23/05/2018
Katika urimwengu wa biashara saa nyingine hali ilivyo inashangaza, eneo hilo hilo watu, watu wale wale, bidha hiyo hiyo na bei ile ile ila utashangaa kwamba, Mtoa huduma huyu anafanikiwa kuuza na kupata wateja wengi hadi anashindwa kuwahudumia wakati mwingine anahangaika kupata wateja. sababu ziko nyingi ila binafsi hapa nafikiria suala zima la Huduma kwa wateja (Customer care).
hili ni suala linalotakiwa kupewa kipaumbele sana katika biashara na katika huduma yoyote mtu anayoitoa kwa wateja wake. Huduma kwa wateja ni huanza hata kabla mteja hajafika ofisini kwako au mahali pako pa kazi, huanza pale anapopiga simu , namna unavyopokea simu yake, namna unavyomwongelesha kwenye simu, atakapofika mlangoni pa ofisi yako namna unavyompokea, unavyomwelezea bidhaa ulizo nazo, unavyojibu maswali yake, unavyohudumia na baada ya huduma unavyomuaga pindi anapokuwa anatoka ofisini kwako.
haishii hapo, inaendelea hadi kwenye namna unavyohusiana na mteja wako baada ya kuwa umemhudumia, je unaendeleza mahusiano mazuri! au baada ya kutoa huduma na kulipwa basi huna haja n aye tena!
nwisho wa siku ni lazima mteja afurahi na ajisikie huru kabisa kufanya kazi na wewe na pia kuhusiana na wewe. hapo ndipo biashara itaenda vizuri. Mahusiano na mteja liwe jambo la msingi na la kwanza. hata asiponunua siku hiyo huenda akaja siku nyingine.
Changamoto ni pale ambapo mteja anaingia ofisini kwako kukuletea fedha yake ili apate huduma yako ila anatoka amefokewa na amekasirishwa kwa namna anavyojibiwa na wafanyakazi au kuonesha kutok*mjali.
Je huduma kwa wateja ikoje ofisini kwako