07/05/2022
Kazi yoyote ya utafiti hurejelea maandishi mbalimbali ambayo ni lazima yaonyeshwe pale mwishoni mwa utafiti wake.
Ubora wa references (marejeo) ni jambo kuzingatia unapoandika tafiti.
Sio kila rejeo (reference) inafaa kutumika katika tafiti.
Zifuatazo ni mbinu za kuchagua reference bora za tafiti yako:
1. Chagua references zisizozidi miaka 15 nyuma
Kwa mfano, ikiwa unaandika Tafiti yako mwaka 2022, references zako ziwe kuanzia mwaka 2007 na kuendelea
2. Chagua marejeo yako kwa kipaumbele/mtiririko huu;
o Makala ya jarida yaliyopitiwa na wataalamu wengine (Peer-reviewed journal articles) โ ๐๐ง๐๐๐๐ ๐ฌ๐๐ง๐
o Vitabu, ensaiklopidia na kazi nyingine za kisomi -๐๐ง๐๐๐๐ ๐ค๐ข๐๐ฌ๐ข
o Majarida, blogu, tovuti -๐๐๐ข๐๐๐ข ๐ฌ๐๐ง๐
3. Chagua marejeo yenye taarifa zilizokamilika k**a vile Jina la mwandishi, mwaka, mchapishaji, jina la jarida, n.k.
Taarifa pungufu huathiri ubora wa references zako. Jitahidi kutafuta taarifa kamili za rejeo
Je, umejifunza kitu? Tafadhali share na marafiki zako