01/08/2026
Mtu aliyeokoka huwa anakuwa na ushirika na Mungu. Kuna mambo ambayo Mungu anamshirikisha. Jambo la kwanza ni asili yake ya uungu. Mtu anapewa asili mpya, asili ya Mungu.
Mtu huyo amepewa kuungana na Mungu katika roho. Yaani, anakuwa ameungwa na Bwana, na anakuwa Roho mja naye.
2
Anakuwa ameungwa na Mungu moja kwa moja, kila siku, kila saa. Hakuna wakati ambapo mtu huyo anapokuwa nje ya Mungu, au anapokuwa ametengwa na Mungu. Mtu huyo haungani na Mungu wakati wa maombi tu, bali ameungwa na Bwana 24/7
K**a umeokoka, unaishiriki asili ya Mungu, ya uungu. Una asili ya Mungu. Unafanana na Mungu; unamiliki, unatawala, unatiisha, unaumba (unazaa), anaongezeka.
Mtu aliyeokoka ameshiriki kifo na ufufuo wa Bwana Yesu.
Mambo niliyoyaelezea hapo juu ni matamu sana kusikia kwenye masikio. Lakini kwa wengine yatakuwa magumu sana. Soma tu 2 Petro 1:3-5.
Mambo hayo ni matamu masikioni, lakini hayadhihiriki kwa kila mtu. Tena, ni Yesu peke yake aliyeyadhihirisha kwa asilimia mia. Mimi na wewe hatujadhihirisha chochote bado. Hatua ya kwanza ya kuyadhihirisha ni kwa kuyafikirifikiri mambo ya Mungu yaliyo kwenye Neno la Mungu, k**a haya ninayokuandikia. Utakapoanza kwa kukubali, itakuwa hatua kuu sana, hautojilaumu kwa kupata huo ufunuo.