02/01/2017
Kheri na fanaka ya mwaka mpya 2017. Bwana mwema aishie milele zote azidi kuwaangazia nuru ya uzima na mafanikio kila uchwao.
Leo, tuangalie mambo machache ya muhimu katika kumchagua mwenzi wa maisha(mchumba).
Ndoa ni taasisi takatifu iliyoanzishwa na mwenyezi Mungu kwa kuwaunganisha mume na mke kuwa mwili mmoja!! Unapo ianza safari ya kumpata mwenzi wako wa maisha tafakari mambo yafuatayo:
1. Dini/imani zinazofanana. Jambo hili ni la msingi sana ktk kujenga ndoa na familia yenye afya kiroho. Kutofautiana ktk imani au dhehebu huleta mtafaruku mkubwa hasa kwa watoto wanapokuwa wamezaliwa. Watoto wanaweza kushindwa kupata sehemu sahihi ya kuabudu endapo baba na mama watakuwa na sehemu tofauti kwa ajili ya ibada.
2. Kiwango cha elimu. Jiridhishe kwamba mtu unae hitaji kuishi nae hamzidiani sana kielimu. Hii ina faida kubwa sana ktk suala la kufanya maamzi ndani ya nyumba hasa ktk masuala ya kipato na maamzi mengine ktk familia. Lakini si lazima kwamba wana ndoa watarajiwa walingane ktk kiwango cha elimu, walengwa wanaweza kukubaliana kuisji pamoja huku wakiweka mipango thabiti ya kusaidiana ili kila mmoja afikie matakwa yake kielimu.
3. Umri. Hakikisha hamuachani mbali sana na mwenzi wako kiumri. Kumbuka, ndoa ni faraja. Mmoja wenu anapokuwa na umri mkubwa sana, wakati mwingine inaweza kuwa ngumu ktk kutimiza yale yanayopaswa kufanywa k**a wana ndoa. Mfano, kucheza pamoja, kusimulia habari za matukio fulani ktk maisha, kuongozana pamoja ktk matukio mbalimbali n.k. Si vema, wakati fulani ujisikie kwamba umeolewa na babu au umemuoa bibi. Unapaswa kumfurahia mke wa ujana wako.
4. Uwazi. Dunia sasa hivi imebadilika sana. Unapokuwa unamtafuta mwenzi wa maisha hebu jaribu kuwa muwazi kuhusu familia yako, hali yako ya maisha, kazi unayofanya, k**a una mtoto au watoto, magonjwa ya kurithi k**a yapo kwenye familia yenu n.k. Watu wengi wanadhani kwamba kumueleza mtu kuhusu kazi unayofanya kutampa shauku ya kutaka kufanya mahusiano kwa sababu ya kipato. Hivi, ni nani alie tayari ktk hali ya sasa hivi kumuoa au kuolewa na mtu ambae uwezo wake wa kujishughulisha ni mdogo? Au ni mvivu wa kufanya kazi? Kwahiyo ni vema, mkawekana wazi ili kila mmoja ajue na ajipange na namna ya kukabiliana na changamoto za familia mnapokuwa mmeamua kuwa pamoja.
5. Tabia. Peleleza vizuri ili kujua tabia za huyo unae mhitaji kuwa nae k**a mke na mme. Elimu ya mahusiano inasema kwamba gharama ya kujua tabia za mwenzi wako zisizo nzuri na kusaidiana kuzirekebisha kabla ya ndoa ni ndogo kuliko gharama ya kuzirekebisha mkiwa ndani ya ndoa. Tabia k**a ukahaba, kuvuta sigara, ulevi, uchoyo, umbea, uvivu, wizi na udokozi. Ujuapo tabia hizi kwa mwenzi wako k**a utakuwa umeamua kuwa nae kuunda familia basi msaidie kwa ushauri na kuomba pamoja ili aweze kubadilika.
6. Uandaaji wa chakula. Familia bora hustawi ktk misingi ya upendo, amani na lishe bora. Mwenzi wako hasa wa k**e ni muhimu kujiridhisha kwamba ana uwezo wa kutengeneza chakula bora kwa ajili ya mmewe na wanafamilia wengine. K**a hawezi, unaweza kumtafutia mafunzo ktk sehemu husika kwa ajili ya kuboresha uandaaji wake. Jambo hili lifanyike kwa makubaliano maalumu hasa baada ya kuridiana kwamba mtakuwa wana ndoa hapo baadae
6. Usiharakishe kufanya nae mapenzi. Tendo la ndoa linaweza kufanyika endapo wawili nyie mmekubaliana kufanya hivyo kwa lengo la kujilinda na magonjwa hasa baada ys kufahamiana vizuri historia zenu za mahudisno ya nyuma. Tendo hili lifanyike kwa umakini sana maana linaweza kuvuruga uchumba na kuacha makovu ya maumivu baada ya mmoja wenu kugundua mapungufu ya mwenzake. K**a wenzi wanaweza kuvumilana hadi safari ya kufunga ndoa inapokuwa imefika basi, tendo la ndoa lisifanyike kabisa. Barikiwa sana unapotafakari kuingia ktk edeni mpya yenye amani, furaha, upendo na kujaliana!!