18/02/2026
WHAT IS PORTABLE APPLIANCE TESTING? (BS7671, IEC60364-6, ISO 14001)
Huu ni mchakato muhimu ulioundwa ili kuhakikisha usalama wa vifaa vya umeme vinavyotumika katika mazingira mbali mbali.
IEC 60364-6:2.1.1.1
Hiki ni kiwango cha tume ya kitaifa ya ufundi wa electronics ambacho kinatoa miongozo ya uthibitishaji wa mitambo ya umeme.
IEC 60364-6:2.1.1.2
Hii ni sehemu ya sheria ya sita ambayo inazungumzia hasa vifaa vya umeme vya voltage ya chini ambayo inaeleza mahitaji ya ukaguzi wa mara kwa mara na upimaji wa vifaa vya umeme vinavyobebeka.
BS7671:2.1.3.1
Hiki ni kiwango cha uingereza kinachojulikana pia k**a kanuni za wiring za IET kinacho jumuisha vifungu vinavyo husiana na ukaguzi na upimaji wa vifaa vya umeme vinavyohusu vipengele k**a vile usalama wa earthing, bonding na insulation ya kifaa.
ISO 14001:2.1.6
Hiki ni kiwango cha ISO cha usimamizi wa mazingira kinachohimiza mashirika kuanzisha na kutekeleza taratibu za kupunguza athari zao za kimazingira kwa kufanya upimaji wa Portable Appliance Testing (PAT)
Upimaji wa PAT ni ukaguzi wa usalama wa vifaa vyovyote vya umeme vinavyoweza kusogezwa au kuvichomoa kwenye umeme vinavyotumia plug, ambavyo vinajumuisha kila kitu kuanzia chaja ya simu yako ya mkononi, vacuum cleaner, pasi ya umeme, friji, machine ya kufulia, majiko ya umeme, vifaa vya hospital, vifaa vya viwandani n.k.
Fikiria k**a ukaguzi wa afya ya vifaa vyako vya umeme.
WHY DO WE NEED PAT TESTING? (Kwa nini tunahitaji upimaji wa PAT?)
Sote tunatumia vifaa vya umeme kila siku, mara nyingi bila kujua k**a vifaa hivyo ni salama kwa umeme, vifaaa vya umeme vyenye hitilafu vinaweza kuwa hatari na kukusababishia moto au kupigwa shock au kukusababishia bili kubwa ya umeme.
Ndio maana kupima mara kwa mara vifaa vyako si zoezi la kuhesabu tu, ni njia moja wapo ya kuwaweka watu salama.
AT WORK
K**a wewe ni mmiliki wa biashara, una jukumu la kisheria la kuweka wafanyakazi wako salama. Hii ina maana ya kufuata kanuni za usalama k**a vile sheria ya afya na usalama kazini.
Hakikisha vifaa vyako vyote vya umeme vinavyobebeka (Portable) viko katika hali nzuri ya kufanya kazi ni njia mojawapo ya kufanya mtendaji wa afya na usalama awe na fu