Tafes_nct family

Tafes_nct family We are the family to make other students become followers of Jesus by preaching the word of God within the college and out of the college

01/09/2023
Baba ubarikiwe kwa kazi ya Mungu unayo ifanya.
14/04/2023

Baba ubarikiwe kwa kazi ya Mungu unayo ifanya.

*Nitajuaje kuwa nimesamehewa dhambi zangu?* Pale unapotubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha maovu, na maisha ya kale ya dha...
09/02/2023

*Nitajuaje kuwa nimesamehewa dhambi zangu?*

Pale unapotubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha maovu, na maisha ya kale ya dhambi, wakati huo huo Mungu anakusamehe dhambi zako kabisa kabisa. Lakini hutasikia, hisia Fulani, au badiliko Fulani la wakati huo huo, kwani fikra zako za dhambi za zale bado zitaendelea kuzunguka kwenye akili yako. Hivyo wengi wakishaona hivi wanadhani kuwa Mungu hawajawasamehe, na hivyo wanaendelea kubaki katika mashaka, au kurudia rudia kumlilia Mungu awasamehe.

Na hapa hapa shetani ndipo anapata nafasi ya kuwatesa, na kuwakandamiza, wengine wanajikuta kila siku wanaomba Toba Mungu nisikie unisamehe!, Mungu nisikie unisamehe!, kumbe tayari Mungu alishawasamehe tangu siku ile ya kwanza walipomaanisha kweli kweli kugeuka na kukataa kurudia dhambi zao.

Ndugu, fahamu hata k**a wewe utakuwa na kumbukumbu la nyuma la dhambi zako, lakini kwa Mungu ni tofauti, yeye akisamehe anasahau kabisa.

Waebrania 8:12 โ€œKwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tenaโ€.

Unapokwenda mbele za Mungu, lazima uamini kwa moyo wako wote umeshasamehewa, vita vya kimawazo vinavyoanza kuja tangu huo wakati, huna budi kuvishinda, kwa kuvipinga, ukisikia moyoni mwako unaambiwa, aah! Wewe dhambi zako ni nyingi, ile dhambi ulishamkufuru Roho Mtakatifu, pinga, kataa sema mimi nimeshasamehewa kwa damu ya Yesu Kristo.

Kisha unavyozidi kufanya hivyo baada ya kipindi Fulani utaona amani ya Mungu imekuvaa.

Lakini pia ni lazima ukumbuke kuwa yapo mambo yanayochangia pia kusamehewa dhambi zetu, na yenyewe ni sisi kuwasamehe waliotukusea k**a wapo.

Bwana Yesu alisema..

Mathayo 6:14 โ€œKwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenuโ€.Hivyo uombapo msamaha zingatia kuwa moyo wako ni mweupe kwa wengine.

Pale unapotubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha dhambi, wakati huo huo Mungu anakusamehe kabisa kabisa, hutasikia hisia fulani, au sauti iku...

Take your order now and get your T-shirt without late because few of them remain
24/01/2023

Take your order now and get your T-shirt without late because few of them remain

๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ 9 days to go, to our special adoration that we plan to do it in our best levels; my dear plan to attend and don't ev...
24/01/2023

๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ๐Ÿ’ƒ 9 days to go, to our special adoration that we plan to do it in our best levels; my dear plan to attend and don't ever plan to miss. Just save the date and tell your friends to tell their friends that abiding in Jesus is better than everything in the world. "Revived Spirit" ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

22/01/2023

*UWE KIELELEZO.*
"Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi."
- 1 Timotheo 4:12.

Kila Mtoto wa Mungu ni barua inayosomwa na watu wote, ni mfano wa Mungu, hivyo wengine humuona Mungu kwa namna tulivyo na tunavyoishi.

Maisha yetu sio ya kwetu peke yetu kwa maana kwamba tunaishi na watu wengine, kwahiyo hata tunavyoongea, tunavyovaa sio kwaajili yetu tu na Mungu ni kwaajili yetu na watu kwasababu sisi ni kielelezo kwa watu sio kwa Mungu.
(Mungu hatuigi, watu ndio wanaotuiga)

Kila Mkristo ni somo kwa wengine, wanaokutazama, unaoishi nao wanajifunza kwako. Ndivyo tulivyo umbwa katika upya wetu lazima, tuishi NENO la Mungu katika USEMI na MATENDO.

Paulo Mtume ana msisitiza mwanae katika Imani, Timotheo, awe kielelezo kwa hao waaminio, hapa nataka niongeze kwa hekima ya Mungu kwamba tunapaswa kuwa kielelezo kwa wanaoamini na wasio amini.

Watu wa kikutazama wanamuona Yesu? wanaona Hekima ya Mungu? wanaona bidii? wanaona upendo? Wanaona utakatifu?

Maisha unayoishi yanapaswa kubeba ushuhuda wa Kristo, ushahidi wa Injili utakao wafanya wanao amini waendele kuamini na wasioamini wapate kuamini.

Pale ulipo, iwe ni kazini(mahali pako pa kazi), iwe ni kwenye ndoa au katika huduma, wewe ni kielelezo kwa mume au mke wako, mfanyakazi mwenzako, wakristo wenzako na watu wote wanao kuzunguka.

Hupaswi kuwa sababu ya mtu Mwingine kuiacha imani au kutikufurahia wokovu, unapaswa kuwa kielelezo kinachochochea wengine kumpenda na kumwamini Mungu.

Kuwa kielelezo ni Kuwa mfano halisi unaofaa kufuatwa au kuigwa. Maisha yetu hayapaswi kuleta shaka wala wasiwasi kwa watu wengine, wakashindwa kuelewa kweli tuna Mungu au tunaigiza.

Tunapaswa kuwa kielelezo katika;
โ€ข Usemi, namna yetu ya kuzungumza, matamko tunayotoa lazima yalingane na neno la Mungu. Sema K**a Mungu, kwasababu watu wanaiga usemi wetu.

โ€ข Mwendendo, mtindo wako wa Maisha, matendo unayotenda, udhihirisho wako. Mungu atusaidie.

Hata Sasa Mungu amekuwa ebeneza katika maisha yetu.
22/01/2023

Hata Sasa Mungu amekuwa ebeneza katika maisha yetu.

21/09/2022

Yeremia 32:26-27 Imeandikwa,
"Tazama mimi ni Bwana Mungu wa wote wenye mwili.
Je,kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?" Neno hili liondoe kila kilicho kigumu ktk maisha yako,
Mungu akutendee miujiza itakayoshangaza wote wasioamini.
Mungu aangushe ngome za maadui zako wote waliokuzunguka.
Pia ajibu kila uombalo kuhusu wito wako, uchumi, afya, ndoa, elimu, watoto kwa jina la Yesu Kristo.

Address

Mahunda
Dar Es Salaam
NATIONALCOLLEGEOFTOURISM

Telephone

+255753145760

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tafes_nct family posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Tafes_nct family:

Shortcuts

Share