24/12/2022
CAREER DEVELOPMENT
Kipi bora kujiajiri au kuajiriwa? Usifanye haraka kujibu swali hili. Fikiri kwa kina kwanza.
Kila upande utakao chagua una faida na hasara. Itategemea wewe unatafuta nini katika maisha yako.
Natambua unalo jibu lako.Hebu tuangalie faida za kila kimoja. Baada ya hapo utakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuchagua upande unaoutaka.
FAIDA ZA KUAJIRIWA
1️⃣Uhakika wa kipato kila baada ya muda fulani. Kipato chako kinatabirika hivyo ni uhakika.
2️⃣Unakuwa katika nafasi nzuri kuweza kukopesheka na taasisi za fedha. Taasisi za fedha ziko tayari kumkopesha mtu mwenye kipato cha kuaminika (reliable source of income)
3️⃣Kujihakikishia kiinua mgongo au pensheni ya uzeeni.
4️⃣Fursa ya bima ya afya kwa wafanyakazi huwa ni rahisi zaidi.
5️⃣Ni shughuli ambayo haina risk kubwa. Hakuna uwezekano wa kupoteza pesa zako. Upande wa kujiajiri kuna wakati unapoteza mtaji wako kutokana na kupata hasara.
6️⃣Mbali na mshahara unaweza kupata marupumarupu ya hapa na pale pamoja na safari za kulipiwa.
FAIDA ZA KUJIAJIRI
1️⃣Mtu aliyejiajiri anapata faida za kodi (Tax advantages).Mwajiriwa hawezi kuepuka makato ya kodi kirahisi.
2️⃣Uhuru wa muda wako. Una maamuzi na muda wako. Unaamua kuutumia upendavyo wewe.
3️⃣Uhuru mkubwa zaidi wa maamuzi. Unakuwa na uhuru wa kufanya maamuzi yako bila kuingiliwa au kupangiwa na mtu mwingine.
4️⃣Uwezekano wa urithishaji. Mradi au shughuli binafsi unaweza kurithisha kwa watoto au ndugu zako. Lakini ajira hakuna kurithisha.
5️⃣ Uwezekano wa kuingiza mapato makubwa zaidi. Kwa aliyejiajiri hakuna ukomo wa kipato chake k**a ilivyo kwa mwajiriwa. Kadiri biashara inavyokwenda vizuri na kipato hupanda zaidi na zaidi.
6️⃣Kuna uwezekano wa kutajirika kwa haraka sababu biashara haitabiriki k**a ilivyo kwa ajiri. Mazingira yakiwa mazuri unatoka haraka.
Vp, bado una msimamo wako ule ule juu ya masuala haya? Nimeeleza upande wa faida pekee. Sijaeleza hasara au madhaifu ya kila upande.
Wewe unayo nafasi ya kuchagua unataka kuwa nani. Si jambo zuri kufuata mkumbo. Angalia malengo yako ni nini hasa. Kisha chagua upande unao utaka. Mimi si wale wanaoshinda wanadanganya watu mitandaoni.
Shea na marafiki
_____________
The best way to learn is to learn from the best