30/05/2023
Sote twajua nafasi ya ibada ya hijja kuanzia nafasi yake katika nguzo za kiislamu furaha yake moyoni na msamaha mkubwa wa madhambi kwa aliye hija kwa kukidhi vigezo .
Hijja ni ibada ambayo mwislamu k**a hajaitekeleza muda wote nafsi yake inahisi mapungufu makubwa sana katika ukamilishaji wa uislamu
Allah kwa rahama zaka ibada hii akailazimisha kwa wenye uwezo tu
Na hapo nyuma wakati waislamu walipokuwa na utawala wa kiislamu basi utawala wa kiislamu ulikuwa ukisimamia ibada hii na kuirahisisha kuwa nyepesi kwa mahujjaji na si biashara kausha damu k**a ilivyo leo hii
Leo hijja imekuwa ni biashara ya kukomoana. serikali ya SAUDIA na mashirika ya kusafirisha mahujaji wame amua kwa pamoja kuwakomesha mahujaji .
Katika dhurufu k**a hizi nanawapa pole waislamu wote ambao hawajahiji na wana nia ya kuhiji.
Ama wale ambao wapo tayari kwenda hijja msimu huu basi wawe na subra na uvumilivu na wasife moyo na waendelee na azma yao hiyo ya kufika hijja
pato wanalo kwapuliwa na SUDIA kwa kushirikiana na tasisi hizi watalikuta siku ya QIYAMA
ifahamike sio haramu kuwepo taasisi ya hijja na kuchukua gharama bali upandishaji wa gharama za hijja tena kwa kiwango cha juu na kufanya watu wengi washindwe kuhiji huu ndio utapeli na haramu
kwanini wasichaji gharama halisi za usafiri, hoteli, chakula , mnyama, nk gharama halisi kisha kutia faida kidogo tu?
Taasisi ina utitiri wa viongozi wajumbe na wana hisa nk.
wote hao maisha yao ya
mwaka mzima yana bebwa na mahujaji hivyo lazima mahujaji wakamuliwe .
Na baadhi ya taasisi ni mtu na family yake na jamaa zake wa karibu tu ili kudhibiti pato hili kubwa na la haraka kupatikana
Tahamiki biashara ya kusafirisha mahujaji imekuwa ni moja ya biashara yenye kuleta utajiri wa haraka wa wachuuzi hawa wa ibada hii
Keifa safari ya kwenda CHINA mwezi mzima ni rahisi kuliko kwenda SAUDIA wiki mbili?
Pia nawapa nasaha wale waislamu wenye niya ya kwenda hija msimu huu mambo kadhaa ya kuzingatia
1 usichukue mkopo kutoka kwa mtu yeyote kwa malengo ya hijja au taasisi yoyote ya kibenk hata ikiitwa BENK YA MTUME, unapoteza muda na pesa zako bure.
2 usipelekwe hijja kwa msaada na hali huku nyumbani kuna madeni au family hawajui watakula nini kwa sababu tu umepata tiketi ya bure. Ukipata tiketi ya bure jipange kwanza nyumbani na pia k**a unadaiwa weka sawa
3 usipokee msaada wa kwenda hijja kutoka taasisi ambazo kazi zake ni za haramu wazi k**a hizi benk au taasisi zenye shub,haat kwa kuchanganya miamala ya haramu na halali k**a zinazo jiita benk za kiislamu au hisa za kiislamu
4 usitumie chumo lako la haram kwenda hijja bali tumia la halali tu ,usuzidiwe na majahili wa kikuraishi ambao walizuia chumo la haramu kujengea AL-KABA
5 Usiende hijja k**a mazowea na mtindo au utalii k**a inavyo taka kufanya sasa hivi serikali ya SAUDIA, kuifanya ibada ya hijja ni utalii na sio ibada ,hivyo wataruhusu hata pagani asiye na dini aende hijja
Mwisho
Tumuombe ALLAH awafanyie wepesi mahujaji wote wenye niya kwenda msimu huu na awakubalie ibada yao hii adhimu ya hijja waende salama na warudi salama
NI NASIO