Naanza na wewe

Naanza na wewe Revolutionary stories. Change in all that turns us down. Mimi naanza na wewe.

Mathayo 24:4-14[4]Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. [5]Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, w...
16/06/2022

Mathayo 24:4-14
[4]Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye.

[5]Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi.

[6]Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.

[7]Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.

[8]Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.

[9]Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu.

[10]Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.

[11]Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi.

[12]Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.

[13]Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.

[14]Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.

29/04/2022
Ukute jirani ndo kimada wa shangazi ndo maana heri imetukimbia. Au hujui pesa imekuwa tamu kuliko sukari?? Tuombe Mungu ...
12/11/2021

Ukute jirani ndo kimada wa shangazi ndo maana heri imetukimbia. Au hujui pesa imekuwa tamu kuliko sukari??

Tuombe Mungu atupe pumzi. Naamini mmeshajua team yetu inamilikiwa na familia kwa sasa.

Another step forward
22/01/2021

Another step forward

 Naomba ukanisaidie kuwaambia kwamba  tofauti ya Fisi yule wa enzi za babu zao na huyu wa sasa ni kwamba Yule alikuwa an...
21/06/2019



Naomba ukanisaidie kuwaambia kwamba tofauti ya Fisi yule wa enzi za babu zao na huyu wa sasa ni kwamba

Yule alikuwa anakula mifugo yao, akawala babu na bibi zao bila huruma. Na kwasababu walimpinga basi naye ndo akazidisha njaa juu yao.

Lakin huyu wa sasa hivi kwa kuwa wanamfuga wenyewe anazidi kunona na amekuwa hali watoto wao mara kwa mara kwani wanajitahidi kumpa mifugo yao aile wao wakizidi kubaki masikini

 Huna wa kumlaumu wala cha kusingizia. Kwani tangu mwanzo wa safari uliambiwa kila kitu kuhusu safari yako na ukakubali....
11/06/2019



Huna wa kumlaumu wala cha kusingizia. Kwani tangu mwanzo wa safari uliambiwa kila kitu kuhusu safari yako na ukakubali.

Makosa yalifanyika pindi ulipoingia kwenye mji ule na kutamanishwa na anasa zake hata baada ya siku nyingi hukumbuki tena kwamba kuja huko uliagizwa. Na kwamba baada ya muda wako wa kazi kuisha utarudi na kuulizwa mrejesho wa yale uliyotumwa.

Nakusihi ujitahidi kukumbuka nini ilikuwa sababu yako kuja duniani kwa njia ya kuzaliwa. Haukuzaliwa ili uishi tu. Kuna kazi maalumu Mungu alikutuma kuifanya.



Address

Mikocheni
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 10:00 - 18:00
Tuesday 10:00 - 18:00
Wednesday 10:00 - 18:00
Thursday 10:00 - 18:00
Friday 06:00 - 23:59
Saturday 08:00 - 23:59
Sunday 08:00 - 23:59

Telephone

+255782732228

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Naanza na wewe posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category