08/01/2023
Kuwa mtu wa thamani katika dunia hii si rahisi/ sio kazi ndogo. Kuna gharama ya kulipa. Baadhi ya watu wanashindwa kuwa vile ambavyo Mungu amewakusudia kwa kushindwa/ kuogopa kulipa gharama. Unakuta mtu ndani yake anaambiwa na Mungu wewe nimekuumba kuwa mwanzilishi na mmiliki wa viwanda kwa kuogopa kuingia gharama anakimbilia kuajiriwa/ kwenye ajira yaani anakimbilia kwenye wito ambao sio wake. Usiuze maono aliyokupa Mungu kwa kuogopa kulipa gharama.
Kuna wengine tumeitwa kuwa watengeneza njia za wengine hivyo tusitegemee kuishi maisha mepesi wakati wa kuanza kutengeneza njia/ barabara ili wengine nao waanze kupita.
Je uko tayari kutengeneza njia, kipindi cha kutengeneza njia, mtengeneza njia huwa haheshimiki ila majibu yakianza kuonekana/ njia ikikamilika ndipo huanza kuheshimika.
Mungu akikupa heshima ya kutengeneza njia ujue nyuma kuna watu wanaokufuata. Mtengeneza njia huwa haeleweki kwa walio nyuma yake.
Mtengeneza njia anaweka maisha yake rehani ili njia ziweze kufunguka. Watengeneza njia ni lazima Mungu atupe tuzo ya kututambulisha. Mungu akikutambulisha katika uwepo wake/ wingu lake zito watu watakuelewa.
Kwenye kutengeneza njia Kuna gharama.
To be somebody worth/ valuable in this world is not easy. There is a price to pay.