Siasa za kimataifa na Kitaifa

Siasa za kimataifa na Kitaifa

Share

Ya jue matukio mbali mbali kwa kina na kwa ukweli zaidi yani uwazi Tutakua tuna elezea mustakabali mzima wa record lebel yetu na kuibrand kimataifa zaidi

18/10/2024

Majasusi wa Korea ya Kusini wameeleza wazi ya kwamba majirani zao Korea ya Kaskazini au kwa kiduku, wametuma wanajeshi kuelekea Urusi kwa lengo la kujiunga na vita uko Ukrain.

jana zilivuja video zikionyesha wanajeshi wa Korea ya Kaskazini wakiwa Urusi, japo hazikudhibitishwa moja kwa moja lakini kuna uwezekano mkubwa wanajeshi hao wa kduku kuwa wametuwa Urusi.

Tunaweza sema ngoma inogil, hawa vijana wa kiduku wanapenda vita kuliko vita vyenyewe, kwa muda mwing hawajashiriki vita naona wameenda pasha.

Tukumbuke tangu vita vianze tumeshuhudia nchi za ulaya zikipeleka wanajeshi wake kwa mlango wa nyuma na wka uficho au kwa mlango wa miseneri au wanajeshi wa kulipwa waliojtolea, mbali na jeshi tumeona msaada mkubwa wa kijeshi ukimiminika uko Ukrain.

Ivyo hakuna kusema kwanini kiduku katuma jeshi, yeye ni swahiba wa Puti, ivyo anasaidia k**a tu NATO inavyomsaidia Ukrain kwa mlango wa nyuma.

Ni mimi Drim Bway Defya

Photos from Siasa za kimataifa na Kitaifa's post 18/10/2024

Baada ya kifo cha Yahya Sinwar kichotokea jana, leo Hamas wamemtangaza Khaled Mashal k**a Boss mpya wa kundi hilo.

kuna vingi vya kuchambua, Mungu akijalia post ijayo nitaelezea juu ya tukio hili ila naweza sema kitendo cha Israel kuuwa viongoz wa juu ya kundi la Hamas ni dalili za kutaka kumaliza vita na washashindwa ivyo wanataka kupoteza morali kwa Hamas na kupoteza utulivu.

Picha namba moja ni Yahya Sinwar ambae ameuwaa hapo jana na picha namba 2 ni Khaled Mashal ambae amerithi kiti.

Post ijayo nitaelezea kwa ufasaha juu ya Israel anataka maliza vita.

NI mimi Drim Bway Defya

Photos from Siasa za kimataifa na Kitaifa's post 07/10/2024

UCHAMBUZI WA KINA WA MWAKA MMOJA WA VITA MPYA YA GAZA NA ISRAEL TANGU TAREHE 7 MWEZI WA 10 MWAKA 2023

UTANGULIZI

Naomba nianze na andiko hili kwa kunukuu moja ya hotuba ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ndugu Antonio Guterres, alioitoa mwaka jana 24/10/2023.

"It is important to also recognize the October 7 attacks by Hamas did not happen in a vacuum. That Palestinian people have been subjectad to 56 years of saffocating occupation"
"They have seen their land steadly devoured by settlement and plagued by violance, their economy stilied; their people displaced and their homes demolsihed. Their hopes for political soluton to plight have been vanishing"

Tafsir huru ya nukuu ya Gutterres, anaelezea ya kwamba.
Ni vema pia kutambua shambulizi la Hamas la October 7 halikutoea tuu k**a ombwe (halijaja bila sababu) ambapo kwa zaidi ya miaka 56 wapalestina wananyanyasika kwa kutokupumua kwa uvamizi unaofanywa kwa ardhi yao.

Wameshuhudia ardhi yao ikithibitiwa na kumezwa na wavamizi na wakichukua kwa mabavu, uchumi wao ukiibwa na watu wao wapalestina wakikosa makazi huku nyumba zao zikiharibiwa.
Matumaini yao yakisiasa kutatua hali zao mbaya yametoweka na hawana matumain tena.

NINI KILITOKEA OCTOBER 7?
October7 mwaka jana itakumbuka kwa waisrael na wapalestina na maeneo ya mashariki ya kati na dunia kwaujumla baada ya wanamgambo wa Hamas kuvamia Israel na kushambulia haswa sehemu mbali mbali za kambi za jeshi, makaz ya askari na maeneo mengine ya umma na raia na kuteka raia mbali mbali walokuwepo nchini humo.

Maelezo yanasema zaid ya wasirael 1,400 na vifo vya watoto zaid ya 20 waliuwawa kati shambulzi hilo, ambapo badae jeshi la Israel likatangaza vita Rasmi na Hamas kwa itawatokomeza wote na itadhibit upya ukanda wa Gaza, pia kuwarudisha mateka wote waliotekwa ambao ni zaid ya 130.

Ni mwaka sasa umepita ambapo Israel inafanya wanachsema vita dhidi ya Hamas, uko Gaza lakin hadi leo bado vita vinaendelea, bado hawajaithibid Gaza na bado hawajakomboa mateka wote, ambapo mateka waliowakomboa ni walifanya makubaliano 'prisoner swaps" na mmoja pekee ndo wamemuooa.

Mwaka mmoja wa vita ni wapelestina elfu 40 wamefariki uku watoto zaid ya elfu 18 wamefariki, sijasema wanawake na vikongwe, sasa sijaelewa k**a watoto tena vichanga na wazee vikongwe nao wanashika silaha pigana na Israel.

UHALISIA WA HII VTA
Uhalisia wa hii vita lazima turudi tuisome tena nukuu ya katibu mkuu Antonio Gutteres ambapo ndo uhalisia, ni mpumbavu pekee atatazama mgogoro huu kwa kutazama tarehe 7 tuu ya mwez wa 10, na akiacha tazama miaka 56 nyuma nini kilikuwepo.

Tuwe wawazi tuu, siungi mkono tukio la tarehe 7 lakini tukubali wapelestina kwa miaka na miaka wamekua watumwa ndani ya nchi yao, hakuna tofauti ya Afrika kabla hatujapata uhuru wetu na nchi namna Palestina anvyopitia, hakuna tofauti wavyoteseka wasauzi Afrka wa manyanyaso ya wakaburu na jinsi leo Palestina anvyonyanyasika na ukaburu wa Israel.

Wapo ndani ya nchi yao lakini hawana mamlaka, hapa nikazie bora kinachotokea Congo au vita maeneo mbali mbali hapa duniani mana ni migogoro ya ndan au mapandikiz toka nje lakin wapo huru na wanajtawala wenyewe na bado vikosi vya umoja wa mataifa vipo, vikosi mbali mbali vipo.

Lakin Palestina haina huo msaada, wao wanatawaliwa na Israel wao hawana msaada wowote ule k**a dunia imeitenga Palestna, hata msaada wa kibinadamu tuu muda wa vita anaemuru uingie ni Israel, huduma za kijamii wao ndo wanamua ziwepo au laa, uku Western bank ndo aibu mnoo.

Western Bank maeneo yote yanatawaliwa na Israel japo kuna Rais wa Palestina, wao ndo wanamua walale saangap, wao ndo wanakagua mipaka na njia toka sehemu nyengine nenda sehemu nyengine, jee huu sio utumwa?

Wachofanya Hamas ni kuikumbusha dunia ambayo ishasahau Palestina, na ishakubali wasrael wafanye wanachotaka, Hamas wamefanya kukumbusha dunia kwamba wamechoka na mateso ya wasrael na wanaona wanaenda toweka katika ramani ya dunia.

Israel na washirika wake wote wamewahadaa nchi za kiarabu ambapo na wao walishakubali Palestina kutoweka kwenye sura ya dunia, bila october 7 dunia isingejali tena kuhusu Palestina.

Leo hii dunia imeamka na sasa wanataka uwepo wa taifa huru la Palestina, leo hii dunia imeamka toka usingiz mzito na kukurupuka sasa wote tunajua kuna Palestina yahitaji uhuru wake.

NANI MSHINDI HADI SASA KATI YA HAMAS NA IDF
Kwenye vitabu viwili vya wanamikakati mashuhuri na wananadharia wa vita wakongwe namanisha kitabu cha 'ON WAR' cha Karl von Clauswitz na kile cha 'ART OF WAR' cha Sun Tzu..

Ndani ya vitabu hivi wamekubaliana au gongana kimtazamo juu ya swala la Malengo ya vita na ushindi wa vita.

Ambapo wote wanaeleza malengo ya vita yanaendana sambamba na malengo ya kisiasa na ushindi ndani ya vita ni pale malengo ya kisiasa yanapotimzwa ndani ya vita ndo mana watalamu wasuala ya mikakati ya kivita wanaamin Urusi ashamaliza mchezo muda tuu ila leo hatupo na mrus.

Tunapotazama vita vya Gaza basi tunatazama malengo ya kisiasa yaliyowekwa na je yametimizwa, kuboa majengo na kuuwa uwa raia waso na hatia hata wenye hatia haifanyi Israel iwe ndo mshindi sababu malengo yao hadi sasa hayatimia.

Malengo ya Israel yalikua matatu ambapo moja kuokoa mateka walotekwa na Hamas, ambapo hadi sasa mateka zaidi ya 100 hawajaokombolewa.
Lengo la pili kuiangamiza Hamas yote na kuitokomeza na hadi sasa Hamas ipo na inaendelea na mashambulizi.
Lengo la 3 ni kuithibiti Gaza na kuwa chini ya uangalifu wao lakini hadi sasa bado Gaza haipo chin ya uangalfu wa Israel.

Tunaweza sema ndani ya mwaka mmoja Israel haijashinda na imepoteza mana dunia kwa sasa yataka Palestina iwe huru na uanzshwaj wa nch mbil zenye kuheshimaina, Hamas hadi leo wameweza washkiria mateka ambapo Israel alijinasibu haitopita meizi mateka wote watakombolewa.
Lakini pia bado Hamas wapo na utawala ndan ya Gaza ambapo bado Israel anaangaika kuapatawala.

Kwanin malengo ya kisiasa ndo hutupa ushind wa vita?
Naomba nianze na mfano wa vita vya 1979 hapa ardhi ya Afrka Mashariki ambapo Tanzania walipigana na Uganda ambapo Tanzania alishinda.

Malengo ya yalikua dhibiti na kurudisha eneo la mtukura, pia kumuondoa madarakan, aliekua Rais wa Uganda Iddy Amin Dada, ivyo basi Tanzania hata ingebomoa na kuwa kila mwanajesh au raia wa Uganda k**a wasingerudsiha ardh ya mtukura, na kumfurumusha Dada basi bado wasingejinadi wameshinda vita.

Mara zote vita ni matokeo ya wanasiasa na sababu za kisiasa iyo malengo yasipofikiwa bado vita ujashnda, ni wazi nasema Israel ameshindwa vita hii achoweza fanya ni uharibifu na uuaji wa wasio na hatia.

Na ndoma japo ya kubomoa bomoa ovyoo majengo na kuuwa ovyo ovyo bado anaendelea na vita ambapo kwa jicho la juu juu utasema mbona haina haja tena mana Gaza ishachakazwa mbona bado anabomoa?

Sababu ni anachofanya sawa sawa na wachezaj wa mpira wenye njonjo na makeke lakini bado hawajapata goli ivyo wanasak**a lango la wapinzan wao na hamas ni sawa na team au wachezaj waliopata goli afu wanalilinda, ivyo mchezo ukiisha Hamas ni washind japo Israel ndo aliutawala mchezo na mbwembwe zote uwanjan. na hapa ndpo Von Clauswitz na Sun Ztu wanaelezea kuhusu 'role of offensive an defensive'

Ambapo jeshi linalojilinda vizur japo dogo kwa mashambuliz ni bora jeshi kubwa linaloshambulia sana, Hamas anashambulia kwa kuvizia lakin amewekeza mua wake mwngi kwenye kujilinda, ndo mana leo wapo wanaendelea na vita.

MWISHO

Wengi waliofungwa na udini huzungumzia kidini na wengi huchagua upande sababu ya udini, ni upungufu wa utimamu na uelewa wa uhalisia wa mambo lakini siwez hukumu, kinachtokea kule hakihusaini na dini japo dini imetumika sana wa muda mwing kleta mgawanyiko, ukwel yanayotoea ni ubabe tuu na dhuruma kwa kuhadaa watu waone wababe ndo wenye haki na wanaoonewa ni wakosaj ivyo wababe wanahaki ya kufanya anachofanya.

Tazama mgogoro huu njee ya udin uliolishwa uje na mtazamo sahihi, ondo chuki au mapenz unapotazama jambo hili, ndo mana Sauz Afrika yeye bega kwa bega na wanaoonewa mana anajua machungu yake.

Nashukuru Mungu dunia inaanza elewa nani mgomvi na nan mchokoz, ndo mana tumeshuhudia maandamano makubwa dunia nzma yakiunga mkono Palestna na kusimama nao huu ushind kwa Palestina ambapo miaka mingi walisuswa na dunia japo wanakufanya nyanyaswa sababu ya propaganda na uzushi.

Ni mimi Drim Bway Defya

28/09/2024

Ni rasm sasa kiongoz mkuu wa wanamgambo wa Hezbollah, Hassan Nasrallah ameuwawa baada ya mashambulizi makali yaliyofanywa na Israel nchini Lebanon katika mji wa Beirut.

Naweza sema mwaka huu umekua mbaya sana kwa anti-zionism, na wote wanaopingana na dhuruma za mazayuni wa kiisraeli, ni mwaka mbaya sana kwa serikali ya Iran ambapo ishapoteza Rais wao Ibrahim Rais kwa ajar ya ndege ya kijeshi, kuuwawa kwa Ismael Haniyeh ambaye ni kiongoz mkuu wa kisiasa wa Hamas na leo kuuwawa kwa Nasrallah.

jana Israel ilifanya mashambuliz makubwa sana tangu mzozo huu unze kupamba moto mwez huu, ripoti za jana zilienea kwamba Nasrallah ameshambuliwa.

Leo majira ya asubuh Israel Defance Force wametoa tariifa ya kuuwawa kwa Nasrallah lakini Lebanon au Hezbollah hawakutoa tariifa rasm hadi majira ya jioni, ambapo Hezbollah wamedhibitisha Hassan Nasrallah, ameuwawa.

Bado ni ombwe na giza zito ndan ya Lebanon na middle east kwa ujumla ambapo hatujui nin chaweza tokea aseee.

Iran inashtumu USA kuwa anahusika na mauaj hayo, lakin Iran amekua akinyoshea vidole bila kufanya majibu tangu tukio la Hanniyeh ambapo alidai atalipa kisasi, kabala hata kovu la Hanniyeh alijaisha, ameuuwawa Nasrallah.

Vitalipwa vifo vya viongoz hawa wa juu wa makundi ya Hezbollah na Hamas yenye ushirika na Iran ambapo nchi za magharib zinayaaita haya makundi iranian back door groups au itakuaje?

kuescaluate the aftermath of Nasrallah death, yaonesha wazi mgogoro unazi pamba moto na hata USA waliionya Israel befor mauji ya Hanniyeh kwamba hayatozuia au kufanya Hamas ipotezee nguvu, and Israel ikapuuzia.

Uhalisia haujazuia au punguza nguvu bado mambo mazito uko Gaza na kifo cha Hanniyeh ndo sababu ya Hezbollah ongeza mashambulizi Israel sasa leo wamemuuwa Nasrallah je hari itakuaje? je Hezbollh watatulia tuu???

Netanyahu amekua anafanya mambo kiupofu sababu yupo na presha kubwa haswa toka kwa waisrael wenyewe ambapo wanaandamana na kuupinga utaala wa Netanyahu, mbal na hapo wanataka vita uko Gaza viishe na raia wao waliotekwa warudishwe.

Netanyahu anahaha so anachofanya anafanya kwa mihemko na sio kwa maono mbali na msaada ya USA na Ulaya basi Israel anakibarua kizito mnooo.

Ni mimi Drim Bway Defya

Photos from Siasa za kimataifa na Kitaifa's post 24/07/2024

Hilo jengo unaloliona hapo ni Capitol Hill, ndo wabunge wa marekani hukutana na kupanga wanayoyapanga, na hilo nyomi unaloliona hapo lenye bendera za Palestine ni raia wa Amerika ambapo wamekusanyika katika jengo hilo kupinga ujio wa waziri mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel, kupata nafasi ya kuhutubia Congress.

Benjami Netanyahu yupo USA kwa ziara ya kikazi kwa siku tatu, ambapo tangu apotua USA amepokelewa na maandamano, na wengi ya waandamanaji wanashinikiza ak**atwe mana yeye ni muharifu wa kivita k**a ICC zivyotoa uamuzi huo.

Siasa zimebadilika sana hari ya sasa ya kisiasa imebadirika sana sio Afrika tuu bali hata Ulaya na Amerika, mambo yapo hovyo kwa Netanyahu naona kaenda kuweka mazingira vizuri, na target yake ni kwa Trump awe upande wake na pia apate baraka za Congress.

Netanyahu leo hii ataenda wapi asikutane na maandamano ya kumtaka ajiuzullu, ya kusitisha vita na ya kumtusi, sio nchin mwake Israel na pia na matafa mengine,

Netanyahu amepaniki leo na kuwatusi waandamanaje na kuwaita "IRAN'S USEFUL IDIOTS" kwa kibongo mana yake wapuuzi au wajinga wanaotumiwa na Iran.

Netanyahu anamiin wandamanaji wanatumiwa na Iran, hahahah hapa kapanic sana na ila tuna la kujifunza mana yake kuna maandamano mengi yaliofanyika au yanafanyika katika nchi fulan laki yanakua yapo chini ya nchi au viongoz wa nchi fulani.

Iran hana uwezo wa kusponser mandamano ndan ya ardh ya Amerika so iyo hoja ni dhaifu, and vip nchin mwake pia Iran anawatumia? and maandamano ypo dunia nzma ya Ulaya, Amerika na Arap pen*sula so wote hao Iran anahusika? basi Iran ananguvu sana.

wandamanaji wanamtaka aache mapigano aache kuuwa wasio na hatia, sasa zaid ya wapalestina elfu 40 wameuwaa tangu october 7 mwaka jana, watoto takibran 15 wameuwawa na waoto zaid ya elfu 20 wamepotea yan hawajulikan wamekufa au laa, watu milion 1 na 9 wamekimbia makazi yao na kuharibiwa.

Hapo unapigana na Hamas au unauwa wasio na hatia? unazuia misaada watu wanakufa njaa unasema HAMAS wanajificha kwenye makaz ya watu sasa mbona mataka hamuaapat si nao watakua ndan ya hao watu?

Waisrael wanataka ndugu zao waliopo mateka uko Gaza mwaka unaaribia, Serikal inatoa ahadi hewa mambo haya yachochoe hasira miongon mwa watu.

Najua watoto wa tafa la mungu hamtopenda post hii.

ni mimi Drim Bway Defya

Photos from Siasa za kimataifa na Kitaifa's post 22/07/2024

Oyaaa wakuconspirancy uyo mwanmama mnaemuona hapo anaitwa Kimberly Cheatle, uyo ndio Director wa United State Secrety Services, leo hi aliitwa na k**ati ya oversight and Accountabilty ya bunge la marekani wamuhoji juu ya tuko la jaribio la mauaji ya Rais mstaafu Donld Trump.

Mchumba wamemkalia kooni wanataka ajiuzuru na hii yote baada ya tukio la jaribio la mauaji ya Donald Trump katika Jimbo la Pennslvanyvania mapema week ilioisha nyuma.

Leo Juma tatu aliitwa ndani ya k**ati ya oversight and accaountability, oyaaa hii k**ati sio poaa asee, sijui k**a kuna maisha marefu ya uyu mwanamama mana alipigwa maswali na alikosa hadi cha kujibu

Katika mambo yaliyo tia ugumu ni kukiri hadi leo hii bado ajatembelea eneo la tukio la jaribio ya mauaji na pia hakuna na maaelezo ya kina juu ya tarifa mbalimbali.

kwanza tuelewane secrety services sio CIA, au NIS, post za mbeleni nitaelezea tofauti ya CIA, NIS na FBI haya yote ni mashirika ya kiusalama na yanatofautiana kazi but tunaposema Secrety Service Agency hawa wapo specifically na ulinzi binafsi wa maVIPs au viongozi wakubwa ndani ya nchi, mfano Rais, Makamu, Mawaziri, wastafu waliohodhi nafas mbali mbali za juu katika nchi ya USA au maeneo maarumu ya umma ambayo wao hufanya usalama lakini kazi kubwa ni ulinzi wa viongoz wa juu wa serikali na familia zao.

Lakini SSA wanajukumu la kulinda mahali panapokuwa na viongoz na maeneo ya kimkakati k**a vile Ikulu, Bunge, katika nk.

Pia wanajukumu la kuwapa ulinzi familia ya VIPs mfano watoto na wake wa marais, wanapata huduma ya kulindwa na Secrety Service so.

shambulio la Trump ni aibu kwa USSS sababu jukumu lao namba moja ni la kuwalinda VIPs, sasa inatokea shambulizi la namna iyo afu kwenye mkusanyiko wa watu ni aibu kubwa sana, na ndo mana anaombwa ajiuzulu.

Katika mambo yalinivutia katika k**ati hi ni maswal ya wanak**ati . nilivutiwa sana na mwanadada Nancy Muce na mchiz Pat Fallon hawa watu walimpelekea moto sana Bi Kimberly, picha zao zipo chini kwenye comments.

ni mim Drim Bway Defya

21/07/2024

Oyaaa wana wana wanangu wa kuconspiriancy hatimae mkeka umetiki, Joe Biden atangaza kutogombea nafas ya uras wa marekani kupitia chama chake cha Democraty.

Narudia kusema katika mambo matamu yafuatilia basi ni pamoja na uchaguz wa marekan 2024.

Post ya majuzi niliweza gusia hili na kuelezea jinsi gani vigogo wa chama cha democratic wanataka Biden kutoendelea na nafas ya kugombea urais kwa maslah mapana ya chama na taifa na leo hii Biden hana namna kaamua achie ngaz.

Biden ammpigia chapua aliekua makamu wake wa rais Bi K**ala Harris, hatujui k**a Democraty watampitisha au laa, japo kuna wapo waliokua wanahitaj K**ala achukue nafas ya Biden.

Naomba nitabili mapema hapa k**a K**ala akiwa mgombea urais wa chama cha Democraty basi namuona Donald Trump Sr mapema sana anashinda uchaguzi huu mapema sana.

Moja K**ala hana ushawish hamfikii hata bi Hirary Clinton hata Nancy Pelos, ushawish wake mdogo labda atumia jenda yake na rangi yake ndo mana mapema tu baada ya Biden kuachia ngazi na kumpa chapua K**ala basi Donald kacoment juu ya hilo kwamba kumshinda K**ala Halissi ni rahisi sana tena mnoo kuliko Joe biden, mana yake mtu atakae letewa ni mwepesi sana.

Lakin niamini wanangu gender ya K**ala nayo yaweza mpoza hawa watu wanatuambiaga mambo ya democrasia mara haki sawa but wenyewe kuna sehemu ukipagusa hawafuatii democrasia wala haki sawa, majama wanaubaguz trust me uyu mwanamama halambii na yawezekana hata chama chake kisimpitishe mana wanaogopa anguko wakat wa uchaguzi.

Uimara wa wagombea uras a Republican ni upo moto sana hapa Donald Trump pale JD Vance ambae ushawish wa JD Vance tuu as Running partner wa Trump ni mkubwa sana, JD Vance ni karata sahahi aliyoichanga Trump kuelekea uchaguz huo.

Muda mwingine tutatazamie why Trump alimchagua seneta uyo wa Ohio kuwa mgombea mweza wake llihali hawakua na ukaribu na wala mahusiano mazuri.

All in All wazee wenzetu wapo na uwajibikaji wapo na democrasia japo wapo na unafiki mwingi la swala la kuwajibika tuu wapo njema sana, wanawaza taifa than maslahi yao tofaut na sisi ambapo tunawaza sana maslahi binafsi kuliko maslahi ya umma, mtu kuachia ngazi tena ukiwa na power hahah not in Afrika brother, mwambie Tinube kule Nigeria ajiuzullu haahah, hapa Tz tuu panga pangua zote zile sababu ya kueka safu ya kumuunga mkono na yenye kumtii hahahaha.

Ni mimi Drim Bway Defya

20/07/2024

Oyaaaa wanangu wa kuconspirancy mzee Biden washaanza kumkataa wanadai apige chini kuendelea na nafasi ya ugombea Urais, nini shida basi shuka na na hii post.

Katika mambo matamu yafuatilia basi ni pamoja na uchaguz wa Amerika una raha sana, unambiwa wanachama wa chama cha Democraty ambacho ndo chama cha Joe biden wanamshinikiza atangaze kutogombea urais ambapo novemba mwaka huu USA wanatarajia kufanya uchaguzi mkuu.

Mambo yanazid kuwa ya moto kwa babu Joe na hapo ni baadhi ya watu wenye heshima na nguvu Marekan na pia ndan ya chama chao cha democratic kuomba Biden apige chini.

Chama chake cha Democraty wanaona Biden hana tena uwezo wa kupambana na Trump, wanaona stamina ya akil haitoshi, lakin pia udhaifu huo unawapa nguvu chama cha Donald Trump Republican wanachukua udhaifu wa afya ya Biden katika kampeni zao.

Mwanamama Nancy Pelosi ambae alikua speaker wa Bunge la marekan, mtu k**a senete Chuck Schumer ambae uyu jamaa ndo kiongoz wa maseneta wa marekan, lakin mtu k**a Hakeem Jafffries jamaa ni naibu speker , lakin na seneta wa Calfonia Adam schiff nae waz wazi kamkaanga Joe Biden asigombee Urais, hao ni wachache tuu kat ya weng wapo magavana wengi ambao wameonyesha kuumtaka Biden apige chini.

Labda utajiulza why wanataka Biden apige chin?? but the major reason ni umr wa Biden na matendo yake ambayo yanaonyesha Mental stamina yake haipo sawa, swala hili haljaaza leo au jana ni tangu awe rais weng wa wamarekan wamekua wanambeza na matendo yake ambayo yanaonesha Biden hana haifai.

Afya ya Biden pia ni tatizo sana hii na fananisha na 2015 uchaguz mkuu wa hapa Tanzania ambapo mgombea rais wa muungano wa vyama vya upinzani (UKAWA) kupia chama cha CHADEMA Mh Edward Ngoyae Lowasa ambapo CCM walitumia sana udhaifu wa afya ya Lowasa katika majukwaa kueleza kuwa hafai na hili jambo ndo sasa linajitokeza uko USA.

moja ya mambo yaliyochagiza Biden aaombwe asiendelee ni mdahalo uliofanyika mwezi uliopita ambapo uliwakutanisha Joe Biden wa Democratic na Donald Trump sr wa Republican ambapo Biden alionyesha udhaifu kwenye kuongea na matendo ambapo Trump alpaa ujio.

The question is who will replace Joe Biden?? K**a Biden akisema hatogombea nafas ya Urais ni nan atakua mgombea urais kupitia chama cha Democraty??

Wapo wanasema K**a Haris anaweza faa ambae ni makamu wa rais wa USA, but wapo wanapinga kwa kuona K**ala hafai na hana uwezo wa kucompete na Trump.

Lakin watalamu wa sayansi ya siasa wanaona anguko la Democraty k**a vile Bden ataachia ngaz sababu itazidsha nguvu kwa Trump na republican lakin wapo wanadai na inaweza ikawapa moral democraty sababu kuna wengi hawavutiwi na Trump lakin Bden wanaona sio mtu sahihi ivyo inawafanya wawe njia panda na wengi wanajikuta hawajui wafanye nn.

Biden kasimamisha kwa muda kampeni za uchaguzi sababu ya "COVID" baada ya kupimwa na kukutwa yupo na Covid19 na hii inafanya Trump na chama chake wapate political miallege.

Huatujui nin kitaendelea lakini Democratic na Biden wapo kiti moto na chama kishagawanyika, lolote litapotokea litachukua muda kufanya Democratic wawe sawa.

Ni mimi Drim Bway Defya

Photos from Siasa za kimataifa na Kitaifa's post 13/07/2024

EUROPEAN UNION NA NATO WAVYOINGIZWA CHA K**E NA JASUSI MBOBEVU VLADMIR PUTIN RAIS WA URUSI

oyaaa wanangu wa kuconspirancy kwanza kitambo sana humu aseee, acha leo turuke na hii hapa ya jasusi mbobevu wazaman wa KGB (SVR&FSB kwa sasa baada ya USSR vunjika) avyowaingiza chakike mabwanyeye wa ulaya na umoja wa kujihami na wakajaa.

Mwaka 2021 kupindukia mwaka 2022 paliibuka minong'ono mingi sana na haswa ya kwamba yaweza Urus akaivamia Ukrain tokana na msuguano wa tangu 2014 kuongezeka sana, na mara zote Urus hakuweza thibitisha hilo.

Intel za majasus wa Amerca (CIA) na mashirika mengine ya kijasus ya ulaya k**a MI6 ya uingereza wanachakarika kutaka jua undan wa kinachojil uku Urus na hii yote sababu ya jesh la urus limeongeza mazoez yasioyakawaida na pia wamesogeza majesh karibu zaid na mipaka ya Ukrain, na mara zote Mrusi hajatia neno.

mnamo mwaka 2022, POTUS (President Of The United State) bwana Joe Biden anapokea habari zenye utata ndan yake na wazokua wanahisia lakini hawakuamini k**a za weza toea, habari izo zinatoka moja kwa moja mjin Langley uko Virginia palipo makao makuu ya ujasui wa marekan.

Joe biden anamua kufumua habari hewan ya kwamba muda si mrefu au masiku machache yawezekana Urusi ikaivamia Ukrain, na kuionya Urus kwamba hawatokubali hilo litokee, na k**a ada baada ya mmarekani kufyata na mataifa shiriki yakafyata kumuonya mrusi.

Naam bas hazikupita siku nyingi toka Biden atangaze hilo, Urusi kwa mara ya kwanza anatangaza special operation ambpo alitoa tahadhari na kuwaonya Ukrain muda bado upo wanaweza badil mawazo yao, lakin Ukrain alikaza na yeye akatangaza hal ya hatari na watu wakaanza jitolea kujinga na jeshi kujiandaa na vita.

Tarehe 24 mwenz wa 2 mwaka 2022, Russia anaingia rasmi, kwa kile anachokiita Oparesheni maarumu na sio vita, akitaka, Ukrain wasitishe mara moja mipango ya kujinga na NATO, na European Union.. ambapo opereshen yake ikaambatana na mambo yafuatayo moja kuipunguza ukrain nguvu ya kijesh kwa kuripua maeneo ya kamb za jesh na silaha, 2 kuyanyakua maeneo ya Luhansk na Donbas au Donesksy ambayo ni maeneo yalyotaka jitenga na Ukrain kwa miongo kadhaa, jambo la 3 ni kushambulia maeneo ya kimkakat ya Ukrain.

Wanangu hapo juu ulikua utangulizi wa hii makala sasa ndo tunazama kwenye mada husika.

Wakat vita vinaanza Umoja wa ulaya na NATO walianza wasaidia Ukrain kwa maficho na wakawaekea Vikwazo vingi sana Urus vya kiuchumi, siasa na hata kijamii, badae umoja wa kimatafa nao wakaweka nao vkwazo vyao, badae haina budi ikabidi Umoja wa ULaya na NATO waanze wasaidia wazi wazi kijesh na kifedha Ukrain.

Naweza nikasema wakati vita vinaanza wengi walijua Urus amekurupuka na hawezi toboa sababu ya vikwazo avyopewa na msaada anaopewa Ukrain, lakin mambo yanavyozd kwenda yamefanya tuone wazi wazi waliokurupuka ni mabwanyeye wa ulaya.

Naweza sema jasus Putin alijipanga vizuri sana na alijiandaa na vita kwa muda mrefu na sio hadi majasus wa ulaya na Amerika kuja kupata habari walichelewa sana na bado Putin muda wote alkaa kimya na wengi walijua mazoezi ya kijeshi yaloshika kasi ni 'GUNBOAT DIPLOMACY' yani Urusi inatumia kuweka jesh mipakani li kuwatisha Ukrain na wafane vile Russia amesema.

Puttn master mnd na yeye akawaacha wajue wanachofanya Russia n Gunboat Diplomacy na wala hawana mpango wa kuvamia ni vitisho tuu na Ukrain akajua vitisho na akaanza vimba bichwa analopewa na Umoja wa nch za ulaya na Nato, muda wote Putin hakuonyesha dhamira ya k**a anampango huo.

Hamadii Putin anatangaza opreshen yake ya kijeshi, na hapa pia akawahadaa mara ya nyengine mabwanyeye wa ulaya, wao walona Putin anangia vitan sababu tuu labda ameona hamna namna baada ya vitisho vyake kugonga mwamba, mana wao walijua vile vilikua ni vitisho hata waje kataa ila waljua jamaa anatishia tuu, sasa avyoona anazama vitan bado wakajua kakurupuka na atampiga na vikawo.

sasa ni miaka miwil na miez mi nne tangu vita vianze, nan? alikurupuka??

moja uchumi wa Urus upo stabble (umeimarika) tofaut na uchumi wa Ulaya, na America na hata dunia nzma uchumi umepuyanga, kibiashara japo Urusi kawekewa vikwazo lakin baishara zake zimezid imarika.

Kisiasa tumeshuhudia hali ya maandmano mbalmbal kwa nch za umoja wa Ulaya na mizozo mbal mbal tangu vta viaze kutokana, Bunge la Amerika lligawanyika juu ya masuala ya misaada wanayowapa Ukraina had speaker wa nch iyo jiuzuru, tumeshuhudia vyama vilvyshika dora vya ulaya kupoteza mvuto na kuondolewa katika nafas zao mfano uchaguz wa majuz uingereza na Ufaransa na bado tunaona Biden hana maisha white hause uchaguz ujao.

tumeona ushawshi wa Urus hapa Afrka uvyoimarika mnoo na umoja wa ulaya na Amerika wakipoteza mvuto, mfano Ufarasa kapoteza nch zake azowah zikolon k**a tatu, US kutimuliwa katika kambi za jesh uko Afrika ya Magharib na kati.

Kubwa zaid Urus ameshachukua asilimia zaid ya 15 aliyokua anamiliki Ukrain.

Russia aliwatega afu wao wakajaa mazima, naamini hii vita visengetokea k**a tuu Umoja wa Ulaya na Amerika wangepata Intel zilizosahihi na wangegundua mapema kwamba Urus aljipanga na sio tuu kivita bali, kchumi, biashara, na mengneyo.

Mapuuza yao na yamewafikisha hapo na bla sahau wameaponza Ukrain hata waseme leo hi Ukrain ajiunge na NATO au Umoja wa Ulaya hamna cha kumzuia mrusi,.

Busara zingetumika mwanzo kumtuliza Mrus haya yasingefika, na wao Ulaya kuacha kuonyesha adhma ya kumpokea Ukrain na wala kujiunga NATO, hapa tusingefika, na ndo mana Donald Trump anajinad angekua madaraka bas Urus isingevamia Ukrain.

kachero mbobevu wa Moscow amewachezeshea shere, plan za kubutua alikua nazo muda sana tena sana na majasusi wa ulaya na langley wameshindwa pata taarfa zaiid ya zile azoamua yeye kuwapa, na badae wanakuja jua jua lishazama wanajipa habar za jamaa kakurupuka lakin leo hii wao ndo wanahaha sasa wanatuma njia ya ugaid kushambulia Urus.

kwa leo tuishie hapo.
nii mimi Drim Bway Defya

Photos from Siasa za kimataifa na Kitaifa's post 29/06/2024

wazee wa kuconspirancy, hiii imekaaje asee?? ndani ya miezi mitatu ndege tatu za kijeshi muundo wa Helikopta zimepata ajari zimetokea na kuhusisha viongoz wa nyazfa za juu katika nchi husika kuna mengi yamesemwa na yamehusishwa na ajar izi twende sawa wazee.

Tukianzia hapo tuu kwa majiran zetu nchini Kenya mnamo tarehe 18 mwezi wa 4, mwaka huu 2024 aliekua mkuu wa majeshi wa nchi iyo meja jenerali Francis Ogolla, alipata ajari ya ndege ya kijesh ya nchi iyo akia na wenzie 9 maeneo ya Kenya ya kaskazini.

Mwezi mmoja badae yani tarehe 19 ya mwezi wa 5 ya mwaka huu 2024, uko Iran ilitangaza kuanguka kwa helikopta ya jeshi iliombeba Rais wa nchi iyo pamoja na viongoz wengine akiwemo waziri wa mambo ya njee ya nchi iyo na mnamo tarehe 20 wakathibitisha tokea kwa kifo cha Rais wa nchi iyo Ebrahim Rais katika safu ya milima ya nchi ya Azbaijan akirud Iran, na habar hii ilichachafya duna mayb ingeleta mzozo k**a ajari ingekua ya kupangwa but Mungu mkubwa ni ajal ya kawaida.

Mwez hata haujaisha vizur tunapata habar zengine toka kwa majirani zetu wa ziwa nyasa yan Malawi, habari mbaya ya kupotea kwa ndege ya aliekua Makamu wa Rais wa nchi iyo Saoulos Chilima hii ilikua ni tarehe 9 ya mwez wa 6 mwaka huu 2024, ambapo alikua yeye na wenzie 9, siku moja baadae yan tarehe 10 ikatoka habar ya ndege kupatikana na hakuna aliepona.

sasa wazee wakuconspirancy wanasema haka katabia kamerejea baada ya miongo kadhaa pita, viongoz wengi walipata ajari za ndege iwe ajar k**a ivyokua kwa Samora rais wa Msumbiji na John de lange de Mabior makamu wa Ris wa Sudan na Rais wa Sudan ya kusin au iwe kwa kudungua ndege k**a ivyotokea kwa Rais wa Rwanda wa enz izo Hybraimana.

Jinsi ilivyo ndege za kijeshi zikipata ajari basi uchunguz wake huo tofaut na ndege za abiria, ndege za abiria huchunguzwa na kampuni lyotengeneza ndege na kuja na majibu but about ndege ya jeshi uchunguz wake ni aupo k**a ivyo so uchunguz hufanya na jeshi na serikali yani hua ni state matter.

Juu ya hili wazee wa kuconspirancy wanadai yaweza ikawa kuna mchezo huchezwa ndan ya nch na izi ajari sio natural bali ni artificial.

Ajar ya mkuu wa majeshi Kenya watu wanahusisha na kuna kanamna sababu yadaiwa k**a Ruto ingelikua idhin yake bas asingempa uCDF jeneral Ongolla but sababu a katiba hapakua na namna yadaiwa CDF uyu na Mkuu wa nchi hawakua na ukaribu, tuyaache hayo wazee wa kuconspirancy ndo wanadai.

Back to Iran, mwanzo ilionyesha k**a USA au Israel wapo nyuma ya Ajar h but Iran wamekanusha lakin habar nyngine ni Ebrahim Rais alikua anatarajiwa chukua cheo au wadhfa wa juu kabsa ambao ni Kiongoz wa heshima ambao upo chini ya Ayyatollah so wanadai labda kuna namna but wapo wanadai labda jamaa alitaka salilit so wamemuawah yote yanabaki kua ni story za maconspiriensa tuu.

Tukimalizia hapo Malawi napo story ni nyng unajua makamu wa Rais na Rasi mwenyewe wameungana tuu but vyama vyao havikua vimoja kuna madai labda Chakwera (Rais wa malawi) kaogopa yale yaliompata Uhuru Kenyata na bwana Ruto yasije jirudia au aliziona dalili, sio mimi nilie sema haya bali wazee wa njama wazee wa kuconspiriancy.

All in all hakuna ajuaye so tuamini vyanzo mama ambayo vinathibitisha izi ajari zote ni ajari za kawaida nahakuna mpango wowote ule.

ni mimi Drim Bway Defya

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Mwalim Nyerere Road
Dar Es Salaam