27/05/2026
IMETOLEWA NA ;
TUMA WAZO BUNIFU KUBORESHA HUDUMA NA MIFUMO YA KODI, USHINDE HADI MILIONI 50
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa fursa kwa Watanzania wabunifu kushiriki katika msimu wa pili wa kuwasilisha mawazo bunifu yatakayosaidia kuboresha huduma za kodi, kurahisisha mifumo ya utoaji huduma za TRA pamoja na kuongeza wigo wa kodi nchini.
Watanzania wanahamasishwa kuwasilisha mawazo yao kupitia tovuti ya Mamlaka katika kipengele cha Innovation, ambapo mwisho wa kutuma mawazo ni Julai 31, 2026.
Mawazo 1,000 yatakayofika kwenye Evaluation Committee yatapatiwa shilingi 100,000 kwa kila wazo. Kati ya hayo, mawazo 20 yatakayofanikiwa kushinda yatapata zawadi kubwa ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi 50,000,000, mshindi wa pili na wa tatu shilingi 30,000,000 kila mmoja, nafasi ya nne na ya tano shilingi 20,000,000 kila mmoja, huku nafasi ya sita hadi ya ishirini (6th–20th) wakizawadiwa shilingi 10,000,000 kila mmoja.
Kwa ujumla, jumla ya washindi 1,020 wanatarajiwa kunufaika na mpango huo unaolenga kuibua na kuendeleza ubunifu utakaosaidia kuboresha mfumo wa Kodi nchini".
KODI YETU , MAENDELEO YETU! Kwa pamoja Tunajenga Taifa Letu.