10/01/2026
Alhamdulillāh 🤲
Kwa uwezo na neema za Mwenyezi Mungu , leo tarehe 10/01/2026, Taasisi ya AL AMEEN FOUNDATION – AIF imefanikiwa kugawa vifaa vya shule kwa watoto yatima wapatao 150, ikiwa ni sehemu ya juhudi zetu za kuinua elimu, utu na matumaini ya watoto wetu.
Hafla hii tukufu ilipambwa na uwepo wa viongozi na wanazuoni mbalimbali wa dini, wakiongozwa na:
Sheikh Mohammed Nassor Amran – Kiongozi Mkuu wa Taasisi
Sheikh Omar Mgaza – Kutoka Ofisi ya M***i
Sheikh Dau Silima – Kutoka Waqf na Mali Amana Zanzibar (Kitengo cha Zakaah na Sadaka)
Sheikh Ahmad Rajab Msomi – Kutoka Chuo Kikuu cha Al Azhar Shareef, Misri.
Viongozi hawa walitoa nasaha, dua na hamasa, wakisisitiza umuhimu wa kuwalea yatima kwa misingi ya dini, elimu na maadili mema, sambamba na kushirikiana katika kazi za kheri kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu.
Tunatoa shukrani za dhati kwa wafadhili wote, wadau, wanachama na kila aliyeshiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha tukio hili.
Mwenyezi Mungu awalipe kheri nyingi, abariki mali zenu na aweke matendo haya katika mizani ya mema.
📌 AL AMEEN FOUNDATION – AIF itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhudumia jamii, kusaidia yatima na kuwekeza katika elimu kwa ajili ya kizazi cha leo na kesho.
“Na wanakuuliza watumie nini. Sema: Kheri mnayotoa ni kwa wazazi, jamaa, yatima, masikini na wasafiri.” (Al-Baqarah: 215)
🤝 Karibu tushirikiane katika kheri.
Goreeb & Yateem Trust Fund
Kijana Wa Kiislam Dsm
Kijana wa Kiislam Tanzania
Najivunia kuwa Bint wa Kiislam
Najivunia kuwa Muislam