Bitale Secondary School

Bitale Secondary School Hii ni page ya shule ya sekondari Bitale iliyopo mkoani Kigoma katika kijiji cha Bitale kilomita 20 kutoka Kigoma mjini.

25/02/2025
Maendeleo ya ukamilishaji wa mabweni kwa ajili ya kidato Cha tano
20/02/2025

Maendeleo ya ukamilishaji wa mabweni kwa ajili ya kidato Cha tano

Shule ya Sekondari Bitale tukizindua unywaji wa uji wa Mchele kwa wanafunzi.
01/05/2024

Shule ya Sekondari Bitale tukizindua unywaji wa uji wa Mchele kwa wanafunzi.

Taswira mbalimbali katika Ufundaji wa wanafunzi wa kiume ambao ulifanywa na walimu wa kiume shule ya Sekondari Bitale. U...
20/03/2024

Taswira mbalimbali katika Ufundaji wa wanafunzi wa kiume ambao ulifanywa na walimu wa kiume shule ya Sekondari Bitale. Ufundaji huo uliangazia Afya kwa vijana balehe, mabadiliko katika kipindi Cha balehe, changamoto wanazokumbana nazo vijana balehe, mambo yanayochangia mabadiliko ya tabia, usafi, kujihusisha na ngono, madhara ya ngono, ulawiti pamoja na madhara yake, punyeto pamoja na madhara yake.

Michezo ni Afya, michezo ni burudani, michezo uchangamsha akili, michezo ujenga urafiki na mahusiano mazuri.
23/02/2024

Michezo ni Afya, michezo ni burudani, michezo uchangamsha akili, michezo ujenga urafiki na mahusiano mazuri.

Wanafunzi wa kidato Cha kwanza, Cha pili na Cha tatu wakipatiwa zawadi kwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
07/10/2023

Wanafunzi wa kidato Cha kwanza, Cha pili na Cha tatu wakipatiwa zawadi kwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

TANGAZO KWA UMMAUONGOZI WA SHULE UNAFANYA MCHAKATO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE KWA KUPANDA MITI, MAZAO YA MATUNDA NA...
27/05/2023

TANGAZO KWA UMMA

UONGOZI WA SHULE UNAFANYA MCHAKATO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA SHULE KWA KUPANDA MITI, MAZAO YA MATUNDA NA MAUA MBALIMBALI YA KUVUTIA. HIVYO WANANCHI MNAOMBWA KUFANYA YAFUATAYO:-
1. SI RUHUSA KUINGIA AU KUPITA KATIKA MAENEO YA SHULE KWA NJIA ZISIZO RASMI.

2. SI RUHUSA KUINGIZA MIFUGO K**A MBUZI, KONDOO AU NG'OMBE KWENYE ENEO LA SHULE.

3. MNASHAURIWA KUCHUNGA MIFUGO MBALI NA MAZINGIRA YA SHULE. MFUGO UKIK**ATWA NDANI YA ENEO LA SHULE MMILIKI ATATOZWA FAINI KWA MUJIBU WA SHERIA.

KWA PAMOJA NAOMBA TUSHIRIKIANE KULINDA MAZINGIRA YA SHULE YETU KWA KIZAZI CHA SASA NA BAADAE.

ASANTENI KWA USHIRIKIANO.

17/03/2023
Leo ni Siku ya KIFUA KIKUU DUNIANI 24/03/2022Bitale Sec tumekuja na Igizo fupi ktk kuelimisha na kuondokana na imani pot...
24/03/2022

Leo ni Siku ya KIFUA KIKUU DUNIANI 24/03/2022

Bitale Sec tumekuja na Igizo fupi ktk kuelimisha na kuondokana na imani potovu pindi mtu anapougua ugonjwa fulani. Wapo wanaoamini kulogwa kutokana na ukosefu wa elimu juu ya kifua kikuu ni nini, kinaambukizwaje na kinatibikaje. Bitale sec tunasema AFYA NI JUKUMU LAKO NA LANGU KUILINDA. Ukiilinda Afya yako basi umelinda na wengine wanaokuzunguka.

Kifua kikuu (TB) huenezwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mgonjwa ambaye hajaanza matibabu anapokohoa au kupiga chafya vimelea husambaa hewani na mtu mwingine anaweza kuvivuta na kuambukizwa.

Kuna aina mbili za TB:
1. TB inayoathiri mapafu
2. TB inayoathiri sehemu nyingine ya mwili k**a tezi, mifupa, tumbo, uti wa mgongo n.k

Watu walio katika hatari zaidi kuambukizwa na kuugua TB:
1. Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU)
2. Wazee zaidi ya miaka 65
3. Watu walio katika msongamano
4. Watoto wenye umri chini ya miaka 5
5. Watu wenye magonjwa ya muda mrefu k**a vile kisukari, saratani
6. Watu wenye lishe duni mfano utapiamlo
7. Walevi kupindukia

DALILI ZA TB YA MAPAFU
1. Kukohoa kwa muda wa wiki mbili au zaidi
2. Homa za mara kwa mara hasa nyakati za usiku
3. Kutokwa na jasho jingi lisilo la kawaida hasa nyakati za usiku
4. Kupungua uzito au kukonda
5. Kukohoa makohozi yaliyochanganyika na damu

JINSI YA KUJIKINGA NA KUWAKINGA WENGINE:
1. Toa taarifa kwa mzazi/mlezi au mwalimu ukigundua wale wote wenye dalili za TB ili wapelekwe kwenye kituo cha huduma ya Afya kwa uchunguzi na matibabu
2. Funika mdomo na pua wakati wa kukohoa au kupiga chafya
3. Epuka msongamano usiokuwa wa lazima
4. Usiteme mate au makohozi ovyo
5. Tema mate kwenye chombo chenye mfuniko kisha fukia kwenye udongo
6. Fungua madirisha ili mzunguko wa hewa na mwanga uwe wa kutosha
7. Kula mlo kamili wenye virutubisho vya aina zote
8. Chanja dawa ya kinga ya TB mara tu mtoto anapozaliwa

KUMBUKA! Mgonjwa aliyekwisha tumia dawa kwa wiki mbili au zaidi hawezi kuwaambukiza wengine ugonjwa wa TB. Pia TB inatibika na unapona kabisa.


Amref Health Africa Tanzania

Mapema leo kwenye School Baraza
21/02/2022

Mapema leo kwenye School Baraza

Address

Bitale
82

Opening Hours

Monday 07:00 - 15:00
Tuesday 07:00 - 15:00
Wednesday 07:00 - 15:00
Thursday 07:00 - 15:00
Friday 07:00 - 15:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bitale Secondary School posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The School

Send a message to Bitale Secondary School:

Shortcuts

Share

Category