15/01/2021
Jinsi ya kumsahau mtu aliyekuacha au mliyeachana na bado unamhitaji lakini haiwezekani Tena kurudiana👉🏼
1. Jua kuwa hakuna kisicho na mwisho, hata Hilo litaisha. Utamsahau. Kwanza unamfanya nani kwako hata moyo wako uendelee kuteseka?
Mwenzako usikute anakula kuku huko aliko hata hakufikrii. Halafu wewe kila siku unalia. Unajidharau Sana. Unakesha unalia halafu bank hamna salio. Hizo nguvu si ukatafutie pesa mwanangu!!😃
2. Yanaumiza, sawa, ila kubali umeachwa. Usipokubali itakusumbua Sana. Kubali moyoni. Kubali hata K**a unajihisi bwege kwa Hilo. Ila kubali tu halafu amua kuanza upya Sasa. Huo ndio uanaume na u superwoman. Sasa superwoman kilio kila siku jamani!
3. Kaa chini fikiria vitu ambavyo ulikosea, na virekebishe, K**a huoni kosa Basi hakuwa wako. Je unataka asiye wako? Halafu ukihisi Yuko na mwingine, siyo kwamba hufai, ila haikuwa sahihi kwako
4. Kuna watu wazuri wengi jamanii. Kweli inauma lkn Kuna wadada na wakaka wazuri huko nje jamanii. Unang'ang'ania sahivi una miaka unateseka tu. Move on, start over. Muoneshe kuwa unaweza ukaishi bila yeye. Unambembeleza miaka inaenda kwani yeye Ni cake😃
5. Angalia future yako. Focus on it. Tengeneza future yako, jiongeze, fanikiwa, ili aje ajilaumu. Unavyojiumiza unachakaa, piga kazi, Soma, baadaye ung'ae. Akirudi mwambie Am no longer the same person😃
6. Uliyeachana naye usiwe adui yake. Usimfanye adui ila mind your own business. Usimfanye kitu kibaya maana hujui baadaye mtakuja kutana wapi.
6. Jiamini kuwa unaweza. Unaweza kuanza upya na unaweza kumpata aliyesahihi na ukatulia na kusahau kabisa maumivu. Move on.
7. Muombe Mungu akupe wepesi, apoze maumivu, na umsahau. Kwanza wewe siyo wa Kwanza.
Be strong, be strong, acha kuteseka.
God loves u