24/07/2021
chande
Ijumaa, 15 Mei 2015
KAMUSI YA LUGHA; MAANA, AINA, TAARIFA NA DHIMA ZAKE.
KAMUSI YA LUGHA; MAANA, AINA, TAARIFA NA DHIMA ZAKE.
MAANA YA KAMUSI
Massamba (2012:24) kamusi ni kitabu cha orodha ya maneno katika lugha, yaliyopangwa kwa utaratibu maalum, pamoja na maana au fasili zake; katika uchanganuzi wa lugha haya ni maneno ya kileksika, yaani yasiyokuwa ya kisarufi au kifonolija.
Tuki (1990:21) kamusi ni kitabu cha orodha ya maneno yaliyopangwa kwa utaratibu maalum, pamoja na maana na fasili zake.
Wamitila (2003:76) kamusi ni kitabu ambacho kina orodha ya maneno katika lugha Fulani ana ambayo hupangwa ki-abjadi au kialfabeti. Maneno haya huelezewa maana zake mbalimbali na labda hata vyanzo vyake.
Matinde (2012:273) kamusi ni kitabu chenye mkusanyiko wa maneno sanifu katika lugha mahususi yaliyoorodheshwa kialfabeti na kutoa taarifa za kifonetiki, kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia, na hata kisemantiki.
Nyambari na Masebo (2012:179) kamusi ni kitabu cha marejeleo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani, na kupangwa kwa utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo msomsji huweza kuelewa.
Kwa ujumla kamusi ni kitabu chenye orodha ya maneno mbalimbali yaliyopangwa vizuri kwa kufuata alfabeti na hutoa taarifa mbalimbali k**a vile maana, matamshi n.k.
MUUNDO WA KAMUSI
i) Utangulizi wa Kamusi
Hii ni sehemu ya mwanzo ambayo hutangulia matini yenyewe ya kamusi.
ii) Matini ya Kamusi
Hii ni sehemu ambayo inaonyesha vidahizo na fahiwa zake kuanzia herufi A-Z.
iii) Sherehe ya Kamusi
hizi ni baadhi ya taarifa ambazo huwa zimeandikwa mwishoni mwa kamusi. Kwa mfano majina ya nchi, lugha za mataifa duniani, vipimo vya urefu, vipimo vya uzito, ujazo n.k.
AINA ZA KAMUSI
Kwa kutumia kigezo cha LUGHA kuna aina kuu tatu (3) za kamusi
i) kamusi wahidiya
hii ni kamusi inayoandikwa kwa lugha moja
ii) kamusi thaniya
Hii ni kamusi inayoandikwa kwa lugha mbili.
iii) kamusi mahuluti
Hii ni kamusi inayoandikwa kw