23/12/2018
SILAHA YA 03.. 2018/2019.
ndani ya mwaka 20172018 katika harakati zangu za kupata maarifa niliweza kufanikiwa kukutana na kazi za waandishi wengi tu ndani na nje ya Tanzania.
mfano:makirita amani, joel nanauka, erick shigongo, tonny robins, brian tracy, robert kiyosaki, Shaban robert, napolean hill, na wengine ambao sijawaorodhesha.
Ndani ya vitabu vya hawa waandishi kulikuwa na mada mbalimbali walizofundisha lakini cha ajabu waandishi karibia wote kwenye uandishi wao kuhusu mafanikio walisisitiza sana kuhusu kujiwekea malengo.
mwishoni mwa mwaka 2017 k**a ilivyo sasa hivi mwezi wa 12 nilikutana na work book ambayo imeandaliwa na mwandishi joel nanauka ambayo inaweza kukusaidia kupanga malengo yako vizuri na pia inasaidia kufanya tafakari vizuri kila wiki juu ya malengo yako.
Kikweli hii work book ilinisaidia sana, unajua kiukweli kitendo cha kujiwekea malengo na kuyaishi malengo yako inahitaji msaada wa hali ya juu na msaada wenyewe nakuomba utafute hii work book utaona matokeo yake.
naamini isingelikuwa kuwa na hii work book labda hata lengo langu la kuwa mwandishi lingekuwa lishafifia kwa hali ya juu sana lakini kutokana na hii work book imenisaidia kwa kiasi chake.
Gharama ya hii work book ni shilingi 10000 lakini msaada unaotokana na hii work book ni zaidi ya 10000 unayotoa.
na hii ndio ilikuwa silaha yangu mwaka uliopita na naenda kuitumia mwaka huu nakusihi na wewe ndugu yangu utumie.