28/10/2024
UBATIZO MMOJA NI UPI?
Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,
Waefeso 4:5
Kanisa lilipozaliwa lilihitaji sana kuelewa fundisho la Kristo , hivyo iliwachukua miaka kadhaa kuyaacha mapokeo ya mababa na vivuli vilivyotumiwa na manabii kumwelezea Kristo atakaye kuja.
Soma zaidi👇👇
Yohana Mbatizaji alikuja akibatiza kwa maji... na UJUMBE WAKE ulikuwa huu
📖Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini nyuma yangu anakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuvichukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Mathayo 3:11
au
📖Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”
Marko 1:7-8
au
📖Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. ”
Luka 3:16
UKIELEWA HAPO JUU katika hivyo vifungu vya waandishi watatu utaona Yohana aliweka wazi kabisa ... kwamba YEYE NDIYE ANABATIZA KWA MAJI kwa ajili ya kumtambulisha atakaye kuja baada yake. Jana niliuliza swali ... kwa nini Yesu anasema Yohana Mbatizaji ndiye mkuu kuliko watu wote waliozaliwa na Mwanamke?
Jibu lake ni hili hapa:👇
Manabii wote waliotangulia kabla yake walitabiri wakisema ... "Bwana Mungu asema" au " Hivi ndivyo asemavyo Bwana..." .... Lakini kwa Yohana Mbatizaji ilikuwa tofauti , Yeye huduma yake ilikuwa ... " Huyu ndiye ...." Hivyo Ukuu katika Ufalme unaelezewa kulingana na kiwango cha UFUNUO wa kumjua Kristo na siyo kiwango cha kufanya miujiza.
Niendelee na somo la Ubatizo....
Tumeona Jinsi Yohana Mbatizaji alivyotangaza... kwamba ajaye baada yake ATABATIZA KWA ROHO na siyo kwa maji.
Lakini baada ya Kristo kuondoka ( kuondoka kwake ndiyo ilikuwa kuingia ndani yao)... Kanisa la mitume liliendeleza ubatizo wa Yohana wa kuwazamisha watu kwa maji... kwa nini ? kwa sababu wao nao walikuwa hawajajua kwa usahihi Fundisho la Kristo .
UJIO WA MTUME PAULO ULILETA UKAMILISHO WA FUNDISHO LA KRISTO.
Mafundisho ya Mtume Paulo ni Ufunuo wa Kristo ambao si wa ushuhuda wa macho ( eye witness account / sense knowledge ) na hii ni kwa sababu hakufundishwa na Mitume walioishi na Kristo wakati wa huduma yake. K**a alivyoandika hapa👇
📖Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu. Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.
Wagalatia 1:11-12
📖Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake, alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote, wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.
Wagalatia 1:15-17
KATIKA HUDUMA YAKE YA INJILI MTUME PAULO AKAFIKA EFESO...
Huko Efeso akawakuta wanafunzi waliokuwa wamebatizwa UBATIZO WA YOHANA yaani wa kuzamishwa katika maji...
📖Apolo alipokuwa huko Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso. Huko akawakuta wanafunzi kadhaa, akawauliza, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?”
Wakajibu, “Hapana, hata hatukusikia kuwa kuna Roho Mtakatifu.” Ndipo Paulo akawauliza, “Je, mlibatizwa kwa ubatizo gani?” Wakajibu, “Kwa ubatizo wa Yohana.”
Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohana ulikuwa wa toba, aliwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja baada yake, yaani, Yesu.” Waliposikia haya, wakabatizwa katika jina la Bwana Yesu. Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akawashukia, nao wakanena kwa lugha mpya na kutabiri. Walikuwa k**a wanaume kumi na wawili.
Matendo 19:1-7
Sasa hapa ndipo Madhehebu yalipochanganywa yakachanganyikiwa.
FUNDISHO POTOFU LINATIKANA NA SABABU MOJAWAPO AU ZOTE KATI YA HIZI ZIFUATAZO;
1. kupindisha Kweli
2. kuongezea kitu katika ile Kweli
3. kuondoa kitu katika ile Kweli
NB: neno "Kweli" hapo linamaanisha "Mtu ambaye ni Kristo" na hapa ninazungumzia fundisho la Kristo ( Mtu ).
Sasa Madhehebu mengi yameacha ubatizo wa Roho ambao ndiyo Paulo aliwasahihisha wale watu wa Efeso ... na ambao pia tumeona Yohana Mbatizaji alisema yeye ajaye baada yake ATABATIZA KWA ROHO....
soma hii itakisaidia
📖Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”
Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni k**a hua, akakaa juu yake. Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, *huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’* Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.
Yohana 1:31-34.
YESU NAYE AMEFUNDISHA KUHUSU UBATIZO:
📖Wakati mmoja alipokuwa pamoja nao, aliwapa amri hii, “Msitoke Yerusalemu, bali ingojeni ahadi ya Baba, ambayo mmenisikia nikisema habari zake. Yohana aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
Matendo 1:4-5
Ubatizo mmoja ambao Mtume Paulo anafundisha ni ule wa Roho yaani Mungu kukaa ndani ya mwamini na siyo mwamini kizamishwa ndani ya maji.
Kanisa kuacha fundisho la Ubatizo wa Roho ambao abatizaye ni Kristo na wahudumu wa Injili kujivuka UYOHANA MBATIZAJI kumepoteza nguvu halisia za Madhihirisho ya Roho wa Mungu kwa makusanyiko.
Imeandaliwa na ...
Bible comentary ( Sir Redfonce Mboma ).
October 26,2024 19:30-20:30.