17/04/2025
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Zuchu ameonesha kuvutiwa na singeli ya ‘Afande’ iliyoimbwa na Dogo Paten.
Wimbo huo wa Singeli ambao umekuwa ukifanya vizuri kwenye mtandao wa Tiktok umemfikia Zuchu na kumfanya aombe kolabo ya wimbo huo. “Aya nampa remix namtafuta,” ameandika Zuchu
Aidha kwa upande wa Paten amemshukuru Zuchu kwa kutambua kipaji chake. “Hakuna mafanikio rahisi kikumbwa kupambana, nashukuru sana hii kubwa kwangu,” Paten
Ikumbukwe Dogo Paten alianza kufahamika baada ya kufanya remix ya wimbo wa Marioo ‘Salio’.