03/12/2022
Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yafanikiwa kufanya mafunzo ya awali kwa walimu mwaka 2022.
Siku ya tarehe 25 Novemba 2022 saa 3:00 asubuhi, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilifanya sherehe za ufunguzi wa mafunzo ya awali ya mwaka 2022 katika ukumbi wa mikutano ulioko katika jengo la Taasisi ya Confucius. Hafla ya ufunguzi iliongozwa na Prof. Mutembei, mkurugenzi Mtanzania wa taasisi ya Confucius, Mheshimiwa Wang Siping, mshauri wa balozi kitengo cha utamaduni cha ubalozi wa China Tanzania na Prof. Mfinanga, makamu mkuu wa chuo utawala, chuo kikuu cha Dar es salaam walihudhuria na kutoa hotuba zao. Prof. Zhang Xiaozhen, Mkurugenzi Mchina wa taasisi ya Confucius chuo kikuu cha Dar es salaam, na Viongozi saba wa chuo kikuu cha Dar es salaam kutoka idara mbalimbali walihudhuria mkutano huo, na Mwalimu Liu Fang alizungumza kwa niaba ya walimu wapya wa kujitolea. Walimu wote wa Taasisi ya Confucius chuo kikuu cha Dar es salaam walihudhuria sherehe ya ufunguzi wa mafunzo haya ya kabla ya kazi.
Viongozi na wawakilishi kutoka Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Mafunzo ya Shahada ya Kwanza, Ofisi ya Utumishi, Ofisi ya Mambo ya Nje, ndaki ya Insia, Shule ya Elimu na Ofisi ya Udhibiti Ubora walitambulisha kwa ufupi kazi zao na muundo wa idara zao, pamoja na uhusiano uliopo kati ya Taasisi ya Confucius na idara hizo. Inatarajiwa kuwa walimu na wanafunzi zaidi wa Taasisi ya Confucius watashirikiana kikamilifu na idara hizi katika siku zijazo.