26/08/2026
Wanangu wa Man U mnajisahau sana kumlinganisha Captain BF na Super Frank.
Wanangu, mjue mnayejaribu kumlinganisha naye ni mfungaji bora wa muda wote wa Chelsea, mtu aliyefunga mabao 211 akiwa na The Blues, mshindi wa nafasi ya pili kwenye Ballon d’Or mara mbili, Bingwa wa Ulaya, kiungo aliyefunga mabao 177 katika historia ya EPL, Bingwa wa EPL mara 3, na Mchezaji Bora wa EPL mwaka 2005, huu msimu alitoa Assists 18 na mabao 13 na Chelsea ilibeba Epl.
Tafuteni mtu mwingine wa kumlinganisha lakini sio super frank watoto wadogo.
Steve Leonard Champion