11/07/2026
WE ARE PROUD OF YOU Kaniki Brown
Kazi zako na jitihada zako zinazungumza zenyewe.
Repost
Mtangazaji wa redio na mwanahabari Awadh Omary Kaniki amesema kuwa kupata tuzo katika umri wake ni jambo lenye thamani kubwa, akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na kujituma, kujifunza kila siku na kujenga uaminifu katika kazi ya uandishi wa habari.
Kaniki amesema tuzo hiyo ni ishara kwamba juhudi zake zimetambuliwa, huku akiwashukuru wadau, wasikilizaji, watazamaji na wote waliomuunga mkono katika safari yake ya taaluma.
Amesema tuzo hiyo inampa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na kuwahudumia wananchi kupitia habari zenye ukweli na manufaa kwa jamii.
Aidha, amewahimiza vijana wanaotamani kuingia kwenye tasnia ya habari kutokata tamaa, wakiamini kwamba mafanikio yanapatikana kwa nidhamu, uvumilivu na kufanya kazi kwa bidii.
Credit MSN Tanzania
Watafute Leca building and furniture.........................................................
Ripota wa Habari za Mikoani ✍ Kaniki Brown
“Endelea kufuatilia kwa taarifa sahihi na za uhakika.
KWA MATANGAZO YA BIASHARA NA HABARI Follow kwa updates zaidi. Kuwasiliana 📞 0622 732 287
”