03/05/2020
CHANGAMOTO YA MADALALI SOKONI
Moja ya Changamoto tunazokumbana nazo wakulima hasa wadogo ni MADALALI masokoni.
Nature ya Masoko yetu yote yameshikwa na madalali,Madalali wapo kwenye Nafaka,Kwenye Mbogamboga, kwenye Matunda n.k.
Mfano;Mkulima ukipeleka matikiti 6000 sokoni ,Wewe k**a mkulima huwezi kuyauza ni lazima umkabidhi Dalali ayauze hizo ndo taratibu za masoko yetu.Na kwa kila tikiti litakalouzwa dalali yake ni Tsh 200.Haijalishi tikiti limeuzwa kwa Tsh ngapi either elfu 2,elfu 1 au hata Mia 5.
Kwa matikiti 6000 Dalali anatengeneza hela yake Tsh 1.2M.Matikiti elfu 6 yanaweza yakauzwa ndani ya siku 1 au mbili Tu.
Hii hupelekea wakati mwingine mkulima kupata hasara au faida ndogo na kuchukia kilimo kabisa,maana gharama za uzalishaji huwa kubwa ukizingatia mkulima kahangaika na matikiti zaidi ya miezi 2,kakodi shamba,kaajiri vijana,kanunua mbegu,madawa,mbolea,usafirishaji kutoka shamba hadi sokoni n.k.
Nini Kifanyike?
1.Serikali (Wizara ya Kilimo,Wizara Ya Viwanda Na Biashara),Taasisi zinahusika na Kilimo & Masoko i.e zitusaidie katika ku control madalali masokoni.
2.Mkulima kabla ya Kulima hakikisha unajipanga na suala zima la soko.Usitegemee aina moja ya soko.
3.Wakulima tupate platform ambayo inaweza ikatuunganisha moja kwa moja na mnunuzi au mlaji wa mwisho wa mazao yetu bila kupitia mikononi mwa madalali.
Hii itasaidia kuinua wakulima na kuhamasisha watu wengi zaidi kuingia kwenye kilimo na kupunguza tatizo la ajira Nchini.