12/11/2020
Adhabu ina elimu yake pia
Zingatia haya wakati Unamwadhibu Mwanafunzi
Kutokana na kesi kuwa nyingi za walimu kuwachapa wanafunzi hadi kuzimia na kufa kabisa. Leo nakupa maelekezo ya kuzingatia wakati wewe mwalimu au mtu yeyote yule unamwadhibu mwanafunzi.
Na msomibora.com (masomo sekondari)
1. Kisheria mwanafunzi anatakiwa anaadhibiwe viboko vitatu tu.
2. Na k**a itaonekana adhabu hiyo ya viboko haimtoshi mwanafunzi, basi aongezewe adhabu nyingine k**a ile kufyeka, kuchimba mashimo nk
3. Ikionekana huyo mwanafunzi bado ni sugu yaani hataki kubadilika, basi aitwe mzazi au mlezi wake hapo shuleni, mzazi ataelezewa makosa anayofanya mwanae, na ajionee mwenyewe tabia ya mwanae ilivyo.
4. Mwanafunzi huyu ikiwezekana aadhibiwe mbele ya wanafunzi wote (mstalini) na mzazi wake akiwepo, hii itamtia aibu sana huyu mwanafunzi. Maana atakuwa amejiharibia heshima yake kwa wanafunzi wenzie na hata huko nyumbani.
5. K**a huyu mwanafunzi bado ataendelea kuwa mkaidi, basi k**ati ya nidhamu ya shule, itaamua kumsimamisha masomo (suspension) kwa muda fulani, au hata kumfukuza shule kabisa k**a itabidi.
6. Usimchape mwanafunzi ukiwa na hasira sana, hii sio vita, bali kumsaidia mtoto arudi katika njia nzuri.
7. Usimwadhibu mwanafunzi k**a njia ya kulipa kisasi kwake, labda kuna kitu alikugomea. Ukifanya hivi mwanafunzi atakuelewa tu.
8. Usimchape mwanafunzi kwa sifa ili walimu wenzako wakuone wewe ni hodari, hapa utajikuta unavunja taratibu za kutoa adhabu na kusababisha maafa, na hata mwanafunzi ajitetetee akitaka kupigana na wewe.
9. Viboko sio adhabu pekee, jifunze kutumia njia zingine k**a kuonya, vikazi vya kumchosha kidogo k**a kufuata maji, kupalilia viunga vya shule n.k
10. Usipende sana kutumia viboko kwa wanafunzi wa vidato vya juu k**a form 5 na 6, hawa wengi wao huwa wanajielewa, kwahiyo kaa nao ukiwaelekeza.
11. Usiwachape wanafunzi wa k**e makalioni, kibaolojia sio salama kwao, wachape mikononi.
--
π MsomiBora.com
Notes for Secondary Schools