29/09/2021
TAFAKURI
Karibu tujifunze lugha adhimu na adimu ya Kiswahili
Uhusiano wa Sintaksia na Matawi mengine ya Isimu
Dhana ya sintaksia imejadiliwa na wanazuoni mbalimbali ;
Massamba na wenzake (1999:34) anasema “sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipasho vyake”. Wanaendelea kusema, utanzu huu huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika.
Habwe na Karanja (2004) wanasema “sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi nyingine zinazounda sentensi k**a vile kategoria za maneno, vikundi na vishazi”
TUKI (2004)anasema “sintaksia ni tawi la isimu linaloshughulikia uchanganuzi wa taratibu na kanuni za mahusiano baina ya maneno katika tungo” kwa ufupi sintaksia ni tawi la isimu ambalo linachunguza muundo wa tungo pamoja na uhusiano wa vipashio hivyo vinavyounda tungo ambayo ni nukta pacha, neno, kirai na kishazi.
Kwa ujumla sintaksia ni tawi la isimu ambalo linahusu namna maneno yanavyoungana na kuhusiana kirai, kishazi na sentensi. Sintaksia inachunguza namna maneno yanavyojipanga katika sentensi kwa kuzingatia kanuni za sarufi ya lugha husika.
Kwa hiyo kutokana na kwamba sintaksia pia ni kitengo mojawapo kinachounda maarifa ya lugha, kwamba, sintaksia haiwezi kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha kutokana na uhusiano mkubwa uliopo baina ya vitengo hivi. Vitengo hivi hutegemena na kuathiriana. Hivyo basi tunaweza kuonesha jinsi sintaksia isivyoweza kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha yaani fonolojia, mofolojia na semantiki k**a ifuatavyo:
Uhusisno uliopo kati ya sintaksia na fonolojia.
Massamba na wenzake (1999:34) wanasema “fonolojia ni uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha mahususi” Ni jinsi ambavyo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika k