01/06/2026
➡️ PAST CONTINUOUS TENSE -WAKATI ULIOPITA UNAOENDELEA
▶️ Tunatumia tense hii katika kuelezea vitendo vilivyokuwa vinaendelea kufanyika wakati uliopita.
▶️ Pia tunatumia tense kuelezea vitendo vilivyokuwa vinafanyika wakati vitendo vingine vilipotokea au vilipoingilia kati (interrupted actions).
Ngoja tuangalie matumizi hayo katika sentensi hizi hapa chini katika maelezo na maswali.
📝Kanuni (structure) katika maelezo ya kawaida/kukubali (positive statements).
Subject + was/were + verb---ing (kitendo kikiwa katika hali ya kuendelea)
"Was" inatumika kwa I, he, she, it na Jina moja.
"Were" inatumika kwa You, we, they na majina mengi.
MIFANO
1. I was drinking coffee at the café - nilikuwa nakunywa kahawa mgahawani.
2. She was doing the dishes when we came in - alikuwa anaosha vyombo wakati/pindi tulipoingia ndani.
3. They were eating supper while arguing - walikuwa wakila chakula cha jioni huku wakijibizana.
📝Kanuni katika sentensi za kukanusha (negative statements)
Subject + was not/were not + verb---ing (kitendo kikiwa katika hali ya kuendelea)
MIFANO
1. I wasn't singing and dancing when you got into the house - sikuwa ninaimba na kucheza wakati ulipoingia nyumbani.
2. We weren't waiting for the bus while preparing for an exam - hatukuwa tunangojea basi huku tukijiandaa na mtihani.
3. It wasn't pouring outside - haikuwa inanyesha (mvua).
📝Kanuni katika sentensi za maswali - positive questions.
Was/were + subject + verb---ing (kitendo kikiwa katika hali ya kuendelea)?
1. Were you rushing to the bus stop? - je ulikuwa unawahi stendi (kituo cha basi au dala dala)?
2. Was he running faster than you when they showed up? - je alikuwa anakimbia haraka kuliko wewe pindi walipotokea(walipofika)?
3. Was she heading to the store? - je alikuwa anaenda dukani?
That's all for today.
If you have any question, we are here to help each other.
See you soon!