03/02/2016
NGUVU YA INJILI PART 1
Injili kwa tafsiri ya Biblia ni uweza wa Mungu uuletao wokovu kwa kila aaminiye Warumi.1:16.injili imejengwa katika kuzaliwa,kuishi,kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
Injili ni nguvu inayotukomboa kutoka katika:
1.hatia na adhabu ya dhambi (kuhesabiwa haki)
2.nguvu na utumwa wa dhambi(kutakaswa)
3.Asili ya dhambi(kutukuzwa).
Kabla ya kuelezea mambo hayo matatu,ni vizuri kuelewa tatizo la dhambi.Injili ni utatuzi wa tatizo la dhambi,mtu hawezi kufurahia utatuzi k**a hajaelewa tatizo lenyewe hasa.
Dhambi
1.Dhambi ilianza katika akili ya lusifa(shetani)Ezekiel 28:14-15
2.dhambi iliingia duniani baada ya Adam na Eva kudanganywa mwanzo 3:1-24,na kufanya shetani kuwa mungu wa dunia hii.luke 4:5-6,2kor4:4.
3.wanadamu wote waliozaliwa na adamu wamekuwa chini ya utumwa wa dhambi. 2Pet 2:9,yoh8:34,warumi 5:12,19.
4.hivyo binadamu si mdhambi kwa matendo,maneno au mawazo yake tu ba li kwa asili yake pia.zab51:5,58:3,warumi 7:14-17.
5.bila msaada wa Mungu mwanadamu hawezi tii maagizo.mema ya Mungu.warumi 8:7.
6.Mungu ni upendo,kinyume cha tabia yake ndio dhambi yenyewe yaani ubinafsi.
itaendelea sehemu ya 2