Seek Knowledge First-Skf

Seek Knowledge First-Skf

Share

providing information, education, skills and knowledge to the Young generation about social issues, self recognition, etc

13/11/2022

Wachungaji na viongozi, niwasihi sana kuwa boresheni mazingira ya ibada za ndani ili kuimarisha afya za washirika wenu. Makanisa mengi hasa ya kiroho yanazidi kupoteza mvuto kwa kizazi cha Digital hasa vijana kwa sababu kanisani mazingira hayaridhishi wala kuvutia......
Mtafuteni Mungu awape mafundisho sahihi yanayotoka kwake, Mwombeni Mungu awape chakula sahihi kwa ajili ya wahirika wenu, boresheni ibada zote, Boresheni eneo la sifa kwa maana ya mifumo ya muziki ili kuwafanya watu wawe na sababu yakuwa sehemu ya ibada makanisani....
Jiulizeni kwa nini Fiesta na matamasha mengine ya Secular yanajaza watu kwa maana ya idadi ya watu bila kujali mazingira ya mvua au usiku mnene, lakini asilimia kubwa ya Makanisa yamepoteza ibada za jioni, ibada za kusifu, vyombo vibovu,.......
Mungu huabudiwa kwa usafi na viwango pia, Roho Mtakatifu bila maarifa ni kumlazimisha mtu tajiri kuishi kwenye nyumba ya Tope....
Jiulizeni na kujitafakari Baba zangu, wachungaji na viongozi wa makanisa, hasa ambayo hayako kwenye mifumo ya Ministry....
Tuwekeze kuzifanya bora nyumba za kristo

07/10/2022

Fanyia kazi maono yako

07/09/2022

SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ULIMWENGU WA MASOKO NA MAHUSIANO KATIKA BIASHARA 1.
Miaka ya nyuma, Tanzania na ulimwengu mzima, uliwekeza sana nguvu kwenye vitengo vya umma, kwa maana ya ofsi za serikali na wakati mwingine taasisi binafsi ambazo hazikuwa na mlengo wa kibiashara. Vijana wengi walikwenda shule kwa lengo la kuajiriwa kwenye ofsi za serikali na taasisi mbalimbali ambazo zilikuwa zikijihusisha sana na masuala ya kusaidia jamii....

Lakini katika utandawazi na ukuaji wa teknolojia umekuja kubadilisha, mitazamo, mifumo ya maisha kwa namna ambayo dunia ilikuwa hajazoea hasa katika dunia ya tatu ambayo inabeba asilimia kubwa ya nchi masikini na duni kwa kiwango cha juu sana....

Mabadiliko ya sayansi na teknolojia yamekuja wakati ambao, hakuna maandalizi wala mapokeo ya mfumo mpya wa maisha ambayo ndiyo yameshika hatamu na kuiendesha dunia kwa namna nyingine kabisa....

Wakati mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi wenzake wanaipokea nchi hii kutoka kwa mwingereza mwaka 1961, asilimia kubwa ya watu katika Tanganyika walikuwa hawana elimu zaidi ya elimu ya ujuzi katika uchongaji vifaa mbalimbali kwa kutumia mikono yao na vifaa vichache ambavyo walivigundua. Hii ni kwa sababu katika kipindi cha ukoloni elimu ilitolewa kwa uchache saba hasa kwa watoto wa machifu na baadhi ya watu ambao walikuwa wakisaidia mawasiliano kati ya mkoloni na mtu mweusi......

Hivyo hata baada ya uhuru mfumo wa elimu, uliendelea kutolewa kwa mlengo wa kwenda kutumikia taasisi na serikali, watu walifundishwa elimu kwa lengo la kutumikia serikali na sivyo ilivyo leo ambapo duniani inamwitaji msomi kwenda kupngeza thamani kwenye kile ambacho tayari wengine wameshakifanya au kugundua kitu kipya tofauti na miaka hiyo ambayo mwajiriwa alikwenda kufanya kazi ambayo tayari inafahamika inapaswa kufanywa kwa namna gani ili kufikia malengo...

Miaka imesogea, ujamaa ambao mwalimu Nyerere aliuhubiri na kuusisitiza kwa nguvu nyingi kwa miaka mingi umekosa nguvu mbele ya mfumo wa kikeptalisti, ambao unarahisishwa sana na kuongezeka kwa matumizi ya sayansi na vifaa vya kisasa ambavyo vinaifanya dunia kukimbia kwa kasi na kila mtu akiwa na shauku ya kutaka kuwa juu ya mwingine ukilinganisha na mfumo wa ujamaa ambao ulimwezesha kila mtu kupata sawa na mwingine hata k**a hakustahili kupata jambo fulani.....

Ukuaji wa elimu nchini na ulimwengu mzima, unakuja na nguvu kubwa ya ufinyu wa ajira kwenye maofsi mengi, kuongezeka kwa matumizi ya mashine imekuwa miongoni mwa sababu kubwa ya wasomi wengi kukosa ajira kwenye mashirika ya serikali na mashirika binafsi, kwa sababu tu kazi za wengi zinamalizwa na matumizi ya mshine yenye uwezo wa kufanya majukumu ya watu wengi.
Wasomi kuongezeka, watu kuongezeka na mahitaji ya ajira kuwa juu yamepunguza sana ukamilifu wa mahitaji ya watu kwenye sokonla ajira, hivyo imepelekea watu wengi kubadili mwelekeo na mitazamo kwa moyo wa kupenda au wa kulazimishwa maana hakuna jinsi....

Mfumo wa kikeptalisti umejikita zaidi katika uzalishaji kwa maana ya biashara na uwekezaji kwenye viwanda vya manual na viwanda vya software na kila mtu anashauku ya kuwa juu kuliko mwingine. Sasa kutoka na mabadiliko hayo makubwa, watu wengi wamelazimika kuingia kwenye ujasirimali, biashara na kazi zingine nyingi nje ya ajira zinazoitwa rasmi, hii inakuja kwa watu wa k**a zote, wasomi, wasio wasomi, walioajiriwa na wasioajiriwa. Hii ni mifumo ambayo inamlazimisha kila mtu kuishi kwenye nini duniani inataka sio wewe unataka nini....

Kutoka na hali hii kushamiri kwa nguvu, baadhi ya watu imewalazisha kuanza ujasirimali, biashara bila kujua ni kwa namna gani biashara inaendeshwa, ufanye nini ili kwenye ile biashara yako iweze kustawi na kudumu kwa muda mrefu na kuleta manufaa kwenye maisha....
Biashara nyingi zinaanzishwa lakini mwisho wa siku zinakufa au kukosa ustawi ambao ulitegemewa. Zipo sababu nyingi sana ambazo zinapelekea hali hiyo kuwa kubwa kiasi cha kutishia maisha ya watu kuwa kwenye umasikini wa kuogelea..

Baadhi ya sababu hizo ni....
1. Sababu za kimasoko..
2. Mitaji..
3. Uwekezaji usiokuwa na ufahamu ndani yake
Na mambo mengine mengi. Sasa ndugu Musa Zephania Mgema, msomi wa chuo kikuu kwenye masuala Mahusiano ya Umma na Masoko amekuandalia darasa huru ambalo kwa hakika litakupa jicho la tatu kwenye eneo la masoko kabla na baada ya kuanzisha baishara yako, unapaswa kufanya nini na ili kuifanya biashara yako ikuwe na kuongezeka kwa kiwango kikubwa na kukupa matokeo unayoyataka....

Kupitia
Instagram ya ,
page ya Media
Kwenye blog ya mosesmgema.blogspot.com na baadae tutakuwa na magroup ya WhatsApp, na twitter, LinkedIn na YouTube account basi tutakuwa na darasa huru lenye manufaa makubwa kwako wewe mfanyabiashara na mjasirimali...
[email protected]
0755632375
0745311928
Karibu sana

12/06/2020
02/01/2019

Mwaka 2018 umepita, tuna sababu ya kumshukuru Mungu sana kwa mengi mazuri aliyotutendea, mengi magumu aliyotuvusha, haikuwa rahisi hata kidogo maana ndugu jamaa, marafiki, majirani wameshindwa kuambana nasi kwa kuunza mwaka huu.

Ni kwa neema wala sio kwa welevu, ujanja, ubora na utakatifu mwingi uliotufanya kuwa hai, is by Grace tu ndo maana tuko hapa.

2019 tumeianza kwa amani na furaha kubwa, wengi tukiwa na matumaini makubwa kwa kuset, mipango, malengo, shauku na hamasa ya kwamba mwaka huu basi ni mwaka ambao ni mwaka wa taofauti
Kiuhalisia imekaaje, kiuhalisia kabisa kugeuza mwaka ni k**a kulala na kuamka siku mpya, au kutoka mwezi mmoja kwenda mwezi mwingine in short ni mwendelezo wa maisha yaleyale tu.

Kwa kweli ndugu zangu tufanye kazi zaidi kuliko kuongea, mipango bila utekelezaji wa majukumu au wa mipango hiyo ni sifuri.
Kuanza mwaka sio kigezo cha wewe kubadilika kitabia na kimtazamo bali, maamzi ya dhati ya kuacha tabia za mazoea ndiyo kitu kinaweza kukufanya kufikia malengo ya kile ulichokifanya.

Kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kuongea bila kutekeleza unachozungumza ni kazi bure. Lazimamabadiliko yaanzie kwenye fikra na maamzi ya dhati toka moyoni hapo ndipo unaweza kuona kweli mwaka umebadilika na uko tofauti na mwaka uliopita.
Katika kila jambo unalofanya mshirikishe Mungu, maana Mungu ndo mwamzi na maratibu wa kila jambo tunalofanya, ni signatory wa kila jambo kwenye maisha yetu hakuna sababu ya kuishi bila kumtegemea Mungu.

Kufanya mambo ambayo yanamsikitisha mzazi wako basi jua Mungu anasikitika zaidi na hapo unajichumia laana utakuwa ukifanya mambo lakini hufanikiwi kumbe umeishi maisha yenye kumchukiza muumba wako.
God ni kila kitu fanya kila jambo kwa kumshirikisha Mungu, toa sadaka, fanya ibada, achana na waganga, na kuwategemea viumbe ambao pia kesho na kesho kutwa watakufa, na Biblia inasema amtegemeae mwanadam amelaaniwa achana na kuwategemea kiumbe k**a wewe.

Jifunze mara kwa mara ili kuujengea ubongo wako maarifa mengi kwa ajili ya matumizi yako binafsi na jamii.

Epuka mogogoro isiyo ya Lazima, hata k**a ni ya lazima basi jitahidi kuepukananayo kwa kila hali.

Samehe kwa kadili uwezavyo, ni afya ya akili nafsi na moyo, ukiombwa msamaha samehe, ukijua kuwa kila mtu anakosea, waweza kukosewa k**a binadamu samehe maana hujui kesho yako wewe

Usiwe mtu wa kubeba mambo yasiyokuwa na faidia hata kidogo, kumbuka jambo likitokea limetokea huwezi kulifuta zaidi ya kusamehe tu.

Ushirika na wenzako liwe ni jambo la lazima kwa mwaka huu, baraka zingine za mafaniko zimefungwa kwenye ushirikiano na watu, kupitia ushirika mzuri na watu hapo ndipo unajenga connection na channels zingine ambazo huwezi zipata ukiwa pekee yako k**a mkiwa jangwani.

Hekima, Busara ni jambo jema kwa mwelekeo mzuri wa maisha yetu.

Nikutakie baraka za Bwana kwa mwaka huu, ukawe mwaka wa ushindi na utajiri kwa kila nyanja ya Maisha yako.

Kumbuka mkono mlegevu huleta umasikini bali mkono wenye bidii hutajilisha.
2019 Is the year of achievements
By
MOSES ZEPHANIA MGEMA
0755632375

Photos 14/08/2018

Story yakuvutia sana toka moja ya vitabu vya Robert kiyosaki "Rich dad and smart kid" anasema ivi Kipind cha ujana cha maisha ya mtu yeyote ndicho kipindi cha kuona fursa zaidi. Sababu kijana huwa na ndoto, malengo na mipango ya kufanikiwa zaidi.
Ushauri wangu kwa vijana wenzangu
Tutumie muda tulionao effectively.
Tafiti
Gundua fursa
Tumia fursa ukiwa na nguvu
Fanya kwa bidii kuitekeleza kila fursa unayoipata
Ikupe matokeo mema ya kuishi kesho.
Wakat mwema

"True Love love lives, fake love dies be careful."

03/07/2018

Members na rafiki zangu sikuwepo kwa takribani half year iv lakini Mungu mwema kuanzia Leo jioni......... Tutaanza somo zuri sana la Attitude (Mtazamo)/Hope mwisho wa siku kuna kitu utagain

05/09/2017

KINACHOMFANYA MTU ATOE MAAMUZI MABAYA AMA MAZURI NI MAMBO YALIOUJAZA MOYO WAKE KINACHOUJAZA MOYO NA NAFSI YA MTU HUMTENGENENEZEA MTU HUYO NAMNA YA KUONA (IMANI) NA NAMNA YA KUYACHUKULIA MAMBO (MTAZAMO)

(Mathayo 12:35) “Mtu mwema katika akiba yake njema hutoa mema na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”

(Mithali 23:7) “Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo”

kitabu cha Mithali 4:23Ukisoma kwa tafsiri ya kingereza“Be careful the way you think your life is shaped by your thought”

Maana yake kuwa makini na namna unavyofikiri ,maisha yako ni matokeo ya fikra zako

Vile vitu ambavyo mtu huambatana navyo ndivyo vitu ambavyo vinapata nafasi kubwa ya kuathiri nafsi yake au kuujaza moyo wake, Kwa mfano;aina ya vitabu anavyosoma, aina ya mziki anaopendelea kusikiliza, aina ya marafiki alionao. aina ya program za televishion anazopendelea kuangalia, aina ya mambo anayopenda kuyaperuzi kwenye mitandaoya kijamii Na kwenye intanet. Pia hapa hujumuisha mambo yote ambayo mtu huyu hupendelea zaidi kuyaona kuyasikia na kuambatana nayo kwa muda mwingi

Vitu hivi ambavyo mtu huyu huambatana navyo humtengenezea mambo makubwa mawili :

-{namna ya kuamini –beliving system}

-{namna ya kuyachukulia mambo-mtazamo(altitude)

Namna ya kuamini + namna kuyachukulia mambo= Aina ya maamuzi

“Namna ya kuamini na mtazamo wa mtu, ni k**a sumaku kwenye moyo wa mtu ambayo huvutia zaidi na kutoa nafasi kubwa zaidi kwa mawazo ambayo hayakizani na vitu ambavyo mtu huyu hupendelea zaidi kuambatana navyo , kwa sababu Maamuzi ya mtu hutegemea wazo lililopata nafasi zaidi kwenye moyo au fahamu za mtu hivyo, maamuzi ya mtu huyu yatafanana na vitu anavyoambatana navyo”

Aina ya maamuzi ambayo mtu huyafanya kwa kujirudia rudia yanapata nafasi zaidi kwenye moyo wa mtu humtengenezea mtu huyo Tabia na tabia hiyo inapojirudia mara nyingi zaidi hutengeneza Mazoea (addiction)

HIVYO MTU AKITAKA KUBADILISHA AINA YAKE YA MAAMUZI AU AACHANE NA TABIA FLANI

29/08/2017

Love is kindness, love comes without any label.

Photos 14/07/2017

THE POWER OF WOMEN.!

Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake.

Hata alipokuwa shuleni hakupenda mama yake amtembelee, na ikitokea mama yake akamtembelea basi watoto wenzie watamcheka siku nzima na kumtania. Hii ilimfanya mtoto huyu kujisikia vibaya sana na wakati mwingine kujuta kuwa na mama wa aina hiyo.

Lakini mama alimpenda mwanae na hakuonesha kukasirika hata pale mwanae alipomnyanyapaa waziwazi.

Badae mtoto akakuwa ak**aliza masomo yake na kupata kazi nzuri. Akafurahi kuwa sasa amepata kazi atakuwa mbali na mama yake 'chongo' anayemtia aibu.

Akachagua kufanya kazi mji wa mbali na alipo mama yake. Akafanikiwa kazini kwa kupandishwa cheo na akawa mtu mashuhuri mwenye mali na mwenye heshima kubwa ktk jamii yake.

Siku moja asubuhi akasikia wanae wakilia walipokua nje wakicheza.. Alipowauliza wakasema kuna mtu anawatisha.. Akatoka nje kujua nani anayewatisha wanae. Kufika akamkuta mwanamke mmoja mzee mwenye jicho moja (chongo). Kumbe wale watoto walitishwa na chongo la yule bibi.

Alipomtizama vizuri yule mwanamke akamgundua ni mama yake mzazi. Alikua amechoka na amezeeka sana. Amedhoofu mwili na anaonekana mgonjwa..

Mtoto kwa hasira akamuuliza "mama umekuja kufanya nini hapa? K**a una shida ungenipigia simu sio kuja? kwanza nani kakuonyesha ninapoishi? Na nani kamruhusu mlinzi kukufungulia mlango? Ona sasa umewatisha wanangu kwa chongo lako"

Mama yake akasema "samahani mwanangu, sikujua naomba unisamehe". Kisha mtoto akamchukua mama yake akamtoa nje na kumpeleka kituo cha basi ili arudi kijijini.

Baada ya siku chache kupita, yule jamaa akapata taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana na anahitaji kumuona. Akaondoka kwa siri kwenda kijijini ili akasikie mama yake anataka kumwambia nini.

Alipofika akakuta watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao. Alipouliza akaambiwa mama yake alifariki baada ya kuugua sana bila msaada wowote.

Alipoingia ndani akakuta barua aliyoandika mama yake.. Barua ilisomeka hivi...

"Kwako mwanangu mpendwa wa pekee,
Naandika barua hii nikiwa kwenye maumivu makali sana na sijui k**a nitapona.. Nimeugua nikakosa matibabu kwa kutokuwa na fedha. Sikuwa na mtu mwingine wa kumueleza shida yangu zaidi yako wewe mwanangu wa pekee... Lakini nilipojitahidi kuja kwako angalau unisaidie matibabu ulinifukuza na kudai nawatisha wanao kwa chongo langu ! Uliniumiza sana mwanangu sitisahau maishani mwangu ila nimekusamehe.

Baba yako alifariki ukiwa mdogo sana. Nami sikubahatika kupata mtoto mwingine. Nilikulea kwa nguvu zangu zote na umasikini niliokuwa nao ilikuwa nikitegemea badae utanisaidia lakini umenitelekeza na kunitupa kwa sababu tu mimi mama yako ni chongo ! Hivyo unaona aibu kuwa nami....

Nisamehe kwa kuwatisha wanao kwa chongo langu, nisamehe kwa kuja kwako bila ya taarifa, nisamehe kwa kukufanya uchekwe na wenzio kwa kuwa mimi mama yako ni chongo....

Lakini naomba nikupe siri ambayo hukua unaijua ewe mwanangu, wewe ndiye uliyezaliwa ukiwa chongo. Ulikua na jicho moja tu. Nikaumia sana kuona mwanangu ana jicho moja, atawezaje kuishi na kukabiliana na changamoto za maisha.. Nikaomba madaktari wanitoe jicho langu moja wakupe wewe, Niliona ni heri mimi niwe chongo kwa kuwa nimeshaona mengi sana duniani kuliko wewe..

Na ulipowekewa jicho langu nilifurahi kukuona una macho mawili nikajua utaweza kuzikabili vema changamoto za dunia hii... Na hakika jicho langu limekusaidia kwani wewe ni mtu mashuhuri na tajiri sana kwa sasa...

Lakini kwa jinsi ninavyoumwa najua nitakufa. Ila nafurahi kuwa nakufa nikiwa nimetimiza haja ya moyo wangu. Kwa kutumia jicho langu umeweza kuwa msomi mzuri na tajiri unayeheshimika na jamii yote.. Wasalimie wajukuu zangu na waambie wawe na amani hawataniona tena nikienda kuwatisha na chongo langu.. Please take care of my eye...

Akupendaye,
Mama"

Alipomaliza kuisoma barua hii akalia sana. Akatamani mama yake afufuke amuombe msamaha na amlipe kwa wema wake aliomtendea.. Lakini haikuwezekana, it was TOO LATE.!

MORAL OF THE STORY.!

Nyuma mafanikio ya kila mwanaume yupo mwanamke. Anaweza kuwa mama yako, mke wako, dada yako au mchumba wako.. Je unatambua nafasi yake katika mafanikio yako au unampuuza tu?

Wapo wanawake ambao walijitoa sadaka ili uweze kuwa hapo ulipo. Jiulize mama yako amefanya mangapi kukufikisha hapo.

Hadithi hapo juu inatueleza juu ya mama aliyetoa jicho lake kwa mwanae.. lakini jicho ni kielelezo tu cha yale wanayofanya mama zetu.

Kuna wengine jicho lao ni vibarua alivyokua anafanya ili wewe usome.. Pengine jicho lake ni namna alivyokua akijinyima kwa kuvaa nguo moja mwaka mzima ili upate ada ya shule na mahitaji mengine.. Je umewahi kumshukuru mama yako kwa kutoa jicho lake kwa ajili yako??

Mpende sana mama yako.. Wapende wanawake wote, waheshimu, walinde, wajali. Wanapitia magumu mengi sana ili kutufanya sisi wanaume tuwe k**a tulivyo.

Share ujumbe huu k**a sehemu ya kuonesha kutambua mchango wa wanawake katika jamii uliyopo.

Credit;
Siku njema

29/06/2017

Habari za wakati watu wangu wa nguvu, naamini mko poa kabisa.

Leo Nina neno dogo na fupi sana kwako mfanya biashara au mtoa huduma fulan ya kijamii
FAHAMU LEO KUWA ILI BIASHARA YAKO ISIPOTEZE WATEJE HAKIKISHA UKIYIMIZA MAHITAJI YAO KWA UBORA WA HALI YA JUU, KWA MUDA SAHIHI NA KWA LUGHA YA KUVUTIA WATEJA ZAIDI YA YOTE MFANYE MUNGU KUWA MHIMILI WA KAZI YAKO
USIKU MWEMA NAWAPENDA Sanat

Want your school to be the top-listed School/college in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Telephone

Website

Address


P. O. BOX 719, SINZA DAR ES SALAAM
Dar Es Salaam