E-MAIL; [email protected] , [email protected]

WELCOME TO JOY LAND INTERNATIONAL SCHOOLS
The mission of Joy land schools is to help young children foster independence, self-reliance and positive self-esteem.

Operating as usual

Photos from Gracious Daycare Centre's post 11/06/2021

Tupo vizuri.......
Gracious Daycare and Pre-school
JUST KNOWLEDGE

20/05/2021

#Daycare #daycarecenter #preschool #Elimu
NAFASI ZIPO KWA MWEZI WA SABA,MWAKA HUU.
JISAJILI SASA.

#Daycare #daycarecenter #preschool #Elimu
NAFASI ZIPO KWA MWEZI WA SABA,MWAKA HUU.
JISAJILI SASA.
GRACIOUS DAYCARE AND PRESCHOOL - JUST KNOWLEDGE

19/05/2021

#Daycare #daycarecenter #preschool #Elimu
NAFASI ZIPO KWA MWEZI WA SABA,MWAKA HUU.

#Daycare #daycarecenter #preschool #Elimu
NAFASI ZIPO KWA MWEZI WA SABA,MWAKA HUU.
JISAJILI SASA.
GRACIOUS DAYCARE AND PRESCHOOL - JUST KNOWLEDGE

18/05/2021

Gracious Daycare and Pre-school.
-JUST KNOWLEDGE

Gracious Daycare and Pre-school.
-JUST KNOWLEDGE

Namna Michezo Inavyomsaidia Mtoto Kujifunza 16/05/2021

Namna Michezo Inavyomsaidia Mtoto Kujifunza

inashauriwa wazazi wawaruhusu watoto kucheza wenyewe bila kuwaingilia. Wanaporatibu michezo yao wenyewe wanapata fursa ya kufanya maamuzi yao, kwa uhuru, na hivyo kujua kitu gani kinawaunganisha pamoja, na malengo yapi wanaweza kuyafikia kwa pamoja kama marafiki wanaoelewana.

Namna Michezo Inavyomsaidia Mtoto Kujifunza Wazazi wengi wanaichukulia michezo ya watoto kama shughuli isiyo na maana. Kimsingi, ipo imani inajengeka kuwa kucheza ni kupoteza muda. Matokeo yake wazazi hujitahidi kuwazuia watoto wasicheze kwa…

15/05/2021

Karibu tanzacomputer Tanzania, Elimu kwa wote

#tanzacomputer #kompyutakwakiswahili #computer #Tanzania

09/05/2021

Unataka kujifunza computer kwa kiswahili? Tembelea blog yetu ya tanzacomputer.blogspot kwa mengi zaidi.

01/03/2021

Kumlea mtoto bila viboko inawezekana?
---------------------------------------------
Malezi bora huhitaji msingi imara kama ilivyo kwa ujenzi wa nyumba. Leo tunaangazia swala la viboko katika malezi na kujielimisha kama inawezekana kulea bila viboko. Haishangazi kuwaona wazazi katika jamii yetu wakichapa fimbo, kwenzi, kumkaripia kwa sauti ya juu (kufoka) na hata kumtusi mtoto wao. Tofauti na dhana iliyojengeka kuwa namna hii mtoto anapata kujifunza utii, watalaamu wa makuzi wanatwambia kuwa mtoto anaweza kutii bila viboko. Hii inajulikana kama uadabishaji chanya unaojengwa kupitia mahusiano mazuri baina ya mtoto na mlezi wake.

Zifuatazo ni nyenzo kuu nne za kujenga msingi bora wa malezi yenye uadabishaji chanya na ambayo hufikia malengo endelevu ya mzazi kwa mtoto wake.

Kuwa na malengo ya muda mrefu juu ya mtoto wako. Kufanikisha kumkuza mtoto tangu anapozaliwa hadi utu-uzima ni kazi ya kujivunia, lakini wazazi wengi huianza safari hii bila kufikiria ni upi mwisho wa safari hii? Ukifanikiwa kujua malengo ya muda mrefu kwa mtoto wako, wewe mwenyewe utakuwa mfano wa kuigwa. Kama unataka mtoto wako awe mwema na mwenye msaada kwa jamii, anayeweza kufikiri, msikivu, asiye mkorofi, mwenye upendo kwa watu wote na mengine kama hayo lazima utembee katika nyayo hizo. Akuige. Ukipanda mahindi huvuni viazi.

Mtengenzee mtoto mazingira ya upendo na mawasiliano. Upendo na mawasiliano kati ya mzazi na mtoto kwa jamii yetu huishia mara nyingi umri wa kuhudhuria kliniki (miaka5). Ili kumkuza mtoto mwema unatakiwa kumuonyesha upendo wakati wote na kumpatia taarifa muhimu hasa kuhusu mabadiliko ya kimwili pale anapoelekea balehe, mfanye mtoto awe rafiki na kwamba kuwa mzazi sio lazima mtoto akuogope bali akuheshimu na kukuthamini.

Elewa watoto wanavyofikiri na kuhisi juu ya mambo mbalimbali. Jipe muda kuelewa hisia na fikra za watoto juu ya mambo mbalimbali kulingana na umri wao. Utakuta mzazi anampiga mtoto mchanga/mdogo kisa analia pasi kikomo usiku na mchana bila ya kujiuliza iwapo mtoto anaelewa hata sababu ya kupigwa? Yapo makosa mengi watoto wanayofanya katika umri tofauti na wazazi hutumia vipigo kama namna ya kuwaadabisha bila ya kujua sababu za watoto (kiumri) kufanya wafanyayo. Vipigo namna hii vinawatengenezea tabia ya kuwa wakorofi na kuamini kuwa matatizo hutatuliwa kwa njia ya ugomvi. Usugu!

Adhabu ni malengo ya muda mfupi. Uelewa juu ya changamoto mbalimbali zitokanazo na hatua za makuzi ya mtoto na namna ya kuzikabili kwa kutumia mbinu rafiki na si viboko ni muhimu kwa mzazi. Utakubaliana nasi kuwa viboko vinamneemesha mzazi/mlezi zaidi hata ya mtoto kwani anapata kutuliza hasira zake huku mtoto akiambulia mafunzo hafifu mno. Kutumia adhabu katika kumuadabisha mtoto hutimiza malengo ya muda mfupi na hulenga katika kutimiza matakwa ya mzazi ya muda huo na si malengo endelevu.

Adhabu za viboko na nyinginezo hugusa zaidi mwili tu na husahaulika kwa muda mfupi wakati kuadabisha kwa njia rafiki hugusa ubongo moja kwa moja na humpa mtoto nafasi ya kufikiri na kujifunza kutokana na makosa. Malezi yanayolenga kukuza mtoto ambaye mzazi anategemea aje kuwa mtu mzima muwajibikaji na anayekubalika kwenye jamii hayana budi kuzingatia nyenzo hizi.

TITANIC 2 HD MOVIE - THE RETURN OF JACK (2020 MOVIE TRAILER) 01/03/2021

TITANIC 2 HD MOVIE - THE RETURN OF JACK (2020 MOVIE TRAILER)

TITANIC 2 HD MOVIE - THE RETURN OF JACK (2020 MOVIE TRAILER) There is no Endless love

15/02/2021

Pata LOGO kwa ajili ya biashara yako uanzia shilingi elfu thelTHINI TU(30,000 TSH). Wasiliana nasi kwa simu namba 0675 117 151. Crystal graphics.

Umuhimu wa Logo katika biashara yako
---------------------------------------------
Katika biashara, kuna vitu muhimu ambavyo mjasirimali/mfanyabiashara lazima avizingatie kabla hajaanzisha biashara yake mbali na kuwa na mtaji, vitendea kazi eneo la biashara, soko n.k. Kwa jamii nyingi za Afrika Mashariki, walio wengi wamekuwa wakifanya biashara na biashara zao kufanikiwa kwa kiasi kikubwa tu lakini bado wamekosa kitu kimoja cha muhimu sana.

Wajasiriamali wadogo wadogo na baadhi ya wafanyabiashara hawana nembo zao za biashara maarufu kama Logo.

Nembo ya Biashara (Logo) ni nini na inamsaidia vipi mfanyabiashara/mjasiriamali?

Kwa tafsiri rahisi, nembo ni alama zinazoundwa na maandishi na picha ambazo zinatusaidia kutambua bidhaa au huduma tunayopenda kwa kuwasaidia wateja kuelewa nini unachofanya, wewe ni nani na unaamini nini na matarajio yako ni yapi.

Kuna umuhimu mkubwa wa mfanyabiashara au mjasiriamali kumiliki au kuwa na nembo ya biashara.

Unaweza kuwa na biashara nzuri tu ya utoaji huduma au bidhaa lakini watu wasivutike na biashara yako wakaenda sehemu nyingine kununua kwa sababu tu wamependezwa na nembo ya mfanyabiashara mwenzako kutokana na dhima au ujumbe uliopo.

Kwanini unashauriwa kumiliki au kuwa na nembo ya biashara?

Nembo ya biashara ni utambulisho wako. Kitu kitakachoitambulisha biashara yako au huduma yako bila kujali kama ni bidhaa iko katika uzito au ujazo gani na kama ni huduma haitajalisha inatolewa sehemu gani ni nembo. Nembo inatengeneza hisia, fikra, mwamko na hamasa ya kununua huduma au bidhaa kwa mteja. Kwa mfano ni kawaida kusikia mtu akisema nimeona matangazo ya kampuni fulani kwani imefika hadi huku? Mara nyingi kitu cha kwanza kujiuliza itakuwa ni nembo ya kampuni au biashara.
Nembo inasaidia kuonyesha umaridadi na ufanisi wa kampuni. Kampuni yoyote yenye kuhitaji kufanya kazi kwa ufanisi lazima iwe na logo (nembo). Nembo inasaidia kuonyesha uthubutu na umakini wa kampuni au biashara ambayo yaweza kuwa ni ya utoaji huduma au uzalishaji wa bidhaa.

Nembo inabeba ujumbe wa biashara yako. Ujumbe ni muhimu katika nembo yako kwa sababu inabeba kile ambacho kampuni yako inafanya. Ujumbe mara nyingi huwa ni wenye mvuto na utakaowafanya wateja wako kuvutika na kuja kuhudumiwa au kununua bidhaa zako- Mathalani unamiliki duka la mapambo linaitwa “Mwanamapambo” Kisha ukaweka ujumbe huu “ Unajenga tunakusaidia kupamba” Ujumbe tu umeshabeba kile unachokifanya ambacho ni uuzaji wa mapambo mtu hatokuwa na haja ya kuja kuuliza duka lako linahusiana na mapambo ya aina gani.

Nembo inasaidia kuonyesha umiliki. Nembo ni moja kati ya alama zinazoonyesha umiliki wa biashara kwa sababu nembo hubeba jina la kampuni au mmiliki wa kampuni. Mfano Azam, Kiluswa Company Limited, Kafulusu Enterprises na mengineyo. Majina hayo yanaonyesha mmiliki wa kampuni ni nani.

Nembo inasaidia kuonyesha matarajio ya biashara. Nembo inasaidia kubeba maono na muelekeo wa biashara yako na hasa kwa kuwaonyesha wateja watarajie nini huko mbele kutokana na huduma au bidhaa unazotoa. Hii inasaidia biashara yako kuwa na ushindani dhidi ya kampuni nyingine zinazotoa huduma kama yako. Mfano kampuni za mawasiliano. Maneno kama “Yajayo yanafurahisha! Uko tayari” yanasaidia kuwafanya wateja wa kampuni kuendelea kusubiria mambo mazuri ambayo kampuni yao imewaahidi.

Nembo ya biashara (logo) ina umuhimu mkubwa katika kutambulisha biashara sokoni hivyo ni vema mfanyabiashara au mjasiriamali kuwa na logo kwa sababu itakusaidia kujitofautisha na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara kama yako. Nembo inasaidi sana kuonyesha uthamani wa biashara unayoifanya.

25/01/2021

Crystal Graphics_ Tz

UNATAKA KUWA FUNDI WA COMPUTER?
Njoo ujifunze ufundi wa computer na simu kwa muda mfupi,(maintanance),laptops na desktop. Tupo toangoma,kigamboni. Unaweza kufundishwa nyumbani kwako,
0675117151

crystalgraphicstz.wordpress.com 15/01/2021

WE DO WEB DESIGNING

PATA WEBSITE KWA AJILI YA SHULE YAKO,TAASISI YA ELIMU NA BIASHARA KWA SHILINGI LAKI TATU TU(300,000). UTAPATA MAINTANANCE BURE KA MIEZI SITA. WASILIANA NASI KWA 0675 117 151. KARIBUNI SANA

crystalgraphicstz.wordpress.com Whether designing from scratch or developing your existing brand, we quickly turn around eye catching deliverable that will appeal directly to your audience. We partner with you to build your web p…

05/10/2020

Crystal Graphics_ Tz

UNATAKA KUWA FUNDI WA COMPUTER?
Njoo ujifunze ufundi wa computer na simu kwa muda mfupi,(maintanance),laptops na desktop. Tupo toangoma,kigamboni. Unaweza kufundishwa nyumbani kwako,
0675117151

03/04/2020

JOYLAND SCHOOLS MANAGEMENT TEAM
----------------------------------------------------------------
We kindly inform parents/ guardians to come to our accounts office today, 4th of April,2020 as from 8am... for,
A/. Taking invoice for second quarter.
B/. Knowing transport fee /has changed/ i.e day scholars.

27/03/2020

Joyland International Schools- Dar es Salaam Tanzania's cover photo

27/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
--------------------------------------------------------
The future Begins Here

22/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
-------------------------------------------------------
The Future Begins Here.

18/03/2020

SHULE KUFUNGWA KWA SIKU 30,TOKA TAREHE 17 MACHI 2020 - SERIKALI YA TANZANIA
-----------------------------------------------------------------
Hapo jana ,tarehe 17 mwezi wa tatu,2020, Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa alitangaza kufungwa kwa shule zote kuanzia za awali mpaka kidato cha sita kwa siku 30 zikiwa ni jitihada za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa CORONA.

Wizara itafanya marekebisho ya ratiba kwa wale wanaotarajiwa kufanya mitihani tarehe 4 Mei, itasogezwa mbele kadiri ya matokeo yatakavyojitokeza ili nao wapate kusoma kwa kipindi kilekile kilichokubalika na ratiba hiyo.

Lakini pia serikali ya Tanzania imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile ligi kuu ya Tanzania, Ligi daraja la pili, ligi daraja la kwanza lakini pia michezo ya shule za msingi (UMITASHUMTA) , michezo ya shule za sekondari(UMISETA) pamoja na michezo ya mashirika ya umma.

Pamoja na kuzuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.

Aidha bwana Majaliwa alisisitiza kuwa nchi imejiandaa vyema kukabiliana na mlipuko wa COVID 19 nchini Tanzania.

Kutokana na agizo hilo,shule yetu ya Joyland imefungwa rasmi jana,kwa muda huo elekezi (siku 30),mpaka hapo serikali itakapotoa tamko. Watoto wote wa boarding wanatakiwa kuwa wamesharudi nyumbani mpaka muda huu.
Tunaomba radhi kwa wazazi/walezi kutokana na usumbufu uliojitokeza,ni nje ya uwezo wetu.
THE FUTURE BEGINS HERE.

17/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
------------------------------------------------------

THE FUTURE BEGINS HERE

13/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOL
---------------------------------------------------

CONGRATULATIONS OUR KIDS FOR PERFORMING WELL ON WORLD SCHOLAR' CUP..... NEXT TRIP IS DUBAI!!!!

THE FUTURE BEGINS HERE.

09/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
--------------------------------------------------------
TWENZETU SERENGETI TOUR

09/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
-------------------------------------------------------
WORLD SCHOLAR'S CUP Feza Schools, Mwalimu Nyerere Memorial Academy
It was a very good experience for our smart kids. We are waiting for the next round.

06/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
-------------------------------------------------------
PRIMARY SECTION EVENTS CATALOGUE

THE FUTURE BEGINS HERE.

[03/05/20]   JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS ON BIRTHDAY
----------------------------------------------------------------------------

This was how it ended @Joyland International daycare Center

04/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS DAYCARE CENTER
-----------------------------------------------------------------------------------

THE FUTURE BEGINS HERE

02/03/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOL DAYCARE CENTER
-----------------------------------------------------------------------------------
Nafasi za Daycare zipo.
Tunaandikisha kuanzia miezi tisa (9)
Day na Boarding.
JOYLANDI NTERNATIONAL SCHOOLS, THE FUTURE BEGINS HERE.

28/02/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS PRIMARY SECTION
-----------------------------------------------------------------------------------
SCIENCE CONTEST
Kutakuwa na mashindano ya sayansi kwa vijana wa upande wa shule yamsingi,siku ya leo tarehe 28/02/2020,katika bwalo la kulia chakula,shuleni hapa. Mashindano haya yatafanywa kwa njia ya maonesho kutoka vikundi mbalimbali vya wanafunzi. Mashindano haya yatahusisha utengenezaji wa kompyuta, mifumo ya binadamu,huduma ya kwanzana mengine mengi ya kuvutia.
JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS. THE FUTURE BEGINS HERE.

28/02/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS DAY CARE CENTER
-----------------------------------------------------------------------------------
Uongozi wa Joyland daycare center na blue class unapenda kukufahamisha kuwa leo tarehe 28 Feb 2020 kuanzia muda wa saa 4.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana kutakuwa na birthday kwa watoto waliozaliwa mwezi wa JANUARI na FEBRUARI.

Watoto wote leo watavaa nguo za nyumbani, rangi za ua la sunflower, yaani nyekundu,njano na nyeupe.Kwa wale wenye birthday wanaweza kuandaa keki zao.

Pia watoto waje na nguo za kuogelea katika bwawaaa la kuogelea watoto lililopo hapahapa shuleni kwetu.
WAZAZI/WALEZI MNAKARIBISHWA.

THE FUTURE BEGINS HERE.

27/02/2020

TWENZETU SERENGETI STUDY TOUR
---------------------------------------------------------
Joyland International Schools inapenda kuwaarifu wazazi/walezi kuwa kutakuwa na STUDY tour kwa ajili ya wanafunzi wake ,kuanzia tarehe 4 mpaka 9 June,2020.

Tour hii itakuwa ya kimasomo na utalii wa ndani, ambapo tutatembelea sehemu mbalimbali,kama ARUSHA NATIONAL PARK,SERENGETI,NGORONGORO CRATER,AICC na EAC HEADQUARTERS_ARUSHA.

Gharama ya trip hii itakuwa ni Tsh 650,000 kwa mtoto mmoja,na kwa wale wenye watoto watatu na kundelea watalipia Tsh 500,000 kwa kila mtoto. Hii itajumuisha usafiri,chakula,malazi pamoja na viburudisho vya kila aina.

Malipo yatafanyika kwa njia ya TIGOPESA kupitia simu namba 0652 733 121 (Calister Mungwe). Nyote mnakaribishwa.

THE FUTURE BEGINS HERE.

26/02/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
----------------------------------------------------------

Nafasi bado zipo - DAY CARE
- NURSERY
- PRIMARY
- SECONDARY
Usahili unafanyika kila siku, shuleni mikwambe nyumba ya njano,kigamboni. JUmatatu mpaka jumamosi,saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni. Wote mnakaribishwa.
THE FUTURE BEGINS HERE.

25/02/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
-------------------------------------------------------
Siku kama ya leo, mwaka 2015, shule yetu ya Kimataifa ya Joyland ilizaliwa. Tunawashukuru wazazi,walezi na wadau wote wa elimu kwa kutuamini na kuwa pamoja na sisi. Pia tunawashukuru directors wetu wa shule,walimu na wafanyakazi wetu wote kwa kufanya taasisi yetu isimame. Happy Birthday JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS.

THE FUTURE BEGINS HERE.

[02/24/20]   Follow us on our Instagram page @joylandinternational

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS, THE FUTURE BEGINS HERE.

23/02/2020

TWENZETU SERENGETI STUDY TOUR
---------------------------------------------------------
Joyland International Schools inapenda kuwaarifu wazazi/walezi kuwa kutakuwa na STUDY tour kwa ajili ya wanafunzi wake ,kuanzia tarehe 4 mpaka 9 June,2020.

Tour hii itakuwa ya kimasomo na utalii wa ndani, ambapo tutatembelea sehemu mbalimbali,kama ARUSHA NATIONAL PARK,SERENGETI,NGORONGORO CRATER,AICC na EAC HEADQUARTERS_ARUSHA.

Gharama ya trip hii itakuwa ni Tsh 650,000 kwa mtoto mmoja,na kwa wale wenye watoto watatu na kundelea watalipia Tsh 500,000 kwa kila mtoto. Hii itajumuisha usafiri,chakula,malazi pamoja na viburudisho vya kila aina.

Malipo yatafanyika kwa njia ya TIGOPESA kupitia simu namba 0652 733 121 (Calister Mungwe). Nyote mnakaribishwa.

THE FUTURE BEGINS HERE.

22/02/2020

JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS
-------------------------------------------------------
JOYLAND INTERNATIONAL SCHOOL INAWALETEA SOMO JIPYA LA MUZIKI, AMBAPO WANAFUNZI WATAJIFUNZA UIMBAJI NA UPIGAJI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA MUZIKI KATIKA HATUA YA KIMATAIFA,WAKITUNUKIWA VYETI VINAVYOTAMBULIKA KIMATAIFA BAADA YA KUFANYA MTIHANI WA KIMATAIFA TOKA UINGEREZA.

MLETE MWANAO SHULE YA KIMATAIFA YA JOYLAND,NAFASI BADO ZIPO. USAHILI UNAFANYIKA KILA SIKU YA JUMATATU MPAKA JUMAMOSI,SAA MBILI ASUBUHI MPAKA KUMI JIONI.

THE FUTURE BEGINS HERE.

Videos (show all)

joyland international schools,nursery section.For more info,visit our website,www.joylandinternationalschools.wordpress....
Joyland international schools.The future begins here
Dar fresh study tour...............Visit our website, www.joylandinternationalschools.ac.tzJOYLAND INTERNATIONAL SCHOOLS...

Location

Telephone

Address


MIKWAMBE,KIGAMBONI
Dar Es Salam
+255

Opening Hours

Monday 06:30 - 18:00
Tuesday 06:30 - 18:00
Wednesday 06:30 - 18:00
Thursday 06:30 - 18:00
Friday 06:30 - 18:00
Saturday 06:30 - 18:00
Other Elementary Schools in Dar es Salam (show all)
New Version Primary School New Version Primary School
25415
Dar Es Salam, +255

To create the first level in education with the Spiritual generation which brings Spiritual and Physical transformation in Tanzania up to the whole world.

Feza Nursery School Feza Nursery School
Mikocheni A
Dar Es Salam

Feza nursery school is located at Mikocheni, near Regency hotel, opposite to the KFC. We accept kids from 3 to 6 years of age.

Jangwani Girls Secondary School Jangwani Girls Secondary School
United Nations Road
Dar Es Salam, PO BOX 2276

Official Page for Jangwani Girls Secondary School

Ecole française / French School Arthur Rimbaud, Dar Es Salaam, Tanzanie Ecole française / French School Arthur Rimbaud, Dar Es Salaam, Tanzanie
Mawenzi Road, Masaki
Dar Es Salam

Ecole Française Arthur Rimbaud de Dar es Salaam : homologuée de la PS à la Terminale

Tanzania Chess Foundation Tanzania Chess Foundation
16th Floor PPF Tower, Ohio Street
Dar Es Salam, 14508

The main aim is to promote Chess in Schools. We call it Chess for Grades