10/03/2026
Umesikia kuhusu childhood trauma?
Umewahi kuadhibu watoto baadae ukagundua hata halikuwa kosa lao ni baadae unajuta na kujilaumu.
Umewahi kujiapiza kimya kimya au kwa sauti wanangu hawatapitia haya NITAWALINDA,NITAWAPA KILA KITU,MIMI MWANANGU HATAKAA KWA WATU…hizi herufi kubwa zoteee ni wewe wa utotoni aliyeumia ni wachache huwapa watoto wao raha ambazo sio KINGA DHIDI YA
Umewahi kutazama malezi k**a FURSA ya kupita utotoni kwako kujipa pole na kutengeneza KINGA YENYE AFYA kwa wanao,
Kwamba huwakingi na uliyopitia ila unawajengea uwezo wao kutoishi machungu yako na maumivu yako,Yes UKIPONA UNAWEZA hii inaitwa KUJILEA wewe taratibu,ukianza kuona wanakutonesha kumbukumbu mbaya za utoto wako andika chini ni kitu gani TAFUTA MSAADA maana tunalea tulivyo na tunatoa tulivyo
Wewe mwenyewe ni shahidi ulilelewa kwa kelele na sasa unalea kwa kelele na kuna mtoto hapo ana kelele k**a zako kwa wenzie🙌🏻😌