الحبيب الشيخ موني - Alhabiib sheykh mwinyi

الحبيب الشيخ موني - Alhabiib sheykh mwinyi Sufism

07/06/2021

🌫️🌺🪐🎙️Daka Lulu Chap Chap

Alhabiib sheikh mwinyi (JLT)
17 March 2021
Mbagala, MADIMBA

Katika vitu ambavyo muridi wanashindwa kupanda na kufika kwa mungu ni kutokuji control na ibada. Utakuta mtu yupo katika daira ama kikazi cha kumtaja mungu lakini muda mwingi anashughulishwa na simu, mara aende nje akaipokee, mara anyanyuke nyanyuka

Yote hii inatokana na kutokuji control yeye kwa yeye

Na ukitaka kujua faida ya kuji control watizame muridi wa zamani. Zama za kina juneyd baghdad,sirri saqatwi, syd abdulqaadiri jeylan,sheikh uweys ahmad nk.

Hata naqshaband (TWARIYQATUL) ukiwatizama katika majaalis zao wakishaanza tu ibada au uradi basi wanaachana na mambo yote ya kujishughulisha na nje ya mungu. Huwaoni wakipokea simu wala wakinyanyuka nyanyuka kwenda sehemu

Lakini ajabu ya muridi wa sasa! wakikaa katika daira basi muda wote wako na simu,mara wanyanyuke kutoka nje

Ukiwauliza nini kinachowanyanyua nyanyua utaskia naenda kupokea simu nje, hii ni AJABU!

Ibada ni ibada, na ibada yatakikana utulivu

Kwanini wakati wa swala yoyote ya faradhi au ya sunnah huachi swala na kupokea simu? au katika taraweh!

Hufanyi hivyo kwa sababu unajua upo direct ( moja kwa moja ) unazungumza na mola wako, basi na katika daira napo uwe hivyo hivyo, na tukitulia khaswaa katika madaira. Tukiwa na khushui ya hali ya juu khabbar zetu zitatupitia papo hapo, sio mpaka tulale usingizi.

Ibn syd othman aljamalullayl....✍🏼🐪

AFISA HABARI
ZAWIYANI KUNDUCHI

Address

Kanani
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when الحبيب الشيخ موني - Alhabiib sheykh mwinyi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to الحبيب الشيخ موني - Alhabiib sheykh mwinyi:

Shortcuts

Share