20/06/2020
USILETE UTANI KATIKA MAPENZI
- Mdada Mmoja alitaka kujua ni kiasi gani anapendwa na mume wake, hivyo akataka kujua mumewe _ atafanya nini endapo ataamua kuondoka na kumuacha!
Mwanamke Huyo akaamua kuandika Barua inayosomeka "Samahani mume wangu, Nimeamua kuondoka na kwenda kuanzisha maisha mapya mbali na wewe" Barua hiyo akaiweka juu ya meza iliyokuwa chumbani
Baadae Jioni, muda wa mumewe kurudi mwanamke Huyo akajificha chini ya Uvungu wa kitanda, mule chumbani mume alipoingia
Akakuta Barua Ile Ipo juu ya meza akaisoma
Kisha akaandika maneno Fulani kwenye Ile Ile Barua, harafu akaanza kuimba imba kwa Furaha huku akiwa anapiga miluzi na akiwa anavua nguo.
Mara akapiga simu na akasikika akisema Hivi *Hello mpenzi nina Raha sana Leo....yule mwanamke nuksi ameondoka mwenyewe bila kumfukuza na kutuachia uwanja jiandae Nakuja * muda Huo huo mume akaondoka
Mwanamke alipokuwa uvunguni akawa analia na kutokwa na machozi akaamua kutoka, huku akiwa amenyong'onyea na ameloa mashavu kwa machozi
Akasogea pale ilipo barua na akataka kujua mumewe aliandika kitu gani kwenye Ile Barua !! Akakuta maneno haya " Nimekuona miguu yako upo chini ya Uvungu tafadhali Andaa chakula nina Njaa Sana
Mumeo ila Nimetoka kidogo nafuata maziwa nilisahau kupitia. Nakupenda mke wangu...
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
-Hivi Nani kampatia mwenzake ??