02/01/2019
Mwaka 2018 umepita, tuna sababu ya kumshukuru Mungu sana kwa mengi mazuri aliyotutendea, mengi magumu aliyotuvusha, haikuwa rahisi hata kidogo maana ndugu jamaa, marafiki, majirani wameshindwa kuambana nasi kwa kuunza mwaka huu.
Ni kwa neema wala sio kwa welevu, ujanja, ubora na utakatifu mwingi uliotufanya kuwa hai, is by Grace tu ndo maana tuko hapa.
2019 tumeianza kwa amani na furaha kubwa, wengi tukiwa na matumaini makubwa kwa kuset, mipango, malengo, shauku na hamasa ya kwamba mwaka huu basi ni mwaka ambao ni mwaka wa taofauti
Kiuhalisia imekaaje, kiuhalisia kabisa kugeuza mwaka ni k**a kulala na kuamka siku mpya, au kutoka mwezi mmoja kwenda mwezi mwingine in short ni mwendelezo wa maisha yaleyale tu.
Kwa kweli ndugu zangu tufanye kazi zaidi kuliko kuongea, mipango bila utekelezaji wa majukumu au wa mipango hiyo ni sifuri.
Kuanza mwaka sio kigezo cha wewe kubadilika kitabia na kimtazamo bali, maamzi ya dhati ya kuacha tabia za mazoea ndiyo kitu kinaweza kukufanya kufikia malengo ya kile ulichokifanya.
Kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kuongea bila kutekeleza unachozungumza ni kazi bure. Lazimamabadiliko yaanzie kwenye fikra na maamzi ya dhati toka moyoni hapo ndipo unaweza kuona kweli mwaka umebadilika na uko tofauti na mwaka uliopita.
Katika kila jambo unalofanya mshirikishe Mungu, maana Mungu ndo mwamzi na maratibu wa kila jambo tunalofanya, ni signatory wa kila jambo kwenye maisha yetu hakuna sababu ya kuishi bila kumtegemea Mungu.
Kufanya mambo ambayo yanamsikitisha mzazi wako basi jua Mungu anasikitika zaidi na hapo unajichumia laana utakuwa ukifanya mambo lakini hufanikiwi kumbe umeishi maisha yenye kumchukiza muumba wako.
God ni kila kitu fanya kila jambo kwa kumshirikisha Mungu, toa sadaka, fanya ibada, achana na waganga, na kuwategemea viumbe ambao pia kesho na kesho kutwa watakufa, na Biblia inasema amtegemeae mwanadam amelaaniwa achana na kuwategemea kiumbe k**a wewe.
Jifunze mara kwa mara ili kuujengea ubongo wako maarifa mengi kwa ajili ya matumizi yako binafsi na jamii.
Epuka mogogoro isiyo ya Lazima, hata k**a ni ya lazima basi jitahidi kuepukananayo kwa kila hali.
Samehe kwa kadili uwezavyo, ni afya ya akili nafsi na moyo, ukiombwa msamaha samehe, ukijua kuwa kila mtu anakosea, waweza kukosewa k**a binadamu samehe maana hujui kesho yako wewe
Usiwe mtu wa kubeba mambo yasiyokuwa na faidia hata kidogo, kumbuka jambo likitokea limetokea huwezi kulifuta zaidi ya kusamehe tu.
Ushirika na wenzako liwe ni jambo la lazima kwa mwaka huu, baraka zingine za mafaniko zimefungwa kwenye ushirikiano na watu, kupitia ushirika mzuri na watu hapo ndipo unajenga connection na channels zingine ambazo huwezi zipata ukiwa pekee yako k**a mkiwa jangwani.
Hekima, Busara ni jambo jema kwa mwelekeo mzuri wa maisha yetu.
Nikutakie baraka za Bwana kwa mwaka huu, ukawe mwaka wa ushindi na utajiri kwa kila nyanja ya Maisha yako.
Kumbuka mkono mlegevu huleta umasikini bali mkono wenye bidii hutajilisha.
2019 Is the year of achievements
By
MOSES ZEPHANIA MGEMA
0755632375