19/08/2026
MAZURI YOTE ,MABAYA YOTE, HUTOKA MOYONI
Moyo wa mtu ni mdanganyifu , una ugonjwa wa kufisha. Mawazo ya mwanadamu ni mabåya tangu utoto wake. Kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. Mtu mwema katika Akiba njema hutoa mema, bali mtu mbaya katika Akiba mbaya huta mabaya .
Kwa sababu hio hakuna mti mzuri unaotoa matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya unaoweza kutoa matunda mazuri.
Ina maana k**a ukipanda maembe na kutarajia kupata ndizi, matarajio yako yatakuangusha. Ukipanda mti wa mpera utapata mapera. Utavuna kile ulichokipanda hio ni sheria ya kupanda. Muda nchi idumupo majira ya kupanda na mavuno , wakati wa baridi na wakati wa hari , wakati wa kaskazi na wakati wa k**i , mchana na usiku , havitakoma.
Yanayotoka katika mayo wako ndiyo hayo unayajenga , k**a ni kwenye mwamba au mchanga.
JINSI GANI UTATOKA HAPA?
1.Ingia katika upendo. Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote na kwa akili yaka yote na kwa roho yako yote.
Na k**a unavyotaka watu wakutendee wewe, watendee vivyo hivyo. usiwaze mabaya juu ya jirani yako..
Usihukumu kwa kuona kwa macho ya damu na nyama. bali hukumu ya kweli inayotoka katika kweli.
Usimnyoshee mtu kidole, ondoa kwanza boriti iliyoko ndani yako, hapo ndipo utakapoona vema kukitoa kibanzi kilichopo katika jicho la ndugu yako..
2.EPUKA KUKAA BILA YA KUFANYA JAMBO , KUONGEZA UJUZI WA KAZI YAKO, KUSOMA VITABU MBALIMBALI.
K**a huna jambo la kufanya , hapo ndipo mawazo mengi huja ili kukufanya upotee kabisa. Utaanza kutazama watu, kuwahukumu, kuwabeza, kuwadharau. kwa nini ? Huna kitu cha kufanya.
Adui anatumia sana akili ya mtu ambayo iko wazi , isiyokuwa na cha kufanya. wakati mwingine mbele yaka kuna uchafu mwingi, nyumba yako ni chafu. Badala ya kuinuka ufanye kazi , utaanza kuita mfanyakazi afanye kitu ambacho kingekuwa ni faida kwako, lakini unamfaidisha mfanyakazi.
Mimi niligundua hiki, kila kitu mfanyakazi yupo atafanya n. kumbe unamwachia adui ili akuteke mawazo yako.
Maovu hutoka Moyoni kwa sababu, kabla hujafanya jambo lolote. Lazima lianzie huko ndani, katika fikra yako. Namaanisha, kabla hujatenda dhambi , uliwaza kwanza Moyoni mwako. Sasa hapa kuna wanaoshinda wachache. lakini wengi huishia kuwaza mabaya mabaya.
3.Soma neno la Mungu likae kwa wingi ndani yako ili likusaidie kujibishana na mawazo yako.
Mungu atusaidie sisi tuweze kuwaza k**a ambavyo anawaza Yeye.
Baba usitutie majaribuni, bali tuokoe na yule mwovu..