12/07/2022
🔖🔖🔖🔖🔖🔖🔖🔖🔖
*Laiti mtoa sadaka angejua kwa yakini kwamba sadaka yake inapokelewa kwa Mwenyezi Mungu kabla ya kuingia mkononi mwa masikini,ingekuwa ladha ya mtoaji....ni kubwa kuliko ladha ya mpokeaji..*
*-Ibn alqayyim*
Je unajua faida ya kutoa sadaka?
Sikilizeni enyi watoa sadaka, nyinyi na ambao wanasaidia kufikisha sadaka..
1- *Sadaka ni mlango miongoni mwa milango ya pepo*
2-Sadaka ni bora ya matendo mema, na sadaka bora ni kulisha chakula
3- *Sadaka inamfunika kivuli mtoaji na inamuondosha kwenye moto*
4-Sadaka inazima ghadhabu za Mola na joto la kaburi
5- *Sadaka ni jambo bora la kumzawadia maiti na inamfaa zaidi, na Mola anaitunza*
6-Sadaka ni usafisho, na utakaso wa nafsi na huongeza mema
7- *Sadaka ni sababu ya furaha kwa mtoa, na ni sababu ya kung'ara uso wake siku ya kiama*
8- Sadaka inaleta amani kutokana na hofu siku ya fazaa kubwa, na humfanya mtoa sadaka asipatwe na huzuni
9- *Sadaka ni sababu ya kughufiriwa dhambi na kusamehewa makosa*
10- Sadaka ni miongoni mwa bishara za mwisho mwema na sababu ya dua ya Malaika
11- *Mtoa sadaka ni mbora wa watu, na sadaka thawabu zake ni kwa kila aliyeshiriki*
12- Mwenye kutoa sadaka ameahidiwa kheri nyingi na ujira mkubwa
13- *Kutoa ni miongoni mwa sifa za wacha Mungu, na sadaka ni sababu ya mapenzi ya waja wa Mola kwa mtoa sadaka*
14- Sadaka ni ishara miongoni mwa ishara za ukarimu na alama miongoni mwa alama za ukarimu na wema
15- *Sadaka ni sababu ya kukubaliwa dua na kuondoshewa matatizo*
16- Sadaka inaondoa balaa na inaziba milango sabini ya mabaya ya dunia
17- *Sadaka inazidisha umri na mali, na ni sababu ya riziki na nusra*
18- Sadaka ni ponya, dawa, na shifaa
19- *Sadaka inazuia moto, gharika, wizi, na inazuia kifo kibaya*
20- Sadaka ujira wake ni ule ule japo ukitoa kwa wanyama au ndege..
*🌴Na sadaka bora ni ile unayoifanya sasa.. ni kueneza maneno haya kwa nia ya sadaka kwani kila anayetekeleza maneno haya na akawafundisha wanaokuja, basi ujira wake uko kwa Mola wake kwa idhini yake*🌴