04/08/2022
ELIMU JUU YA RUTUBA YA UDONGO.
âś…Rutuba ya udongo hutengenezwa na vitu vitatu muhimu ambavyo ni uasilia wa kibaiolojia, kikemia na kifizikia.
âś…Kati ya hayo, utunzaji wa udongo unategemea kwa kiasi kikubwa na mazingira ya kibaiolojia.
✅Viumbe hai wana mchango mkubwa sana katika kuendeleza rutuba ya udongo. Kazi yao kubwa ni kumeng’enya mabaki ya mimea, wanyama na viumbe hai wengine. Mchakato huu husababisha uwepo wa virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa pamoja hutengeneza rutuba kwenye udongo.
▶️Njia rahisi ya kutambua baiolojia na ufanyaji kazi wa udongo ni kwa kuangalia uwepo wa nyungunyungu (earthworms).
▶️Kujua muundo wa udongo husaidia kuweka usawa kati ya upitishaji wa hewa safi, umwagiliaji na ushamirishaji wa mizizi.
▶️Pembejeo za kilimo hai pamoja na mbinu za kilimo zinazosaidia katika kuzuia kusumbuliwa kwa udongo na kusawazisha upatikanaji wa viumbe hai zinaweza kutumiwa ili kuimarisha udongo na kulinda ardhi.
▶️Udongo wenye rutuba hauwezi kugandamana, hasa wakati wa mvua nyingi, ama kupasuka-pasuka wakati wa kiangazi, una harufu nzuri, una viumbe hai ama unaonyesha uwepo wa viumbe hawa, na mimea huonekana yenye afya.