08/08/2026
Jumuiya ya Wanafunzi Waliosoma Pugu, PUGU SECONDARY SCHOOL ALUMNI, wamelenga kukusanya Shilingi milioni 325 kwa ajili ya kuchangia ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya shule. Mchango huo pia utasaidia kuboresha mazingira ya wanafunzi wenye mahitaji maalum, wakiwemo zaidi ya wanafunzi 130 wanaohitaji mazingira rafiki na salama zaidi ya kujifunzia.
Fedha zitakazokusanywa zitatumika katika:
* Ukarabati wa jengo la Zahanati ya Shule;
* Ukarabati wa jengo la Ofisi ya Taaluma;
* Kukamilisha ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la shule.
Mbali na fedha, kampeni hii pia inapokea vifaa vya ujenzi na ukarabati, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum (Vitimwendo, Fimbo maalumu za kutembelea, mafuta maalum kwa wenye ulemavu wa ngozi, Kompyuta, Vishikwambi n.k) pamoja na vifaa na thamani za ofisini na hospitalini, kulingana na mahitaji ya shule.
Kampeni ya kuchangisha fedha na vifaa inaendelea hadi mwezi Oktoba 2026, ambapo kilele chake kitakuwa Pugu Alumni Day 2026, itakayofanyika tarehe 14 Oktoba 2026 katika viwanja vya shule. Siku hiyo itaenda sambamba na maadhimisho ya Nyerere Day, tukienzi na kukumbuka urithi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye pia aliwahi kuwa Mwalimu wa PUGU BOYS SECONDARY AND HIGH SCHOOL
PUGU SECONDARY SCHOOL ALUMNI wanawakaribisha wahitimu wote wa Pugu, pamoja na wazazi, marafiki, wadau, vyombo vya habari, makampuni, taasisi na mashirika mbalimbali, kuungana nasi katika kuenzi urithi wa Pugu kwa kuchangia maendeleo ya kizazi cha sasa na kijacho.
CHANGIA LEO KUPITIA:
Jina la Akaunti: Pugu Secondary Alumni Group
CRDB Akaunti: 10355320109
Lipa Namba (CRDB): 118168695
Jina: Pugu Secondary Alumni
Unaweza pia kuchangia kwa kuscan QR Code, au kuwasiliana moja kwa moja na viongozi wa Jumuiya kwa ajili ya kuwasilisha michango isiyo ya fedha taslimu, ikiwemo vifaa vya ujenzi, ukarabati na vifaa vingine vinavyohitajika.
MAWASILIANO:
Mwenyekiti: +255 766 029 345
Makamu Mwenyekiti: +255 757 686 331
Katibu Mkuu: +255 767 054 942
Naibu Katibu Mkuu: +255 688 899 652
Mtunza Hazina: +255 655 115 552
PUGU ALUMNI
Brother of the Nation, Sons of Legacy