25/11/2021
USHAURI WA BURE KWA VIJANA WASOMI (WAHITIMU) na Mushobozi.
1. Tunaamini Vijana wengi tunatoka familia duni na za Vijijini. Wakati mwingine kula milo miwili katika familia zetu ni tatizo.
2. Unapobahatika kupata nafasi ya kuendelea kimasomo jicho la mzazi linaanza kukutazama k**a mkombozi wa familia yenu. Hapo mzazi/wazazi hujitoa kwa kila kitu ikiwemo kuuza kuku, mbuzi, bata na mashamba lengo ni usome upate kazi ili uwainue wadogo wako na familia kwa ujumla.
3. Unakuta kijana anapata nafasi ya kwenda chuoni huku akiwa amebebeshwa mzigo wa matatizo yote ya familia yake.
4. Ila vijana wengi wakishafika vyuoni mizigo ya familia zao wanazitua chini na kuanza kuiga maisha ya vijana wengine ambao wakati mwingine hujui wao wanatoka familia ya namna gani, basi mnakuwa watu wa club, pombe, mademu/wanaume, iphone, na mwishowe vijana unaanza kukabiliwa na (SUP) za kutosha na mawazo yako yanakuwa ya ulimbukeni, na mwishowe wengine wanashindwa kuendelea na masomo (disco) na wanaobahatika wanamaliza chuo wakiwa na iphone 7, techno, infinix na G.P.A ya 2.5 huku kichwa kikiwa kina ziro kuhusu elimu ya mtaani.
4. Unarudi mtaani (Kijijini/mjini) ambako maisha yako yote yatakuwa huko (street) ukiachana na maisha ya mda ya chuo ya miaka mitatu, unaanza kusambaza barua za ajira mwishowe ajira hupati kwasababu waliohitimu mtaani ni wengi sana. Na ukibahatika unapata ajira za mateso (mshahara laki na nusu/laki mbili) na wakati mwingine hupati kwa wakati.
5. Hapo kumbuka wazazi wanakutegemea k**a mkombozi wao ajira serikalini ni finyu. Mwishowe na umri umesogea. Unaonekana mzigo katika familia mpaka wazazi wanaanza kukuchukia maana umekula kila walichokuwa nacho hujarudisha chochote na jembe ushasahau kushika ama hutaki kazi za shambani zinakuchafua.
6. Unaamua kwenda mjini kutafuta kazi na mjini ndo kuna hatari zaidi. Unatoa maamuzi ya kuishi dukani kwa muhindi huku (UNAOMBA KUFANYA KAZI YOYOTE) ilimradi mkono uingie kinywani huku familia yako kijijini inateketea na wewe umri unasogea 40's kwasababu umekaa shuleni miaka 23 na umehitimu ukiwa na miaka 30.
USHAURI
1. UNDA VIKUNDI
Vijana jifunze kutengeneza umoja mkiwa chuoni na baada ya kumaliza vyuo na kujenga mipango thabiti ya kushirikiana kwa kujijenga kiuchumi na Kwa kujiajili. Mkishakuwa na vikundi weka mikakati, andika miradi bunifu, sajilia vikundi vyenu katika ofisi za afisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata na wilaya, omba mikopo kutoka kwenye mifuko ya maendeleo ya vijana akina mama na wazee, JIAJILI kwa kuendesha miradi yenu.
Itaendelea...................