21/08/2026
UNAWEZA KUACHA UGALI… LAKINI BADO UKAWA HUJAANZA KUCHOMA MAFUTA.
Ngoja nikueleze…
Kuna mama mmoja aliniambia:
“Coach, nimeacha wali, ugali, mikate na sukari…
Lakini uzito wangu umesimama.”
Nilipomuuliza anakula mara ngapi kwa siku, akasema:
“Asubuhi nakunywa chai.
Baadaye nakula karanga kidogo.
Mchana nakula.
Jioni nakunywa juice.
Usiku nakula chakula.”
Nikamuambia:
Tatizo si chakula unachokula pekee…
Tatizo jingine ni kwamba mwili wako haupati muda wa kumaliza kile ulichopewa.
Kila unapokula—hata k**a ni “kidogo tu”—mwili unapokea kazi mpya.
Unapokula mara nyingi siku nzima, insulin inaweza kubaki ikipanda mara kwa mara.
Na insulin ikiwa juu, mwili hupokea ujumbe wa:
“Hifadhi nguvu… usifungue mafuta yaliyohifadhiwa.”
Ndiyo maana mtu anaweza kuacha ugali…
Lakini bado akawa anakunywa chai yenye maziwa, anakula karanga, matunda, juice na vitafunwa kutwa nzima.
Kwa macho yake anaona anakula kidogo.
Lakini mwili wake unaona:
“Chakula kinaendelea kuingia.”
Hapa ndipo wengi wanapokosea.
Kupunguza uzito si kubadilisha aina ya chakula pekee.
Ni pia kuupa mwili muda wa kutumia chakula ulichokula kabla hujaongezea kingine.
Kwa hiyo, kuanzia leo…
Usiangalie tu umekula nini.
Jiulize pia:
“Nimekula mara ngapi?”
K**a huna njaa ya kweli, usile kwa sababu tu chakula kipo.
Usile kwa sababu ni muda wa chai.
Usile kwa sababu umeona mtu mwingine anakula.
Na usijidanganye kwamba kitafunwa kidogo “hakihesabiki.”
Mwili wako unakihesabu.
Sasa nataka nijue hali yako…
Kwa kawaida unakula au kunywa mara ngapi kwa siku—mara 2, 3, 4 au zaidi?
Andika idadi yako hapo 👇
Usione aibu—andika ukweli.
Nitasoma majibu yenu, kisha somo linalofuata nitawaonyesha tofauti kati ya njaa ya kweli na hamu ya kula tu.
Huenda hapo ndipo utakapogundua kitu ambacho kimekuwa kinakuzuia kwa muda mrefu.