Maktaba Hekima

Maktaba Hekima Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Maktaba Hekima, Education, Bunda.

"Unlock ur golden doors using pure heart that pumps useful ideas to minds so that u can learn more, do more and never give up even when u are failing more" Solonya

20/04/2025

Power of thoughts

*JE, WAJUA KWANINI KUNA ONGEZEKO KUBWA SANA LA UTUMIAJI WA MIWANI SIKU HIZI?*  Tafsiri ya neno Miwani:  Ni kifaa cha msa...
24/09/2024

*JE, WAJUA KWANINI KUNA ONGEZEKO KUBWA SANA LA UTUMIAJI WA MIWANI SIKU HIZI?*

Tafsiri ya neno Miwani:
Ni kifaa cha msaada wa kuona kinachotumiwa na watu wenye matatizo ya macho au mara nyingine K**a urembo tu.

➡️Kwa kawaida, miwani ina lenzi za aina mbili za Kioo au Plastiki zinazoshikwa na Fremu.

✅Je, Shirika la Afya duniani Linasema Nini kuhusu matatizo ya macho na utumiaji wa miwani.

➡️Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa matatizo ya macho ni moja ya changamoto kubwa za kiafya duniani.

➡️Zaidi ya watu bilioni 2 duniani kote wana matatizo ya kuona, na kati ya hao zaidi ya watu bilioni 1 hawana huduma za kutosha za matibabu.

➡️WHO inabainisha kuwa uwepo wa matatizo mengi ya macho ndio chanzo kikuu cha ongezeko la utumiaji wa miwani.

➡️ *Sababu za Utumiaji Miwani kwa Ujumla ni Pamoja na:*

*1. Matatizo Ya Macho*

Kuongezeka kwa Matatizo ya macho hasa yenye kusababisha utumiaji wa miwani kumesababisha ongezeko kubwa duniani lautumiaji wa miwani.

🔅 Matatizo yanaoongoza kusababisha utumiaji wa miwani kwa watu wengi zaidi ni pamoja na;
1️⃣Myopia (kutoona mbali)
2️⃣Hyperopia (kutoona karibu)
3️⃣Astigmatism, na
4️⃣Presbyopia (kupungua kwa uwezo wa kuona karibu kwasababu za Umri zaidi 40yrs)

*2. Ulinzi Wa Macho*

Miwani maalumu zipo kwa ajili ya ulinzi wa macho kwa baadhi ya wagonjwa wa macho na baadhi ya wale wanaotumia miwani ili kusaidia kulinda macho dhidi ya miale ya jua yenye madhara (UV rays).

🔅Pia, kuna miwani maalum kwa ajili ya kazi k**a vile kuchomelea vyuma au michezo K**a yakuogelea nk.

*3. Urembo Na Mitindo*

Watu wengine huvaa miwani k**a sehemu ya mtindo wao wa mavazi na urembo.

➡️ *Kwanini Matumizi Ya Miwani Yameongezeka Sana?*

🚫 Kuongezeka kwa matumizi ya vifaa vya kielektroniki hasa simu, TV na Tanakilishi(Kompyuta)

🔅 Matumizi ya mda mwingi kupita kiasi ya vifaa hivi yanahusishwa kusababisha kutokuona mbali (myopia) kwa watoto na vijana.

🔅Pia huusishwa na ugonjwa wa macho kukauka, mkazo wa macho na mkao mbaya wa kichwa na shingo ambao unaweza kusababisha maumivu ya kichwa na macho vya mara kwa mara.

🚫 Ongezeko la watu wengi kufanya vipimo vya macho mara kwa mara na kuvaa miwani inapohitajika.

🚫 Kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira na miale ya jua yenye madhara kumechangia ongezeko la matumizi ya miwani.

🚫 Changamoto za kiumri zaidi ya miaka 40

🔅Hii kitaalam huitwa presbyopia, hili sio gonjwa Ila tu nichangamoto ambayo huwapata watu wa zaidi ya Umri wa miaka 40

🔅Ufikishapo Umri huo lenzi za macho huanza kuchoka nakuanza nakupoteza nguvu zake zakuona karibu.

🔅Dalili kubwa ni mtu wa Umri huo ukishindwa kusoma maandishi kwenye kitabu ambapo zamani alikuwa anauwezo huo.

➡️ *Namna Ya Kukabili Tatizo la Matumizi Ya Miwani*

🔅Punguza muda wa kutumia vifaa vya kielektroniki hasa simu na TV au kompuya

🔅K**a kazi yako inakuhitaji umtumie vifaa hivi kwa mda mrefu basi wakati wa vifaa hivi miwani maalum ya kuzuia mwanga wa bluu.

✅ Fanya uchuguzi wa macho yako angalau mara moja kwa mwaka, ili kugundua matatizo mapema na kupata matibabu sahihi.

🔅 Kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya ya macho k**a vile vitamini A, C, na E.

✅ *Vyakula Vyenye Vitamini A:* Husaidia macho kutengeneza pigment zinazosaidia uoni

🔅Vyakula hivi ni pamoja na;
1. Karoti
2. Viazi vitamu (Vina kiasi kikubwa zaidi)
3. Maini
4. Maembe
5. Spinachi, zina kiasi kikubwa Cha kemikali aina ya lutein na zeaxanthin, ambayo ina idadi kubwa ya antioxidants kali ambayo inaweza kusaidia kuzuia kuzorota kwa seli za uoni kadri Umri unapoongezeka.

🔅 *Vyakula Vyenye Vitamini C :* Vina antioxidants Kali ambazo hupunguza seli za Uoni Kufa Mapema.
1. Machungwa na jamii yake
2. Limao na jamii zake
3. Papai
4. Broccoli
5. Pilipili hoho
6. Mapera (Kiasi kikubwa Zaidi machungwa na limao).

🔅 *Vyakula Vyenye Vitamini E:* Vina antioxidants Kali ambazo hupunguza seli za uoni kufa mapema.

1. Karanga
2. Mlozi (Almonds)
3.Mbegu za alizeti
4. Mafuta ya alizeti
5. Avocado 🥑

✅ Kutumia muda mrefu ukisoma au kuangalia simu kunaweza kusababisha mkazo katika macho, macho makavu na maumivu ya kichwa.

➡️ *FANYA YAFUATAYO KUPUNGUZA ATHARI HIZI*

Kwa kutumia sheria ya 20 - 20 - 20 kusaidia macho yako:

🖥️ Baada ya kutumia skrini kwa dakika 20

📏 Angalia kitu kilicho umbali wa futi 20(6m)

🕓Angalau Kwa sekunde 20

➡️ *ZINGATIA HILI*

🔅Neno macho limetajwa zaidi ya 471, likielezea yote macho ya nyama na roho

🔅Kulinda macho yako ya mwili na roho pia ili tueze kuona frusa nyingi kiroho nazile zikuzungukazo.

🔅 Mwanzo 21:19
Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji. Akaenda akajaza kiriba maji nakumnywesha kijana.

Mungu awabariki nyote 🙏

Somo limeandaliwa na Daniel Solonya kupitia Maktaba Hekima

JE UNATAKA AFYA BORA?HILI HAPA JAMBO LILILO SAHAULIKA KATIKA AFYA.➡️Usingizi ni hali ya mwili na akili kupumzika ili kur...
24/09/2024

JE UNATAKA AFYA BORA?

HILI HAPA JAMBO LILILO SAHAULIKA KATIKA AFYA.

➡️Usingizi ni hali ya mwili na akili kupumzika ili kurejesha nguvu.

📚Wakati wa usingizi, mwili hufanya kazi muhimu k**a vile

✅Kurekebisha seli

✅Kuimarisha mfumo wa kinga, na

✅Kuimarisha kumbukumbu na kujifunza.

✅Usingizi ni muhimu kwa afya ya mwili na akili.

✅Ukosefu wa usingizi unaweza kuathiri vibaya afya kwa ujumla.

📚Umuhimu wa Usingizi (Kiufupi)

✅Kurejesha Nguvu za Mwili, Wakati wa usingizi, mwili hufanya kazi ya kurekebisha misuli, viungo, na seli.

✅Usingizi mzuri ni muhimu kwa afya ya akili

✅Kuimarisha kumbukumbu.

✅Usingizi hupunguza Msongo wa Mawazo na kuboresha hali ya hisia.

📚Madhara ya Ukosefu wa Usingizi:

✅Huongeza hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi.

✅Huongeza hatari ya kupata uzito kupita kiasi kutokana na mabadiliko ya homoni zinazodhibiti njaa.

✅Hudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili, na hivyo kuongeza hatari ya kupata magonjwa.

✅Ukosefu wa usingizi unaweza kusababisha matatizo k**a vile wasiwasi, unyogovu, na matatizo ya kumbukumbu.

✅Kwa wanafunzi kutopata usingizi wa kutosha hupunguza usikivu ( concentration)

📚Je nilale kwa masaa mangapi ili kuleta afya?

✅Masaa ya kulala yanatofautiana kulingana na umri watoto wanahitaji kulala sana kwasababu wakati wa usiku vichocheo vya ukuaji ndio huzalishwa kwa wingi ( growth Hormone production )

Umri Masaa
0- 1 12-16 hrs
1-2 11-14 hrs
3-5 10-13 hrs
6-12 9-12 hrs
13-18 8-10 hrs
18+ 6-8 hrs

Hivyo Lala kulingana na umri wako

📚Je, wajua ufanye Nini Kupata Usingizi Mzuri?

✅Tengeneza ratiba ya maalum ya kulala na kuamka kwa wakati ule ule kila siku, hata K**a ni wikendi.

✅Fanya mazoezi mara kwa mara lakini pia epuka kufanya mazoezi hasa magumu masaa masaa machache karibu na muda wa kulala.

✅Usile chakula na kwenda kulala papo gapo mana hiyo ifanya uote ndoto mbaya na kukosa usingizi

✅Lala kwenye Chumba Chenye Giza na Utulivu

✅Joto la chumba linapaswa kuwa la wastani, si baridi sana wala joto sana.

✅Usilale na nguo zinazokubana sana hizo zitafanya mzunguko wa damu kutokuwa vizur.,

🤷Wanaume tusilale tukiwa tumejifunga mikanda Tanzania hakuna vita.

✅Kitandani siyo sehemu ya kutumia simu maliza mambo yako ukifika kitandani Lala

✅Fanya kazi wengi hukosa usingizi kwa sababu akili haitumiki hawafanyi kazi hivyo hutafuta sana usingizi kwa sababu hakuna kinachochochea usingizi

📚ZINGATIA

✅Ni kweli Mungu anahitaji tufanye kazi kwa bidii na kupata vitu vyetu wenyewe
Mahubiri 9:10

✅Bwana ametupa nafasi ya kupumzi ndio mana amempa usingizi kwa kila mtu na ametoa siku moja ya juma kila mtu apumzike hebu hakikisha unafanya hivyo

✅Kulala sana ni uvivu na inaweza kuleta changamoto kwa afya yako acha kutumia masaa mengi kitandani muda mwingine hata hujalala.

Mungu awabariki nyote 🙏

Somo limeandaliwa na Daniel Solonya kupitia Maktaba Hekima

18/09/2024
16/09/2024

"Asilimia kubwa ya adui zako ni watu uliowahi kuwa nao karibu na wengine ni wale uliowahi kuwasaidia"
wisdom

📚HOMA YA INI "A" (HEPATITIS A)➡️Imeandaliwa na Daniel Solonya chini ya Maktaba Hekima Kumbuka kushare watu wengine wajif...
16/09/2024

📚HOMA YA INI "A" (HEPATITIS A)

➡️Imeandaliwa na Daniel Solonya chini ya Maktaba Hekima
Kumbuka kushare watu wengine wajifunze pia🙏

➡️Somo hili ni mwendelezo wa somo ya kwanza kuhusu homa Kali ya ini na ambayo ndio hatari zaidi ya hizi, hivyo nashauri ukasome nasomo la kwanza kwa uelewa mzuri zaidi

➡️Mtu asiye na maambukizi na asie na Kinga ya Virusi vya hepatitis A (HAV) huambukizwa virusi hawa kwa kumeza chakula au maji yaliyochafuliwa (kwa kinyesi cha binadamu alieathirika na virusi hawa) au kwa kugusana moja kwa moja na mtu aliyeambukizwa.

➡️Hivyo hatari kubwa ipo maeneo yenye ukosefu wa maji salama na hali duni ya usafi binafsi na hasa usafi wa mikono na ngono pia (oral-anal s*x).

➡️Watoto wengi (90%) wameambukizwa virusi vya hepatitis A kabla ya umri wa miaka 10.

➡️Mara nyingi maambukizi haimaanishi ugonjwa kila wakati kwa sababu wengi walioambukizwa hawapati dalili zozote zinazoonekana.

➡️Kwa kawaida huchukua siku 14 hadi 28 Baada ya maambukizi kuanza kuonesha dalili K**a homa, mwili kuchoka, kukosa hamu ya kula, kuhara, kichefuchefu, usumbufu wa tumbo, mkojo wa rangi nyeusi, macho na ngozi kuwa njano.

➡️Licha yakuwa hakuna tiba maalum ya Aina hii ya homa ya ini lakini watu wengi hupona kikamilifu kutokana na hepatitis A, nakupata kinga ya maisha yote.

➡️Na idadi ndogo hufa kutokana na kufeli kwa ini. Chanjo salama na yenye ufanisi inapatikana ili kuzuia homa hii ya ini.

📚HOMA YA INI "D" (HEPATITIS D)

➡️Virusi vya Hepatitis D (HDV) ni virusi vinavyohitaji virusi vya hepatitis B (HBV) ili viweze kuzaliana.

➡️Hivyo maambukizi ya HDV hutokea pekee wakati ambao mtu anapoambukizwa na hepatitis B na D kwa wakati mmoja (maambukizi ya pamoja) au kupata hepatitis D baada ya kuambukizwa kwanza na hepatitis B (maambukizi mengi).

➡️Idadi ya watu ambao wana uwezekano mkubwa wa kuwa na maambukizi ya pamoja ya HBV na HDV ni pamoja na watu wa kiasili, wanaopokea hemodialysis na watu wanaojidunga dawa.

➡️Ulimwenguni kote, idadi ya maambukizo ya HDV imepungua tangu miaka ya 1980, kutokana na mpango wa kimataifa wa chanjo ya HBV yenye mafanikio.

➡️Mchanganyiko wa maambukizo ya HDV na HBV inachukuliwa kuwa aina kali zaidi ya homa ya ini ya virusi sugu kutokana na kuendelea kwa kasi kuelekea kifo kinachohusiana na ini na saratani ya ini.
➡️Maambukizi ya Hepatitis D yanaweza kuzuiwa kwa chanjo ya hepatitis B, lakini viwango vya mafanikio ya matibabu ni vya chini.

📚HOMA YA INI "E" (HEPATITIS E)

➡️Kila mwaka kuna wastani wa maambukizo ya HEV milioni 20 duniani kote.

➡️World Health Organization (WHO) inakadiria kuwa homa ya ini ya ini E ilisababisha takriban vifo 44,000 mwaka 2015 (ikiwa ni asilimia 3.3 ya vifo vinavyotokana na virusi vya homa ya ini).

➡️Virusi huambukizwa kupitia njia ya kumeza chakula au maji yalioathiriwa na kinyesi cha mgonjwa wa HE. Hepatitis E inapatikana duniani kote, lakini ugonjwa huo ni wa kawaida katika baadhi ya sehem hasa Mashariki na Kusini mwa Asia.

➡️Chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya hepatitis E imetengenezwa na imepewa leseni nchini Uchina, lakini bado haijapatikana kwingineko.

Mwisho🙏

🩺 UGONJWA HATARI WA HOMA YA INI✅Ukimaliza kusoma share kwa watu wengine wajifunze pia 📚kazi kuu ya ini ni nini? ✅Ini ndi...
16/09/2024

🩺 UGONJWA HATARI WA HOMA YA INI

✅Ukimaliza kusoma share kwa watu wengine wajifunze pia

📚kazi kuu ya ini ni nini?

✅Ini ndio kiungo cha pili
kwa ukubwa Baada ya ngozi katika mwili wa binadam. Ini hufanya kazi zaidi ya 500 mwilini, huku kazi ake kuu ikiwa nikupambana na sumu mwilini.

📚Homa ya ini ni nini?

Homa ya ini humaanisha kuvimba kwa ini.

📚Homa ya ini husababishwa na nini?

Homa ya ini hutokana na sababu mbalimbali zakuambuakizika na zisizo ambukizika.

➡️Miongoni mwa sababu hizo, virusi vya homa ya ini au hepatitis virus 🦠 ndio huongoza kwa kusababisha homa ya ini yenye kuambukizika, Visababishi vingine ni pamoja na :

➡️Pombe

➡️Dawa

➡️Kemikali

➡️Kasoro zakuzaliwa hasa zakushindwa kuchakata madini ya chuma na kopa.

📚Leo tutajifunza kwaundani juu ya homa ya ini yenye kusababishwa na virusi vya homa ya ini (Hepatitis virus)

📚Kuna Aina kuu ngapi za Virusi vya homa ya ini?

➡️Kuna Aina kuu Tano(5) za virusi vya homa ya ini (Hepatitis virus A, B, C, D & E) vyenye uwezo wa kusababisha homa ya ini.

➡️ Lakini virusi hawa hutofautiana kwenye njia za uambukizaji, ukali wa homa ya ini, na njia zakujikinga.

📚Virusi wapi wa homa ya ini nihatari zaidi ya wengine?

➡️Miongoni mwa virusi hawa, Virusi vya Homa ya ini B na C(HVB and HVC) ndio virusi hatari zaidi ambao husababisha homa kali ya ini kwa watu zaidi ya million 350 duniani kote, saratani ya ini na vifo vingi vitokanavyo na homa ya ini.

📚NI ZIPI DALILI ZA HOMA YA INI KWA UJUMLA?

Hizi ni dalili za ujumla za aina zote za homa ya ini:
➡️Homa(kupanda kwa jotoridi la mwili zaidi ya 37.0 C

➡️ Kuhara tumbo maumivu ya tumbo

➡️Maumivu ya maungio
➡️ Njano ya ngozi na macho
➡️Mkojo mweusi
➡️Hisia ya uchovu sana
➡️ Kichefuchefu
➡️Kutapika
➡️Kufeli kwa ini kwenye Kazi zake,kupelekea kifo

🔰Leo tutazungumzia aina moja tu ya ugonjwa wa Ini somo lijalo tutazungumzia namna gani tunaweza kujikinga

📚HOMA YA INI "B" (HEPATITIS B)

🩺WHO inakadiria Kuna maambukizi mapya milioni 1.2 kila mwaka. Mnamo 2022,

🩺Homa ya ini ya B ilisababisha vifo vinavyokadiriwa kufikia milioni 1.1, hasa kutokana na ugonjwa wa cirrhosis na saratani ya ini.

🩺Homa hii ya ini husababishwa na Virusi Aina ya Hepatitis B (HVB).

📚Namna gani mtu anaweza kupata Hepatitis B ?

➡️ Virusi hivi mara nyingi hupitishwa kutoka kwa mama hadi kwa mtoto wakati wa kuzaliwa na kuzaa

➡️Kwa kugusa damu au Kuongezewa damu isio pimwa

➡️Kugusa mate

➡️Kugusa vimiminika vingine vya mwili wakati wa kujamiiana na
mwenzi aliyeambukizwa

➡️Kuchangia vitu vyenye ncha Kali K**a sindano,

➡️Maambukizi kwanjia ya ngono yapo zaidi kwa watu ambao hawajachanjwa na wapenzi wengi wa ngono.

➡️Mara nyingi maambukizi wakati wa utotoni ndio husababisha homa ya ini ya kudum mda mrefu( 95%).

➡️Virusi vya hepatitis B vinaweza kuishi nje ya mwili kwa angalau siku 7

➡️Baada ya maambukizi ya virusi vya hepatitis B huchukua kati ya siku 30 hadi 180 kuanza kuonesha dalili.

➡️Licha ya uhatari wa homa hii ya ini lakini Watu wengi hawaoneshi dalili zozote wanapoambukizwa.

➡️Nahivyo hueza kuambukiza Watu wengi zaidi pasipo kufaham. Watu wengine huonesha dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa

📚Je mtu aliyepata maambukizi anaweza kupona tena ?

➡️Ingawa watu wengi wenye hepatitis ya mda mfupi hupona lakini baadhi yao wenye hepatitis B sugu hupata ugonjwa wa ini unaoendelea na matatizo k**a vile cirrhosis na saratani ya ini nahatimae kupoteza maisha.

➡️Hepatitis B inaweza kuzuiwa kwa chanjo ambazo ni salama, zinapatikana na zinazofaa.

➡️Hakuna tiba ya homa hii ya ini isipokuwa tu hueza kuzuilika kwa chanjo ambayo hutewa kwa mtu pekee asie na maambukizi.

➡️Chanjo itakulinda dhidi ya hepatitis B kwa angalau miaka 20 na pengine kwa maisha yote.

➡️Watu 8 Kati ya watu 100 wenye hepatitis B wanamaambukizi ya Virusi vya Ukimwi duniani.

📚HOMA YA INI "C" (HEPATITIS C)

➡️Hii ni homa ya ini isababishwayo na Virusi vya hepatitis C.
➡️Virusi hivi vinaenezwa kwa njia kuu ya kugusa damu ya mtu alieathirika na Virusi hawa.
➡️Maambukizi mengi hutokea kwa kuathiriwa na damu kutoka kwa njia zisizo salama za kutumia vitu vya ncha Kali k**a sindano, kuongezewa damu bila uchunguzi, kuchangia sindano wakati wa matumizi ya dawa za kulevya na kwanjia ya ngono(kwa mfano, watu wenye wapenzi wengi na kati ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume).

➡️Pia hueza kuambukizika kutoka kwa mama aliyeambukizwa hadi kwa mtoto wake hata hivyo, njia hizi za uambukizaji si za kawaida.

➡️Hepatitis C haienezwi kupitia maziwa ya mama, chakula, maji au mguso wa kawaida k**a vile kukumbatia, kumbusu na kushiriki chakula au vinywaji na mtu aliyeambukizwa.

➡️WHO inakadria kuwa takriban watu milioni 50 wana maambukizi ya virusi vya homa ya ini sugu ya C, huku takriban maambukizi milioni 1.0 hutokea kwa mwaka. mnamo 2022, takriban watu 242 000 walikufa kutokana na hepatitis C, wengi wao wakiwa kutokana na cirrhosis na saratani ya ini.

➡️Maambukizi ya papo hapo ya HCV kawaida hayana dalili na mengi hayaleti ugonjwa wa kutishia maisha.

➡️Takriban 30% (15-45%) ya watu walioambukizwa huondoa virusi kwa hiari ndani ya miezi 6 baada ya kuambukizwa bila matibabu yoyote.

➡️Asilimia 70 iliyobaki (55-85%) ya watu hupata maambukizi ya muda mrefu ya HCV. Kati ya wale walio na maambukizo sugu ya HCV, hatari ya ugonjwa wa cirrhosis ni kati ya 15% hadi 30% ndani ya miaka 20.

➡️Dawa za kuzuia virusi zinazofanya kazi moja kwa moja zinaweza kutibu zaidi ya 95% ya watu walio na maambukizi ya hepatitis C, lakini upatikanaji wa utambuzi na matibabu ni mdogo.

➡️Kwa sasa Hakuna chanjo yenye ufanisi dhidi ya hepatitis C. Njia bora ya kuzuia ugonjwa huo ni kuepuka kuambukizwa virusi hawa.

📝Usikose kufuatana nasi somo lijalo kuhusu homa ya ini isababishwayo na Virusi wa homa ya ini Aina A, D na E

Imeandaliwa na
Daniel Solonya chini ya Maktaba Hekima

Tanzania bila ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi inawezekana🌍🙏
16/09/2024

Tanzania bila ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi inawezekana🌍🙏

Nyakati zenye furaha K**a hizi ni chache maishani ukizipata ziishi haswaa
12/09/2024

Nyakati zenye furaha K**a hizi ni chache maishani ukizipata ziishi haswaa

Hata mbuyu ulianza K**a mchicha, can't wait 🙏
12/09/2024

Hata mbuyu ulianza K**a mchicha, can't wait 🙏

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Mulla Oscer, Jofrey Frugance Mangoma, Tz Chusseboy, Siraj...
31/08/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Mulla Oscer, Jofrey Frugance Mangoma, Tz Chusseboy, Siraji Bakari, Elizabeth Elisha, Minza Tumaini, Mohamed Dickson, Hristina Zegge, Happy John

Are you this person?
29/08/2024

Are you this person?

Address

Bunda

Telephone

+255696932946

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maktaba Hekima posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Maktaba Hekima:

Shortcuts

Share

Category