AL MADRASAT IHSAANIYYAH -kwa bi maif/tandale/dar es salaam/tanzania

AL MADRASAT IHSAANIYYAH -kwa bi maif/tandale/dar es salaam/tanzania

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from AL MADRASAT IHSAANIYYAH -kwa bi maif/tandale/dar es salaam/tanzania, Education, tandale kwa tumbo, Dar es Salaam.

17/09/2017

بسم الله الرحمن الرحيم
ASSALAAMU ALAYKUM WARAHMATU LLAAHI WABARAKAATUH.
VIPI HALI ZENU?
UONGOZI WA MADRASAT IHSAANIYYAH(KWA Bi maifu) ILIYOPO TANDALE KWA TUMBO KWA HESHMA NA TAADHIMA TUNATASHARRAF KUWAJULISHA/KUWAALIKA KATIKA SHUGHULI YETU YA MAHAFALI,NA KUMSHUKURU ALLAAH KWA MWAKA NA MIEZI KADHAA TANGU TUIFUFUE MADRASA HII,SHUGHULI YETU TWATARAJI KUIFANYA TAREH 28 na 29(j/mosi na j/pili)MWEZI WA KUMI,....
MATUKIO YA KUFANYIKA NI:
(1)JUMAA MOSI: MAONESHO YA MADA KWA VIJANA NA MASHINDANO YA QURAAN NUSU JUZUU(muda kuanzia SAA Tisa alasiri)
(2)JUMAA PILI: MASHINDANO YA QURAAN JUZUU MOJA MBILI,NA TATU(inshaa allaah).
(3)ZOEZI LA UGAWAJI VYETI KWA WAKHITIMU (tuloanza nao alif na wakahifadhi juzuu walizojaaliwa na hadithi 40 kuendelea alhamdulillaah)
MUDA: KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI MPAKA ADHUHURI,.
shime alaykum wapenda kheri,na WAISLAMU wote KWA ujumla(NA wasokua waislamu waje waone wasikie huenda allaah akawaongoa)
katika kulielekea hilo tumejitahidi mpaka tulipofikia bado nguvu yetu imekua ndogo twaomba kila mpenda kheri awekeze KWA hili,qauli mbiu "MAADUI WA UISLAMU WANAWEKEZA KWA KUHARIBU UMMAH WA KIISLAMU,SIE TUWEKEZE KUHUISHA UISLAMU WETU"
mahitaji ya shughuli ni k**a vile:
(1)zawadi za washiriki= takriban laki tatu
(2)maspika ya kukodi =laki na nusu
(3)mchele kilo 200 == laki tatu na sittini
(4)maji ya kunywa == laki moja
(5)turubai kukodisha=laki na sittini
(6)nyama kilo 80 == laki NNE na themanini
(7)viti na mikeka.
(8)upishi
n.k
KWA CHOCHOTE ULICHOJAALIWA TWAHITAJIA SWADAQA YAKO KUWEZESHA JAMBO HILI KWA AJILI YA ALLAAH,NA TARAJI MALIPO KWAKE.

watumishi wenu:
alfaqeer said Sayyeed Saalim El Bakry(abuu salim)0713388866.
maallim khalfan ally balo: 0659238207
shukran na allaah atuwafiqishe ktk kila yenye kheri

21/08/2017

بسم الله الرحمن الرحيم
MAHIMIZO YA KUZIDISHA MATENDO MEMA KATIKA KUMI LA MWANZO LA DHUL HIJJA/MFUNGO TATU {NO 02]
naam baada ya kuona baadhi ya nuqta muhimu,na kutazama viapo ambavyo allaah ameapa mwisho wa kiapo ak**alizia kwa maneno ya kua: "HAKIKA KATIKA VIAPO HIVYO KUNA MAZINGATIO KWA WENYE AKILI"
naam na mazingatio huja baada ya kukijua kitu ndio utaona leo kwa kutojua thamani mtu huona hayana maana masiku haya,na wapo watu husema ni uzushi kufunga siku tisa za mwanzo za mwezi huu,je wanazo akili?maana yafaa kuuliza akili kabla ya mazingatio,kwani allaah ameweka mazingatio kwa wenye akili pekee tumuangalie mtume s.a.w akituelekeza yepi mazuri ya kufanya,au akitutaka tujipinde kufanya mazuri katika 10 la mwanzo kwenye mwezi mtukufu wa dhul hijja:
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
"ما من أيام التي العمل الصالح فيها أحب إلى الله من هذه الأيام -أي العشر من ذي الحجة -
قالو: "يا رسول الله ولا الجهاد في سبيل الله"؟ قال: "ولا الجهاد في سبيل الله إلا رجل خرج بنفسه وماله فلم يرجع من ذلك بشيئ" {رواه البخاري}
imetokana na abdillaah ibn abbaas r.a asema: amesema mtume s.a.w: "HAKUNA MASIKU MIONGONI MWA MASIKU AMBAYO MATENDO MEMA YANAPENDEZA ZAIDI KWA ALLAAH KULIKO MASIKU HAYA -kumi la mwanzo la dhul hijja-[jumlatul i3tiraadhwiyya haipo katika hadithi bali yafafanua] akaulizwa na maswahaba: "EWE MJUMBE WA ALLAAH HATA KUPIGANA KATIKA NJIA YA ALLAAH?" akajibu mtume s.a.w "NDIO HATA KUPIGANA KATIKA NJIA YA ALLAAH ISPOKUA MTU ALIETOKA YEYE NA MALI YAKE NA HAKIKUREJEA CHOCHOTE"[yeye kafia kwenye jihaad na mali yake haikurudi][ameipokea hadithi imaam bukhaar ktk swahiih yake]
naam twaona kua katika masiku hayo matendo mema yapendeza zaidi kwa allaah,si kua kwenye masiku mengine hayapendi,laa bali kwenye masiku haya huwa kuna nyoongeza zaidi ya twawabu,na hili limethibiti la nyoongeza kwa kuzingatia mambo kadhaa k**a vile:
[1]MUDA/NYAKATI: mfano ni hadithi hiyo tuliotoka kuiashiria ndani ya masiku kumi hayo nyoongeza inavyokua,pia mfano wa pili ni pale allaah aliposema: "ليلة القدر خير من ألف شهر"
"usiku wa cheo/mtukufu/wenye kubanwa/wenye kupangwa mambo ni bora kuliko miezi alfu moja" [suuratul qadr aya ya 3]

[2]بإعتبار المكان: KUZINGATIWA SEHEMU HUSIKA
ni mfano wa ibada ya swala mtume s.a.w aliposema: "صلاة في مسجدي هذا أفضل من ألف صلاة فيما سواه إلّا مسجد الكعبة"
"swala katika msikiti wangu huu ni bora kuliko swala alfu moja katika misikiti mengine ispokua msikiti wa makka"
[3]KUZINGATIA KINACHOTENDWA [IBADA] k**a alivyosema allaah ktk hadithi qudsi kuahusu kujiqurubisha kwa aloyafaradhisha,maana yake ni kua SWALA YA SUBHI NI FARADHI,na ina rakaa mbili,qiyaamu llayl ni sunna unaswali utakazo[mbili mbili] sasa mtu aamue kukesha usiku akiswali sunna halafu swala ya subhi asiswali,pamoja na kuswali kwake rakaa 8 au 20 usiku ila kule kutokuiswali swala ya subhi yupo makosani kaacha waajib huyo kwa kujitia aswali mno sunna.
[4]KUZINGATIA MFANYAJI WA IBADA[kitendo] mtume s.a.w asema:
"لاتسبوا أصحابي،فو الذي نفسي بيده لو أنفق أحدكم مثل أحد ذهبا ما بلغ مد أحدهم ولا نصيفهم"
"msiwatukane maswahaba zangu,naapa kwa allaah yeyote miongoni mwenu lau atoe swadaqa mfano wa mlima wa uhd dhahabu tupu,hawezi kufikia kibaba chao au nusu yake[nusus kibaba] [bukhar na muslim]
hapa utaona utofauti mkubwa uliopo baina yetu na maswahaba,vivo hivyo pana utofauti kati yetu kulingana na iimaan,ikhlaasw,mutaaba3 n.k.
ukizingatia mifano hiyo minne tuloiashiria wala hutopata tabu katika kufanya mema kwenye miezi mitukufu,k**a aya tuloashiria darsa iliyopita allaah atuhimiza kutenda mema katika masiku hayo matukufu miongoni mwa mema ni kufunga siku tisa za mwanzo[haraam kufunga siku ya kumi ya mfungo tatu] na ikiwa wanatokea washadadivu na kuharamisha na kusema ni bidaa kufunga siku tisa za mwanzoni ktk mwezi wa dhul hijja basi waje na hoja zao,wapo wasemao bidaa,ni kutoa lugha kali kwa wafungao,sasa wala pasizungushwe kwenye mafhuum ya bidaa pawekwe sawa tu je kufunga ni bidaa?au uvivu wetu wa kufanya ibada tu?au kujua kwetu kwingi tumewazidi hata walotufundisha dini?
kwa haraka tutaweka siku ambazo hazifai kufunga:
[1]SIKU ZA EID MBILI:
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أنّ رسول الله صلى الله عليه وسلم نهى عن صيام يومين: يوم الفطر ويوم النحر.
baba said lkhudriyy r.a asema "hakika mtume s.a.w amekataza kufunga ktk siku mbili,siku ya fitr[wanayofungua watu,siku ya kwanza mfungo mosi/shawwaal]na siku ya kuchinja[siku ya kumi mfungo tatu}[bukhar na muslim]
na hapo twaona hiyo nahy ni:النهي يقتضى التحريم"

[2]MASIKU YA KUANIKA NYAMA/YA KUTAWANYIKA[siku tatu baada ya eid el adhwhaa]
mtume s.a.w asema:
"أيّام التشريق أيام أكل وشرب وذكر الله عز وجل"
"masiku ya kutawanyika ni masiku ya kula na kunywa na kumtaja allaah"[muslim]
ktk hadithi nyengine mama aisha r.a asema "hatukuruhusiwa kufunga ktk masiku ya tashriiq ispokua kwa yule alokosa mnyama wa kuchinja'[bukhar][kwa mahujjaaj]

[3]KUFUNGA SUNNA SIKU YA IJUMAA PEKE YAKE[kinyume na sunna k**a vile arafa,ashuraa,yakusudiwa mtu aloamua kufunga ijumaa peke yake sunna yake]mtume s.a.w asema:
"لا يصومن أحدكم يوم الجمعة إلا أن يصوم يوما قبله أو يوما بعده"
"asifunge mmoja wenu siku ya ijumaa pekee ispokua afunge siku moja kabla yake[alkhamis]au siku moja baada yake[j/mosi] [bukhar muslim]
pia kuna kufunga siku ya shakka haifai,ajabu mtu leo anaharamisha kufunga siku tisa hizi kwa dalili gani? au kufunga si katika matendo mema?ifahamike dini yetu si dini ya midadi mtu mdadi ukimpanda aseme au afanye lolote,wala mambo ya ibada hayataki ushabiki kisa kasema fulani mie nafuata,tuweke kituo kwa kutaja baadhi ya mema ambayo tujipinde kwayo ktk masiku haya:
[1]KUTUBIA KIKWELI
[2]KUSWALI SWALA ZETU KWA JAMAA
[3]KUFUNGA SIKU TISA
[4]KUJIPINDA KUSOMA QURAAN YOTE
[5]KUUNGA UDUGU
[6]KUKITHIRISHA KUTOA SWADAQA
[7]KUKITHIRISHA KUMSWALIA MTUME S.A.W
[8]KUFANYIA WEMA WAZAZI NA NDUGU
[9]KULISHA MASKINI NA MAYATIMA NA KUWAVISHA
[10]KUDUMU NA IBADA ZA SUNNA
[11]KUJIPINDA VISIMAMO VYA USIKU
[12]KUTEMBELEA WAGONJWA
[13]KUREJESHA AMANA[KULIPA MADENI]
[14]KUFANYA DHIKRI
[15]KUCHINJA SIKU YA 10.
n.k
n.b kwa wote waloazimia kuchinja wanatakiwa wajizuie kunyoa nywele zao zote,na kukata kucha kuanzia mwezi utakapoandama mpaka baada ya kuchinja,hivyo ni bora zaidi kunyoa sehemu zote mapema,na kukata kucha kabla mwezi haujaandama[tutaifafanua]
tuweke kituo inshaa allaah tukipata wasaa tutaendelea.
rukhsa ku share na wengine wanufaike,itakua umefanya wema na allaah atauhesabu wema huo
MTUMISHI WENU
ALFAQEER SAYYEED SAALIM EL BAKRY[abuu saalim]

30/06/2017

بسم الله الرحمن الرحيم
ALHAMDULILLAAH kwa wingi wa kheri zake kwetu,na rahma zake kwetu,rehma na amani zimfikie mtume wetu muhammad s.a.w na jamaa zake na swahaba zake,naam leo TUKUMBUSHANE au TUFUNDISHANE wazazi wa mtume s.a.w upande wa baba yake,yaani baba zake na shangazi zake,na unuani yetu inabebeba jina la:
WATOTO WA MZEE ABDUL MUTTWALIB
k**a tunavyofahamu kua mtume s.a.w aitwa MUHAMMAD ibn ABDILLAAH ibn ABDUL MUTTWALIB,,sasa twaangalia watoto wa babu yake mtume s.a.w mzee huyu alikua na watoto kumi na sita[16] wa kiume ni kumi na wanawake ni sita,tukianza kuwataja hao wa kiume kwa haraka haraka ni:
[1]ABBAAS
[2]HAMZA
[3]ABDULLAAH [baba ake mtume]
[4]ABUU TWAALIB [jina lake ni abdi manaaf]
[5]ZUBAYR
[6]HAARITH
[7]JAHLAA
[8]DHWIRAAR
[9]MUQAWWAM
[10]ABUU LAHAB [jina lake ni abdul u'zzaa]
ama upande wa wanawake ni
[1]SWAFIYA
[2]UMAYMAH
[3]UMMU HAKEEMUL BAYDHWAA
[4]ARWAA
[5]A'ATIKAH [atike][عاتكة]
[6]BARRAH
hiyo ndio idadi yao ukitazama kwa umakini wapo maarufu na wapo wengine walikua hawafahamiki,wapo ambao mpaka aya za quraan zimewashukia,ama tukiangalia mama zao ni hivi:
ABDILLAAH,ZUBEYR,NA ABII TWAALIB,UMMU HAKIIM,AATIKAH,UMAYMAH,ARWAA NA BARRAH,hawa ni baba mmoja mama mmoja na mama yao[ambae ni bibi yake mtume mzaa baba] aitwa: FAATWIMA BINTI AMR,AAID,IMRAAN,MAKHZOUM,YAQADHWAH,MURRAH,IBN KA'AB,LUWAYY,GHAALIB,IBN FIHRI,MAALIK,NNADHWRI,KINAANAY.
ukitazama kwa makini utaona babu wa nne wa bibi faatwima anaungana nasabu yake na mumewe mzee abdul muttwalib.na mama wa bibi yake mtume aitwa SWAKHRAH bint ABDI,IBN IMRAAN,IBN MAKHZOUM napo ukiangalia silsila ya kinasaba utakuta mama ake mkubwa[mama ake bibi ake mtume]aliolewa na ndugu yake kinasaba[.
tukiangalia mama ake ABBAAS na DHWIRAAR anaitwa: NUTAYLAH bint JANAABI.
ama mama ake HAMZA na MUQAWWAM na JAHL na SWAFIYYAH, anaitwa; HAALAH bint UHAYB,ibn ABDI MANAAF,IBN ZUHRAH,IBN KILAAB,IBN MURRAH,IBN KA'AB,IBN LUWAYY,[pia nasabu yake yaungana na mumewe,na yaungana na bibi yake mtume s.a.w]
ama mama ake ABUU LAHAB ni: LUBNAA bint HAAJIR,IBN ABDI MANAAF IBN DHWAATWIR IBN HUBSHIYYAH IBN SALUUL IBN KA'AB IBN A'MR IBN KHUZAAI'YY.
ama tukimalizia mama ake HAARITH ni: SAMRAAU au SWAFIYYAH BINT JUNDUB.
naam hapo ndio uchache wetu unapokomea,kwa kufahamu angalau jina lala bibi yake mtume s.a.w na watoto wa mzee abdul muttwalib,siku kadhaa nyuma yupo mtu aliambiwa "nitajie jina la bibi yake mtume s.a.w mzaa baba ukipatia nakupa elfu khamsini" yule bwana ikabidi akiri kutomjua bila natija kupatikana hivyo tuwajue japo kwa majina,sio tuwajue wacheza mpira na wasanii na wanasiasa pekee.
MTUMISHI WENU
ALFAQEER SAYYEED SAALIM EL BAKRY

23/06/2017

بسم الله الرحمن الرحيم
[FIQHI YA FUNGA NO 15]
alhamdulillaah baada ya ukimya wa muda mrefu ambao hatukua na budi zaidi ya kuridhia qadar ya allaah leo tumepata fursa japo kidogo kuandaa darsa yetu ambapo itabidi turuke vipande vingi ili twende na masiku husika,na tutatazama jambo muhimu ndani au baada ya ibada ya funga,nalo ni:
زكاة الفطر:
ZAKAATUL FITRI:
kisheria ni swadaqa ambayo hutolewa kwa kufungulia ramadhani,.
HEKMA YAKE:
ni kufanya ukaribu na mafuqara,na kuingiza furaha ktk nyoyo zao na majumba yao,kwani eid ni siku ya furaha na furaha yapendeza waislamu wote kufurahika,si hawa wafurahi kwa kula na kunywa na kubakisha halafu wengine hawana chakula,na pia zakaatul fitwri inasafisha makosa madogo madogo aloyafanya mtoaji wakati alipofunga,
حكم زكاة الفطر:
HUKMU YA ZAKAATUL FITWRI:
hukmu yake ni waajib kwa kila muislamu,na wamekubaliana juu ya uwajibu wake[bidaayatul mujtahid 500]
MAHANAFI WAO WANASEMA:
hukmu ya swadakatul fitwri ni waajib kwa sharti zifuatazo:
[1]uislamu
[2]kua huru
[3]kumiliki kiwango cha kutoa.
MAHANAABILA:
zakaatul fitri ni waajib tangu kuzama kwa jua usiku wa eid kwa kila mwenye chakula cha kula nyumbani kwake na ziada,baada ya kukamilisha mahitaji ya walio chini yake[kimalazi]na atajitolea yeye na kuwatolea walio chini yake.
MASHAAFI:
zakaatul fitri ni waajib kwa kila muislamu na ni waajib kwa kafiri kumtolea mtumishi wake,
MAMAALIKI:
zakatul fitri ni waajib kwa kila muislamu huru,mwenye kuweza kiwango cha kutoa.
na imechukuliwa HUKMU YA UWAJIB WAKE katika hadithi ya mtume s.a.w
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: "فرض رسول الله صلى الله عليه وسلم زكاة الفطر طهرة للصائم من اللغو والرفث،وطعمة للمساكين،فمن أداها قبل الصلاة فهي زكاة مقبولة،ومن أداها بعد الصلاة فهي صدقة من الصدقات"
abdillaah ibn abbaas r.a asema: "mtume s.a.w amefaradhisha zakatul fitwri,inamsafisha mfungaji kutokana na upuuzi na maneno mabaya,na hutolewa kuwapa maskini,yeyote mwenye kuitoa kabla ya swala basi hiyo ni zaka yenye kukubalika,na mwenye kutoa baada ya swala[ya eid]basi hiyo ni swadaqa k**a sadaka nyengine" [abuu dawd 1609,ibn maajah 1827,alhaakim 409]
katika hadithi hii yapo mambo kadhaa mabayo twajifunza:
[1]zakaatul fitwri ni jambo lilowajibishwa
[2]inamsafisha mtoaji alipoteleza ki maneno wakati aliofunga,na pale ambapo moyo ulimili katika ujinga.
[3]utoaji wake ni kuwapa wasiojiweza[wa karibu ni bora zaidi]
[4]utoaji wake ni tangu kuingia eid mpaka muda wa swala,baada ya swala inakua ni sadaka ya kawaida,kwa nini?kutoa mapema kunampa ahueni huyu maskini kujua kapunguziwa hili na kabaki na hili.
pia tukiangalia riwaya nyengine:
عن ابن عمر رضي الله عنهما قال:
"فرض رسول الله صلى الله عليه وسلم زكاة الفطر صاعا من تمر،أو صاعا من شعير،على العبد والحر،والذكر والأنثى والصغير والكبير من المسلمين،وأمر بها أن تؤدى قبل خروج الناس إلى الصلاة"
abdillaah ibn omar asimulia kua:
"mtume s.a.w amefaradhisha zakaatul fitwr pishi ya tende,au pishi ya shair,kwa mtumwa na mtu huru,kwa mwanaume na mwanamke,kwa mkubwa na mdogo katika waislamu,na ameamuru itolewe kabla watu hawajatoka kwenda kuswali"
[bukhaariyy 1503,muslim 984]
pia hapa kwa haraka twapata funzo kua ZAKAATUL FITRI NI CHAKULA KINACHOLIWA ZAIDI MJI HUSIKA,hivyo kwa sie east africa ni mchele,na wanaokula sana shairi wao shairi na tende na mtama vivyo hivyo.
asema saiid ibn musayyab na umar ibn abdul aziiz kuhusiana na qauli ya allaah:
"قد أفلح من تزكى"
wao wanasema kusudio hapo ni zakaatul fitri,.
amesema ibnil mundhir "tumekusanya kwa kila tuliechukua elimu kwake kua swadaqatul fitri ni fardhw"[ijmaai ya ibn mundhir kurasa ya 49]
JE NI NANI ALOWAJIBIKIWA KUTOA ZAKAATUL FITRI?:
[1]MUISLAMU,kwani tumeona zaka hii inamsafisha mfungaji hivyo kafiri hahusiki na ibada hii,hata kipimo cha funga pia hakufunga,na ukiangalia hadith ya ibn umar utaona wamekhusishwa ibada hii waislamu tu,na uislamu ni sharti kwa jumhuur ispokua imaam shaafi yeye asema kafiri afaa kumtolea mfanya kazi wake,au mtu wake wa karibu.
[2]KUWEZA KUTOA ZAKA HIYO
na sharti hii yatakiwa mtu awe na uwezo,na ukomo wa uwezo ni mtu kua na chakula cha kula yeye na watu wake siku hiyo ya eid na ziada k**a ipo ndio atoe,[jumhuur]sio mtu ajitie dhiki kukopa au kutanga huku na kule,ikiwa hana kweli na allaah ashuhudia basi asikope kwa kutimiza,bali allaah amjua na atamlipa kwa dhamira yake nzuri.na hapa ipo tabia ya watu wanacho cha kukila mchana na usiku wake lakini bado wanakusanya na kulimbikiza jambo hilo halifai,ikiwa umeletewa tafuta wa chini yako nawe mpe,kwani mtume s.a.w asema:
"mwenye kuomba hali ya kua anacho cha kumtosheleza hakika mtu huyo azidishiwa moto" maswahaba wakasema ewe mjumbe wa allaah kipi kiwango cha kutosheleza? mtume akajibu: "ni mtu kua na kiwango cha kula mchana na usiku wake"[abuu dawd 1629].
na je ikitokea ushatoa na ukapewa utafanyaje?au ikiwa una uwezo na ukapewa utakataa?lililo bora zaidi ni kuchukua na kuwapa walio chini yako,na zaka hii haikufungwa kua lazima kutoka juu kuja chini bali yaeza toka chini kwenda juu na wala hakuna kifungo katika hilo,kwani inamzindua na inamfanya nae aone haya huenda akatoa kwa ukumbusho huo wa kitendo..
KIWANGO CHAKE
ni takribani kiwango cha kilo mbili na nusu,au mbili na robo,na muda wa kutoa ni k**a tulivyoainisha hapo mwanzo.
JE INAFAA KUTOA ZAKAATUL FITRI KABLA YA MUDA WAKE?
naam inafaa kuwahisha zakaatul fitri kwa siku moja au kwa siku mbili.
عن نافع قال: "كان ابن عمر يعطيها الذين يقبلونها وكانوا يعطون قبل الفطر بيوم أو يومين"
naafi3 asema alikua abdillaahi mtoto wa umar akiwapa zakatul fitri watu wanaomuelekea[karibu]na walikua wakitoa kabla ya fitri kwa siku moja au kwa siku mbili" [bukhaariyy 1511,muslim 986]
JE HUONDOKA JUKUMU LA ZAKAATUL FITRI KWA KUONDOKA MUDA WAKE?
k**a tulivyoona katika hadithi kua yatakiwa itolewe kabla watu hawajatoka kwenda msikitini,sasa suali je muda ndio ushaisha na mchele hujautoa utaacha kabisa au utatoa hivyo hivyo?
jawabu ni kua wamekubaliana wanachuoni kua wajibu wa zakaatul fitri hauporomoki ikiwa imepita muda wake,kwani uwajibu huo upo kwenye dhima ya mwenye haqqi na chakula hiko,na mwenye haqqi ni maskini muhitaji,hivyo hilo ni deni,haliondoki mpaka lilipwe,kwani hiyo ni haqqi ya mja imekua,na kule kuchelewesha kunamuhusu allaah,muhimu ni mtu kujutuia na kuomba maghfira kwa kuchelewesha kwake huko.na allaah ndie mjuzi zaidi.
JE YAFAA KUTOA KIWANGO CHA PESA BADALI YA MCHELE?
asli ni kutoa kitu husika ambacho ni chakula kiliwacho na watu wa mji huo,tena kutoa kwa namna ambavyo tamko limekuja,haipindishwi kwa kutoa kiwango cha pesa ispokua kwa dharura au haja maaluma au maslahi mapana ya huyu muhitaji,ikiwa ni kwa hayo itajuzu,mfano mtu kapata mchele kilo tano na ni muhitaji mwenye familia kubwa,hana mafuta hana mkaa hana kitoeo n.k halafu mwengine anataka kutoa zakaatul fitri kwa maskini yule yule na anajua kua kapata mchele lkn hana vifaa vyengine basi hujuzu kwa hali hiyo kumpa pesa ili atengeneze chakula na wafurahi vizuri,kuliko kumlimbikizia michele na akakosa mkaa,mafuta na kitoeo mkampa mtihani wa kutengeneza bwimbwi tena.
JE MAKUNDI GANI YA KUPEWA HIYO ZAKKA?
wamekhtalifiana wanachuoni katika wakupewa na kuna qauli mbili:
[1]HUPEWA WATU WALE WA AINA NANE
na qawli hiyo ni mapito ya jumhuur kasoro imaam malik
[2]HUPEWA WENYE KUHITAJI [1]masikini[2]na mafuqara basi.
hayo ni mapito ya imaam malik na ameyachagua ibn taymiya .
WALLAAHU AALAM
kituo tuweke hapa
MTUMISHI WENU
ALFAQEER SAID SAALIM EL BAKRY

15/06/2017

بسم الله الرحمن الرحيم
{FIQHI YA FUNGA NO 14}
naam sifa njema anastahiqi allaah subhaanahuu wataala,rehma na amani zimfikie mtume wetu muhammad s.a.w,na jamaa zake na maswahaba zake,katika muendelezo wa darsa zetu kwa sasa tutaangalia jambo muhimu katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani fursa ambayo si ya kukosa:
فضل العشر الأوخر من رمضان
UBORA WA KUMI LA MWISHO LA RAMADHANI:
ramadhani ni msimu wa faida na ili ipatikane faida ni watu kufikia au kukaribia malengo ambayo allaah s.w asema:
"يا أيها الذين آمنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم لعلكم تتقون"
"enyi ambao mlioamini,mmefaradhishiwa nyie kufunga k**a walivyofaradhishiwa waliopita kabla yenu ili mpate kumcha allaah[kua wacha mungu}"
uchamungu haupatikani hivi hivi,yatakikana kufanya juhudi katika kuyaendea yaliyokua mema ya faradhi na sunna,hali ukijiepusha na maovu na yenye kuharibu mema yako,k**a alivyokua mtume s.a.w akifanya na alivyofundisha sie tufanye.
عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم أجود الناس وكان أجود ما يكون في رمضان حين يلقاه جبريل وكان يلقاه في كل ليلة من رمضان فيدارسه القرآن فلرسول الله صلى الله عليه وسلم أجود بالخير من الريح المرسلة"
"abdillaah ibn abbaas asimulia kua "alikua mtume s.a.w ni mkarimu wa watu[kawazidi watu sifa ya ukarimu]na alikua akizidisha ukarimu ndani ya mwezi wa ramadhaan ikawa jibriil akimshukia mtume s.a.w katika kila usiku wa ramadhani akimsomesha quraan,mtume s.a.w alikua mpenda kheri kuliko upepo wenye kuvuma"[bukhar na muslim}
hivyo tutumie ramadhani hasa 10 lilobakia kufanya ukarimu kati yetu na yapo mengi tu mambo ya ukarimu,k**a kulishana,kusaidia mayatima,kusaidia vituo vya quraan kwani ndani ya ramadhani panapatikana nyongeza kubwa mno.
عن عائشة رضي الله عنها قالت: "كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يجتهد في العشر الأواخر ما لا يجتهد في غيره"
MAMA AISHA R.A asema: "alikua mtume s.a.w akijitahidi kujipinda katika ibada katika kumi la mwisho,jitihada ambayo hakujitahidi katika makumi mengine"[muslim}
twataja haraka haraka mambo muhimu ya kujipinda nayo katika kumi hili la mwisho,ikiwa mtume ndio kiigizo chetu tena yeye hana dhambi tazama mama aisha anavyomsimulia:
كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا دخل العشر شد مئزره وأحيا ليله وأيقظ أهله"
"alikua mtume s.a.w linapoingia kumi la mwisho la ramadhani alikua akikaza kibwebwe chake[majaaz kua alikua akizidisha juhudi katika ibada]na alikua anauhuisha usiku wake kwa kukesha na alikua akiwaamsha watu wake"[bukhar}
labda twaweza kujiuliza kwa nini mtume s.a.w alikua akijitahidi na kujipinda katika masiku hayo?
لأن في هذه الأيام فضائل كثيرة لا تحصى فمنها:
HAKIKA KATIKA MASIKU HAYO KUNA FADHILA NYINGI MNO,MIONGONI MWA FADHILA HIZO NI:
(1)ليلة القدر التي هي موسم للتجارة الرابحة مع الله سبحانه وتعالى لأنه تعالى قد خصها بخصائص من بين الليالي ومن هذه الخصائص هي كالتالية:
(1)jambo la kwanza kubwa ni kua ndani ya 10 hili kuna usiku mtukufu[usiku wenye cheo] ambao ni msimu wa biashara yenye faida kati ya mja na mola wake,kwani hakika allaah amekhusisha kwa mambo maalum katika usiku huo wa masiku hayo,miongoni mwa hayo mambo maalum ni haya yafuatayo:
tuangalie maana ya neno hili LAYLATUL QADRI
فمن معنى ليلة القدر: التعظيم أي أنها ليلة ذات قدرٍ وأنَّ الذي يحييها يصير ذا قدر.
maana yake ya kwanza ni kuutukuza yaani usiku wenye utukufu[cheo] na hakika ya mtu ambae atahuisha usiku huo kwa ibada atafikia darja ya ya juu[cheo cha juu].
hivyo ni waajib kwetu kujipinda angalau tupate darja hizo.
ومنها: القدر بمعنى التضييق لإخفائها عن العلم بتعيينها أو أنّ الأرض تتضيق فيها من كثرة الملائكة.
maana ya pili qadri inamaanisha kubanwa,kwa kufichika kwake kielimu[yaani hakuna mwenye uhakika kua siku fulani ndio laylatul qadri] au pia ardhi hubanwa kwa wingi wa malaaika usiku huo.
ومنها: القدر بمعنى القدر بفتح الدال وذلك أنه يقدر فيها أحكام السنة كلهاز
na maana ya tatu neno qadr twapata ni kupangiliwa/kuqadiriwa mambo kwa kuieka fatha daal QADAR na imekua hivyo kwa sababu katika usiku huo hupangwa mambo ya mwaka mzima.
MIONGONI MWA MAMBO MAALUM KATIKA USIKU HUO:
[1]imeteremshwa quraan katika usiku huo [qadr aya ya 1]
[2]umepewa sifa maalum usiku huo kua ni bora kuliko miezi 1000,amesema hilo allaah ktk suuratul qadri aya ya 3
[3]umekhusishwa usiku huo kwa kushuka malaaika [suuratul qadr aya ya 4]
[4]umekhusishwa usiku huo kua na amani isiyo mfano yaani amani ambayo shetwani hawezi kufanya uovu wala maudhi suuratul qadr aya ya 5.
[5]umekhusishwa usiku huo kwa sifa maalum kua ni usiku wenye barka[suuratu ddukhaani aya ya 4]
[6]umekhusishwa usiku huo kwa hupitishwa bajeti ya mwaka mzima k**a rizki,maradhi n.k na allaah hubadili qadar [suuratu ddukhaan aya ya 4]
[7]umekhusishwa usiku huo kua ni usiku wa msamaha kwa mwenye kusimama kwa ajili ya allaah na akiwa na imaan na kutaraji malipo toka kwa allaah,mtume s.a.w asema: "من قام ليلة القدر إيمانا واحتسابا غفر له ما تقدم من ذنبه"
"yeyote mwenye kusimama[kufanya ibada]katika usiku wenye cheo akiwa na imani ya kweli na akataraji malipo toka kwa allaah husamehewa mtu huyo madhambi yake aloyatanguliza"[bukhar]
mambo saba hayo ndio tumewafiqishwa kuyaandaa,tumalizie kipengele hiki kwa kuangalia twapaswa kufanya nini katika masiku haya?
INATAKIWA KWETU KUFANYA MAMBO MATATU,KUACHA MAASWI MAKUBWA NA MADOGO,NA KUTIMIZA FARDHWI ZOTE,NA KUJIBIDIISHA KATIKA SUNNA MIONGONI MWAZO:
[1]KUSIMAMA KUFANYA IBADA K**A ILIVYOTANGULIA HADITHI TUMEONA FADHILA ZAKE
[2]KUFANYA ITIKAFU[kujifunga na msikiti]MTUME S.A.W ASEMA: "تحروا ليلة القدر في العشر الأواخر من رمضان"
"UTAFUTENI USIKU WENYE CHEO KATIKA KUMI LA MWISHO LA RAMADHANI"[bukhar] hapa twaona mtume s.a.w alikua akikesha kumi lote k**a alivyosimulia mama aisha r.a
[3]JAMBO LA TATU NI MTU KUSEMA "ALLAAHUMMA INNAKA AFUWWUN TUHIBBUL AFWA FA AF ANNIIY" mama aisha alimuuliza mtume s.a.w ewe mjumbe wa allaah unaonaje nikifahamu kua usiku fulani ni usiku huo wenye cheo niseme nini katika usiku huo"? mtume s.a.w akamwambia:
"قولي: اللهمّ إنك عفو تحب العفو فاعف عني"
sema; ''ewe allaah hakika wewe ni msamehevu unapenda kusamehe nakuomba niswaameh mimi"[tirmidhiyy 3513,annasaai 10708,ibn maajah 3850,ahmad 25490,haakim 530]
hivyo uradi huo popote pale uwe mdomoni mwetu si mchana si usiku,na haswa usiku tukithirishe,na hata wanawake walio katika ada zao za mwezi au nifaas nao watashiriki kwa kusoma uradi huo.wallaahu aalam
mtumishi wenu
alfaqeer said saalim el bakry

15/06/2017

بسم الله الرحمن الرحيم
{FIQHI YA FUNGA NO 13}
naam bado tupo katika kuelezea mambo yanayoharibu funga,baada ya kutazama kigawanyo cha kwanza cha mambo yenye kuharibu funga na kuwajibika kulipia siku hiyo,sasa tuangalie kigawanyo cha pili ambacho ni:
ما يبطل الصيام ويجب القضاء والكفارة: {وهو الجماع لا غيره}
MAMBO YANAYOHARIBU FUNGA NA NI WAAJIB KULIPA NA KAFARA,[nalo ni jimai pekee]
k**a tulivyoashiria mwanzo kwa aya kua mwanzoni mwa kufaradhishwa ibada ya funga ilikua hairuhusuwi baada ya ftari mtu kukutana na mkewe,ila ikaja aya na kuondoa kifungu kile na allaah akaruhusu usiku watu kukutana na wake/waume zao,hivyo kwa mchana wa ramadhani haifai kukutana na mke/mume na ikimpitikia mtu akakutana na ahli yake ni waajib kufanya kafara ya kuacha huru mtumwa,au kufunga siku 60 mfululizo,akishindwa alishe maskini 60,tuangalie tukio lilotokana na swahaba abuu hurayrah r.a asema:
"tulikua sisi tumekaa na mtume s.a.w punde akatujia mtu akasema mtu huyo: "ewe mjumbe wa allaah nimeangamia mie" mtume s.a.w akamuuliza: "UNA NINI WEWE/KIMEKUANGAMIZA KIPI?" akajibu yule bwana: "NIMEMUINGILIA MKE WANGU MCHANA WA RAMADHANI HALI YA KUA MIMI NIMEFUNGA" mtume s.a.w akamuuliza: "UNAWEZA KUACHA HURU MTUMWA"? yule bwana akajibu: "HAPANA" mtume s.a.w akamuuliza: "UNAWEZA KUFUNGA MIEZI MIWILI MFULULIZO"? yule bwana akajibu: "HAPANA" mtume s.a.w akamuuliza: "JE UNAWEZA KULISHA MASKINI 60"? yule bwana akajibu: "HAPANA" mtume s.a.w akanyamaza muda ule ule na sie tumekaa mara akaletewa mtume s.a.w chombo chenye tende,akauliza mtume s.a.w "YUKO WAPI YULE MUULIZAJI"? yule bwana akajibu: "MIMI HAPA" mtume s.a.w akampa tende kisha akamwambia: "CHUKUA TENDE HIZI UTOE SWADAQA" yule bwana akamwambia mtume s.a.w "HIVI YUPO MTU MASKINI KULIKO MIMI EWE MJUMBE WA ALLAAH?NAAPA KWA ALLAAH BAINA YA NCHA MBILI ZA MADINA HAKUNA NYUMBA YA FAMILIA MASKINI KULIKO YANGU" mtume s.a.w akacheka sana mpaka meno yake yakaonekana kisha akamwambia: "KATOE SWADAQA KWA FAMILIA YAKO,WAPE WAO" [bukhar1936,muslim 1111]
katika hadithi twapata mafunzo mengi mno kubwa ni mfumo wa kafara ya mtu alokumbwa na janga la kumuingilia mkewe mchana wa ramadhani,pia funzo jengine la kuvutia ni utoaji wa swadaqa kwa familia,zama zetu swadaqa imekua kwa baadhi ya watu kutoa kwa fakhari,mtu familia yake hali duni lkn nje asifika kwa ukarimu,mtu wazazi wake hawakumbuki kwa kutengeneza mambo yao[mahitaji]tena pengine wana hali ngumu kweli lakini nje kwa watu kando huyu bwana asifiwa kwa ukarimu,laa swadaqa ianzie kwako ikiwa wahitaji wapo,
jumhuur ya wanachuoni ikapita kua hakika kuingilia kwa mfungaji katika mchana wa ramadhani kwa makusudi na kwa kuamua kwa kukutana tupu mbili kisha kikazama kichwa katika moja ya njia mbili[njia ya halali tupu ya mbele,au njia ya haramu tupu ya nyuma]mtu huyu hua ameharibu funga,na ni waajib juu yake kulipa na kufanya kafara iwe ametoa manii au hakutoa manii.
asema abuu maalik msimamo wa jumhuur katika kuwajibisha kulipa kwa huyu mwenye kuingilia mchana wa ramadhani kuna ziyada ilopokelewa katika baadhi ya hadithi kwa njia tofauti tofauti,nayo ni kua mtume s.a.w amesema mwisho wake:
"NA AFUNGE SIKU KULIPIA SIKU ILE" [daara qutwniyy 190] na wasema wanachuoni kua nyongeza hiyo ni dhaifu haikuthibiti,hivyo akapita ibn hazim kua ni waajib juu ya mtu huyo kafara tu.
tukiangalia upande wa mke nae je:
هل تجب الكفارة على المرأة كالرجل؟
JE NA MWANAMKE NAE ANAWAJIBIKA KAFARA K**A MWANAUME?
naam ukiangalia hadithi iliyotangulia utaona kua mtume s.a.w amemuamuru mwanaume kufanya kafarana akanyamaza kwa mwanamke ambae aloingiliwa,je anawajibika nae kufanya kafara au yeye hawajibiki?
jambo hili lina qwali kadhaa,,,QAWLI YA KWANZA:
ليس على المرأة كفارة مطلقا:
MWANAMKE HANA KAFARA YA MOJA KWA MOJA;
nayo ni mapito ya imaam shafi na qawli ya imaam ahmad,kua inawatosheleza wao kafara moja nayo ni kwa mwanaume kinyume na mwanamke kwa fahmu ifuatayo:
[1]hakika mtume hakuamuru kafara kwa mwanamke pamoja na kua ndie aloingiliwa,na kitendo kimetokea kwa mume na mke pamoja,wakatoa dalili kua ingekua mtume s.a.w kaona kuna uwajibu wa kafara kwa mwanamke angemlazimisha wala asingenyamazia jambo hilo.
[2]hakika haqqi ya kafara ni mali na mali amekhusishwa nayo mume k**a ilivyo katika mahri.
tukitazama QAWLI YA PILI NI KUA:
أنّ على المرأة كفارة كالرجل:
MWANAMKE NAE ANAWAJIBIKA KWA KAFARA K**A MWANAUME:
na hii ni qawli ya jumhuur,abuu hanifa,maalik,na qawli ya imaam shaafi,na qawli ya imaam ahmad katika qawli yake swahihi zaidi katika riwaya zake mbili,kwa ikhtilaaf na upambanuzi wao kuhusiana na mwanamke huru na mtumwa,na mwenye kukubali kufanyiwa kitendo na mwenye kuchukia[alojizuia ila akaingiliwa kwa kubakwa] wakasema:
[1]hakika mwanamke huyu amevunja funga yake ya ramadhani kwa kuingiliwa huko,na ni waajib juu yake kafara k**a mwanaume,na sheria imekua sawa kwa watu katika mambo ya kihukmu ispokua katika sehemu ambazo imekuja dalili ya khaasw,kukhusisha baadhi na kuwaacha baadhi,ikawa imelazimika kwak kuilipia siku hiyo kwa kule kuharibika funga hiyo,basi anawajibika na kafara k**a ilivyo kwa mwanaume.
[2]ama suala la mtume kutomuamuru mwanamke kufunga katika simulizi hii hii simulizi haikuenea mpaka kwa mwanamke,ukiangalia imesimuliwa upande mmoja ambao ni wa mume tu,na mume alivyosimulia kasema "nimeangamia" wala hakusema "tumeangamia"[kumjumiasha na mkewe] hivyo yawezekana ikawa mkewe hakua mwenye kufunga siku hiyo,kwa udhuru wa maradhi au safari,au mke alikua mwenye kuchukia ila mume akatumia mabavu,au yawezekana mke alijisahau k**a kafunga,n.k
[3]jambo la tatu ni kua mke hakwenda kumuuliza mtume s.a.w aloenda ni mumehivyo alojibiwa ni muulizaji ambae ni mume
[4]na imechukuliwa pia sababu ya mtume s.a.w kunyamaza ni hekma baada ya kuona maneno ya huyu mume kila aulizwalo hawezi ikiwa mume hawezi je kwa mke itawezekana vipi?
ama tukiangalia jambo hili QAWLI YA TATU:
أن يجزيهما كفارة واحدة إلا إن كانت الكفارة بالصيام فعليهما:
INAWATOSHELEZA WAO KAFARA MOJA[kuacha huru mtumwa,au kulishiza maskini 60}ISPOKUA IKIWA KAFARA YA KUFUNGA BASI WATAWAJIBIKA KILA MMOJA AFUNGE:
na haya ni mapito ya al awzaaiiy.
na qawli yenye nguvu kwa hili ni qawli ya jumhuur ambayo ni no 2,na qawli ya imaam shafi haiko mbali na hiyo.
ANGALIZO:
ikiwa mwanamke hakupenda jambo hilo,bali akabakwa,au akashiriki hali amejisahau k**a kafunga,hawajibiki kutoa kafara,pia ni hivyo hivyo kwa mwanaume akijisahau wala hana hukmu hiyo au nae akibakwa wala hawajibikiwi na kafara,na haya ni mapito ya abuu hanifa,shaafi,na ahmad [[al mughniy 3/27]
هل تجب الكفارة على الترتيب؟
JE NI WAAJIB KAFARA KWA MPANGILIO?
wamepita jumhuur ya ulamaa kua uwajibu wa mpangilio katika kafara wala hauhami kutoka katika kufunga miezi miwili mfululizo ila itapotokea mtu huyu ameshindwa kutoa huru mtumwa,na wala mtu halishi maskini 60 mpaka aada ya kua ameshindwa kufunga miezi miwili mfululizo,kwa uwazi wa hadithi iliyotangulia..
ama imaam maliki yeye asema mtu huyo ana khiyari kwa hadithi itokanayo na abuu hurayrah r. "أن رجلا أفطر في رمضان فأمره النبي صلى الله عليه وسلم أن يكفر بعتق رقبة،أو صيام شهرين متتابعين،أو إطعام ستين مسكينا"
"hakika mtu mmoja aliharibu funga yake ktk ramadhani[kwa jimai]mtume akamuamuru afanye kafara ya kuacha huru mtumwa au kufunga miezi miwli mfululizo,au kulisha maskini 60 [muslim 1111]
wakasema wanachuoni kua hadithi ilopokelewa na imaam bukhari hailazimishi mpangilio hakika katika suali hili mtu atafanyia kazi kwa kuchagua,imechukuliwa kua kuongoza kwake ktk kuacha huru mtumwa inakua ni karibu zaidi kuipitisha kafara,na wakachukua baadhi ya wanachuoni.
ama jumhuur ya wanachuoni wakapita mpito wenye nguvu kua hadithi iloweka mpangilio na ilokuja kwa khiyari hadithi iloweka mpangilio ndio ina nguvu zaidi,kwani walopokea hadithi hiyo ni wengi,pamoja na mmoja mmoja katika mapokezi,na hadithi ya khiyari inageuka geuka katika matamko,na qawli ya mpangilio ina nguvu zaidi na ndio ilochukuliwa[na mpangilio ni huu:]
KUACHA HURU MTUMWA
KUFUNGA SIKU 60 [miezi miwili]MFULULIZO
[3]KULISHA MASKINI 60.
tumalize kipengele hiki kwa kufafanua jambo hili:
هل تتكرر الكفارة بتكرر الجماع؟
JE ITARUDIWA KAFARA KWA KURUDIWA JIMAI[yaani kafara itakua zaidi ya moja ikiwa jimai imekua zaidi ya moja]?
[1]MWENYE KUINGILIA MCHANA WA RAMADHANI KISHA AKATOA KAFARA,KISHA SIKU INAYOFUATA AKAINGILIA TENA NI WAAJIB JUU YAKE KAFARA NYENGINE.
[2]MWENYE KUINGILIA KATIKA MCHANA MMOJA WA RAMADHANI ZAIDI YA MARA MOJA HUKMU YAKE NI KAFARA MOJA.
[3]MWENYE KUINGILIA MCHANA WA RAMADHANI N IKAWA HAJATOA KAFARA KISHA AKAINGILIA TENA SIKU INAYOFUATA,,,,katika hili kuna qawli mbili:
[1]NI WAAJIB KWAKE KILA SIKU KUTOLEA KAFARA KWANI KILA SIKU ALOINGILIA NI IBADA YA PEKE YAKE,[na ni qawli ya imaam shafi a malik na jamaa]
[2]WAAJIB KWAKE KAFARA MOJA MAADAM HAKUA AMEITEKELEZA KAFARA HIYO YA MWANZO,NAYO NI QAWLI YA ABUU HANIFA NA AWZAAIIY NA ZUHRIYY,wao wamefanya qiyaas ktk haddi ya zinaa,mzinifu alozini mara moja sawa na mzinifu alozini mara 20 na wakipatwa wana hukmu moja,sio kumuhesabia huyu wa 20 na masiku ambayo hakukutwa kua ndio apigwe bakora 2000 hapana atapigwa 100 tu,NA UKIANGALIA QAWLI MBILI HIZI UTAPATA QAWLI YA KWANZA INA NGUVU ZAIDI,KWANI KILA SIKU NA IBADA YAKE YA FUNGA HAIWEZEKANI HARIBIKO LA FUNGA YA LEO LIKAHARIBU YA KESHO,HIVYO HUYU MTU KAHARIBU LEO,NA KAHARIBU KESHO HIVYO ZOTE MBILI ATAWAJIBIKA.
mtumishi wenu
alfaqeer said saalim el bakry

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Tandale Kwa Tumbo
Dar Es Salaam